Hoja Binafsi za Zitto na January:Je, Wabunge watalipa visasi

Ndio maana nahoji kama kweli aliwashirikisha wabunge wenzie katika kudraft mapendekezo. Ni lazima tukiri kuwa alifanya utafiti mzuri sana lakini tujue kuwa pale wapo katika mchezo wa siasa na sisi wote tupo katika mchezo wa siasa ndio maana tunajadili haya. kwa kuwa hoja hizi huwasilishwa mapema walikwishaikalia hoja ya Mhe Zitto na kumundalia mb unge atakayetumia Kanuni kuipiga knock technical out hoja yake.
kwa ufahamu wangu mambo yote aliyopendekeza Mhe Zitto ni ndoto za mchana kwa watendaji wa serikali ya CCM ambao hukaa kuvizia posho wakati wote.

Sababu ingine iliyofanya haja hiyo kutupwa ni kashafa zilizoko katika ubinafsishaji wa mashamba ya mkonge mojawapo likiwa shamba alilochukua CHAVDA aliyesababisha Mhe Lyatonga Mrema kuondolea katika baraza la mawaziri. Ndio maana Hoja hii ilitakiwa kukaliwa kweli kweli na kuandaliwa makakati wa pamoja kama chama.

Kwa hilo nipo ukurasa mmoja na wewe. Kwa mtazamo wako, nini kifuate? Zitto asubiri hiyo kamati gani sijui imalize kazi yake kama alivyo adhidi Waziri wa Kilimo? Zitto ajipange tena na hoja yake binafsi? Au Zitto na Chadema kwa ujumla wajipange zaidi kwa kuliweka hili katika bajeti yao ya wizara kivuli ya kilimo hapo mwezi Juni?
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Hoja zote mbili zimetupiliwa mbali kwa maelezo yenye sura mbili:

Moja, hoja hizi hazina umuhimu kwa sasa kwa sababu kuna ground work inayohitajika kufanyika kwanza, na baada ya hapo, ndipo hoja hizi mbili zitakuwa na mashiko.
Mbili, Serikali tayari imekuwa inafanyia kazi mambo mengi ambayo yamewasilishwa na Zitto na Jaruary. Kwa maana nyingine, masuala mengi ndani ya hoja hizo sio mageni kwa CCM na serikali yake kwani tayari yamekuwa yanafanyiwa kazi, mengi yalishajadiliwa na kutolewa maelezo na serikali bungeni katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita lakini vile vile mengi yalikuwepo hata kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM 2010.

Binafsi, naachwa na maswali matatu: JE

  • Kuanguka kwa hoja hizi ni matokeo ya Zitto na January kutofanya home work yao vizuri?
  • Au Kuanguka kwa hoja hizi ni matokeo ya siasa za bunge linalotawaliwa na CCM?
  • Au hizi ni siasa za nyongeza za posho?

Mtamzamo wangu kuanguka kwa hizi hoja za hawa 'Boys II Men' ni salamu kutoka kwa wabunge wa ccm kwamba wasijione kama wao (Zitto na January) ni smarter kuliko wabunge wengine. Inawezekana wanahisi (hasa January) anakitumia chama chake cha ccm kujijenga yeye kisiasa baada ya chama kumfikisha hapo alipo. Whether kuna ukweli kwenye hili au la hayo ni mambo mengine lakini kwa sasa safari imeanza ya kufungana speed governor. CCM wanaweza kuwa na wakati mgumu kwa kutaa hizi hoja lakini wanaweza kuvuka kizingiti kama wakitoa sababu za msingi (kama wanazo).

Zitto naye amekuwa muumini mzuri wa hizi siasa za calculations. Huyu kijana is very smart lakini sina hakika kama approach aliyotumia siku hizi itamfikisha kwenye kiti cha enzi. Kwa kurudia maoni yangu niliyowahi toka huko nyuma naomba niseme, naridhika na Zitto wa Buzwagi era na ninasononeshwa na Zitto wa Blackberry.
 
hoja ya makamba ni contradicting, wote twajua gharama za ujenzi zilivyo juu, na watu wengi hukopa ili kujenga, leo hii utamwambia nin mtu huyu eti kodi ni ya miezi 2 tu maximum...

Hata wenye daladala nao huwa wanakopa ili kununua magari yao.lakini bado wanakuwa controled na sumatra.wewe unaonekana live kuwa ni mmoja kati ya akina BABA MWENYE NYUMBA
 
ccm haina wabunge, ina watu mbumbumbu, mazoba, wasifikiri, watu legelege, wasiofaa, hakika ccm ni kielelezo cha watu duni na mamluki kwa taifa lao.

Kimsingi una hoja lakini nadhani huo umbumbumbu, uzoba, ulegelege n.k, ni wa wabunge wa CCM kitaasisi, sio mbunge mmoja mmoja, kwani wapo wabunge kadhaa wa CCM ambao ni makini sana. Unajua kinachowabana wabunge wengi ni suala la kwenda kinyume na serikali na chama chao cha CCM ambapo adhabu yake ni jina kukatwa na vikao vya chama i.e. NEC, baada ya mchakato wa kura za maoni kugombea ubunge kupitia CCM huko majimboni. Ni hilo tu; vinginevyo wakiruhusu tu suala la mgombea binafsi, mambo mengi sana yatabadilika, kwani kuna wabunge ambao wapo tayari kuachana na CCM lakini hawapo tayari kujiunga na upinzani kama vile Chadema kutokana na historia baina ya vyama hivi viwili humo bungeni. Ndio maana defections nyingi za CCM zikija, wa kufaidika watakuwa vyama kama CCK na NCCR. Naenda nje ya mada lakini mawazo yangu ndio hayo juu ya hilo.
 
Naelewa hoja yako lakini kikubwa hapa ni kwamba tunaelekea bajeti ya 2012-2013, mimi nadhani Zitto angeitumia bajeti ijayo itakayowasilishwa bungeni mwezi June, kama reference wakati wote wa kujenga hoja yake, na hii ingeipa hoja yake nguvu kubwa zaidi - kwa kusema kwamba kutokana na umuhimu wa zao hili....ni matarajio yangu kwamba kuanzia bajeti ya mwaka huu wa fedha, wizara ya kilimo itafanya haya haya na haya kuhusu zao la mkonge;

Iwapo zitto angefanya hayo kwa kulink na bajeti ijayo, waziri angeingia tu mtego wa kutoa ahadi kemkem kwamba watafanya hili na lile kwenye bajeti, then zitto kumsibiria na bajeti yake na kuanza nae upya.

The point is very clear,
linalowezekana leo lisingoje kesho. Its only february, bajeti mpya ni june kwa
ajili ya mwaka 2012/2013, sioni tatizo lolote kwenye hoja ya Zitto kama nia
ingekuwepo. Au kama Serikali ingehitaji kujipanga zaidi, marekebisho yangekuwa
kwenye mwaka tu... lakini tumeona haikuwa hivyo.

Nasikitika kukuambia mchambuzi huyo unayejaribu kumuelimisha ana ugonjwa wa
Zittophobiasis.
 
na kiwanda kilichokuwa Morogoro si hizi kimekuwa nini. Isije ikawa ni kituo cha Mabasi au bohari

Kwa mwendo wa CCM na Serikali yake, inawezekana kabisa kiwanda hicho sikuhizi ni ghala la kuhifadhi unga wa ulezi bila ya wahusika kuchukuliwa hatua kutokana na kwenda kinyume na mkataba wakati wa zoezi la ubinaifshaji.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Wabunge wa CCM sasa wafike mahala pa kikomo hoja zeje tija kwa Taifa wasiziache wazishupalie kuliko kuzikataa
 
The point is very clear,
linalowezekana leo lisingoje kesho. Its only february, bajeti mpya ni june kwa
ajili ya mwaka 2012/2013, sioni tatizo lolote kwenye hoja ya Zitto kama nia
ingekuwepo. Au kama Serikali ingehitaji kujipanga zaidi, marekebisho yangekuwa
kwenye mwaka tu... lakini tumeona haikuwa hivyo.

Nasikitika kukuambia mchambuzi huyo unayejaribu kumuelimisha ana ugonjwa wa
Zittophobiasis.

Upo sahihi kwani kimsingi Zitto stands to be correct both in content (hoja yenyewe) na context (2012); Cha ajabu ni uwendawazimu wa serikali kupinga hoja kwa kwa kujenga hoja inayobebwa zaidi na context (2012), badala ya content (umuhium wa kufufua zao hili haraka iwezekanavyo ili tupate MW 100 za umeme, tutoe ajira kwa vijana, tuongeze pato la uchumi);
 
Mtamzamo wangu kuanguka kwa hizi hoja za hawa 'Boys II Men' ni salamu kutoka kwa wabunge wa ccm kwamba wasijione kama wao (Zitto na January) ni smarter kuliko wabunge wengine. Inawezekana wanahisi (hasa January) anakitumia chama chake cha ccm kujijenga yeye kisiasa baada ya chama kumfikisha hapo alipo. Whether kuna ukweli kwenye hili au la hayo ni mambo mengine lakini kwa sasa safari imeanza ya kufungana speed governor. CCM wanaweza kuwa na wakati mgumu kwa kutaa hizi hoja lakini wanaweza kuvuka kizingiti kama wakitoa sababu za msingi (kama wanazo).

Zitto naye amekuwa muumini mzuri wa hizi siasa za calculations. Huyu kijana is very smart lakini sina hakika kama approach aliyotumia siku hizi itamfikisha kwenye kiti cha enzi. Kwa kurudia maoni yangu niliyowahi toka huko nyuma naomba niseme, naridhika na Zitto wa Buzwagi era na ninasononeshwa na Zitto wa Blackberry.

Umenena masuala ya msingi sana ambayo kimsingi ndiyo yanatakiwa kutoa mwongozo mkubwa sana kwenye mada hii juu ya kwanini wamekwama na hatima yao ni nini katika vyama vyao na siasa za Tanzania kwa ujumla, kwa kuzingatia both, vyama husika, lakini pia the electorate.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Wadau kumbukeni mashamba yote ya mkonge yalishauzwa wa wawekezaji uchwara ambao wameshindwa kuyaendeleza. Na wengine ni viongozi ndani ya serikali. Hoja hii ingepita, ingeibua madhambi mengine yaliyojificha kwenye sekta ya kilimo cha mkonge.
.

Hapo kwenye red nadhani ndio pa kuanzia. Kwanza ku-idenfity mashamba ya mkonge yalipo na nani anamiliki shamba lipi? Nahisi kuna kitu hapa sio bure!
 
Leo, hoja ya Zitto kuhusu mkakati maalum wa kufufua zao la mkonge na ile ya January kuhusu umuhimu kulinda wapangaji zinawasilishwa bungeni. Je zitapita? Kwa mtazamo wangu, kuna uwezekano mkubwa kwamba, pamoja na umuhimu wa hoja hizi mbili, hoja hizi zitakwama, sababu kubwa ikiwa ni hasira ya wabunge juu ya msimamo wa Zitto na January kupinga ongezeko la posho.
siamin baba anaweza kataa neema kwa wanae ila leo baba amekataa maendeleo jimboni kwake kwa madai serikali haiko tayari ni kweli ama 'cake eaters' hawako tayari kulinda maslahi yao???
 
Hoja zote mbili zimetupiliwa mbali kwa maelezo yenye sura mbili:

Moja, hoja hizi hazina umuhimu kwa sasa kwa sababu kuna ground work inayohitajika kufanyika kwanza, na baada ya hapo, ndipo hoja hizi mbili zitakuwa na mashiko.
Mbili, Serikali tayari imekuwa inafanyia kazi mambo mengi ambayo yamewasilishwa na Zitto na Jaruary. Kwa maana nyingine, masuala mengi ndani ya hoja hizo sio mageni kwa CCM na serikali yake kwani tayari yamekuwa yanafanyiwa kazi, mengi yalishajadiliwa na kutolewa maelezo na serikali bungeni katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita lakini vile vile mengi yalikuwepo hata kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM 2010.

Binafsi, naachwa na maswali matatu: JE

  • Kuanguka kwa hoja hizi ni matokeo ya Zitto na January kutofanya home work yao vizuri?
  • Au Kuanguka kwa hoja hizi ni matokeo ya siasa za bunge linalotawaliwa na CCM?
  • Au hizi ni siasa za nyongeza za posho?

Kuna mambo mengi ambayo serikali ilishasema inayafanyia kazi lakini muda mwingi unapita bila matokeo kujulikana; ina maana mbunge akileta hoja juu ya jambo hilo haikubaliki?
Je hoja ikukubaliwa na kujadiliwa si serikali itakuwa imepata input nyingine katika utekelezaji!
Kwa maoni yangu hoja hizi zimehusishwa na suala la posho.
 
Wabunge wa CCM wanaongozwa na ilani ya chama chao ambayo haiwezi kumletea mtanzania maendeleo na kumtoa mwananchi kwenye lindi la umaskini.

Nenda kajisaidie ukirudi utakuwa na mawazo mazuri zaidi kwani waonyesha kuna kitu kinakusumbua

Ndio maana nahoji kama kweli aliwashirikisha wabunge wenzie katika kudraft mapendekezo. Ni lazima tukiri kuwa alifanya utafiti mzuri sana lakini tujue kuwa pale wapo katika mchezo wa siasa na sisi wote tupo katika mchezo wa siasa ndio maana tunajadili haya. kwa kuwa hoja hizi huwasilishwa mapema walikwishaikalia hoja ya Mhe Zitto na kumundalia mb unge atakayetumia Kanuni kuipiga knock technical out hoja yake.
kwa ufahamu wangu mambo yote aliyopendekeza Mhe Zitto ni ndoto za mchana kwa watendaji wa serikali ya CCM ambao hukaa kuvizia posho wakati wote.

Sababu ingine iliyofanya haja hiyo kutupwa ni kashafa zilizoko katika ubinafsishaji wa mashamba ya mkonge mojawapo likiwa shamba alilochukua CHAVDA aliyesababisha Mhe Lyatonga Mrema kuondolea katika baraza la mawaziri. Ndio maana Hoja hii ilitakiwa kukaliwa kweli kweli na kuandaliwa makakati wa pamoja kama chama.

Kwa kuwa CCM ni chama kikongwe na ina machinery ya serikali nyuma yake ilitumia 2011 kuusoma uwezo wa wabunge wa CDM mmoja mmoja na inabuni mikakati ya kuwamaliza pole pole. Mfano halisi ni wakati wa kuhitimisha hoja ya katiba mwanasheria Mkuu wa Serikali alikuwa antumia maneno kwa uangalifu mkubwa kuonyesha kuwa Mhe Tundu Lissu sio mstaarabu na muungwana k.m "Mimi nimefunddishwa kumsikiza mtu akiongea" "Mimi sikufundishwa kumnyooshea mtu mwingine mkono" n.k.

Hizi ni baadhi ya strategies ambazo CDM inabidi iwe aware nazo. Na wabunge wake wanapotaka kupeleka hoja binafsi kama hizi lazima ziandaliwe mkakati maalum. Nafikiri pia timingi ya hoja binafisi ya Mhe Zitto haikuwa nzuri sana baada tu ya kuwachafua wanaopaswa kumuunga mkono kuhus posho n.k
Wabunge wa ccm hawashindi kwa hoja bali kwa kutumia vibaya wingi wao wakisaidiwa na kinara wao Makinda. CDM endeleeni hivyo hivyo, sisi wananchi tunawasikia na kusikia na kuona hayo yanayotokea bungeni. MSIOGOPE KUPELEKA HOJA ETI HAZITAPITA. Ni kweli hazitapita, lakini kamailvyosema Mbowe jana; hoja zenu tutazipokea huku kwenye umma.
 
Shida kubwa waliyo nayo wabunge wengi wa Chukua Chako Mapema ni UVIVU WA KUFIKIRI. Hoja hizo zitakataliwa tu kwa sababu hakuna aliyejipanga kufikiri namna ya kuzichangia huko Mjengoni.

imwan
 
siamin baba anaweza kataa neema kwa wanae ila leo baba amekataa maendeleo jimboni kwake kwa madai serikali haiko tayari ni kweli ama 'cake eaters' hawako tayari kulinda maslahi yao???

nadhani una maana mbunge aliyepinga hoja ya Zitto au? Kama una maana hiyo, ni kweli, huyu mheshimiwa hajui kabisa kucheza na siasa za zama hizi, hilo jimbo ndio asahahu kabisa 2015 kwani hata kama alikuwa na hoja, kitu ambacho mimi sikukiona, mpinzani wake 2015 akifanya political spinning kidogo tu, huyu mheshimiwa atakwenda na maji.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Shida kubwa waliyo nayo wabunge wengi wa Chukua Chako Mapema ni UVIVU WA KUFIKIRI. Hoja hizo zitakataliwa tu kwa sababu hakuna aliyejipanga kufikiri namna ya kuzichangia huko Mjengoni.

imwan

Hivi kweli unadhani suala hapa ni uvivu wa kufikiri kweli? Mimi sikubaliani na hilo; ni uwoga wa kupingana na serikali inayoongozwa na chama chao kwani wakicheza na hilo, majina yao kwenye kura za maoni ubunge 2015 yatakatwa; wabunge wa CCM wanakuwa na ujasiri pale tu ambapo hoja husika inakuwa imeigawanya serikali (in terms of msimamo), nusu kwa nusu huku serikali ikiwa tayari kulalia upande wowote kutegemea na upepo wa siasa, hapo ndio utabaki umeduwaa jinsi gani wabunge wa CCM wanavyokuwa mbogo mle bungeni.
 
Wabunge wa ccm hawashindi kwa hoja bali kwa kutumia vibaya wingi wao wakisaidiwa na kinara wao Makinda. CDM endeleeni hivyo hivyo, sisi wananchi tunawasikia na kusikia na kuona hayo yanayotokea bungeni. MSIOGOPE KUPELEKA HOJA ETI HAZITAPITA. Ni kweli hazitapita, lakini kamailvyosema Mbowe jana; hoja zenu tutazipokea huku kwenye umma.

Ni wananchi wangapi wanasikia haya mkuu. Ninavyosikia ni kwamba bunge halitangazwi tena kwenye redio, sijui kama ni kweli, ila kama ni kweli, wananchi wamebakiwa na TV tu, na je ni wangapi wanaotazama hizo TV? Otherwise the most watched programme on TV in Tanzania ni Ze Comedy,ikifuatiwa na taarifa ya habari ya saa mbili usiku. Tupo pamoja mpaka hapo?
 
hoja ya makamba ni contradicting, wote twajua gharama za ujenzi zilivyo juu, na watu wengi hukopa ili kujenga, leo hii utamwambia nin mtu huyu eti kodi ni ya miezi 2 tu maximum...

Nakubaliana na ww kabisa hoja ya Makamba haina mshiko na haiwezi kupita asilani, kwa nini mtu nyumba yako uweke wapangaji si bora uiweke stoo, au uweke kabisa Guest hela utaiona kuliko kupangiwa kodi ya kumtoza mpangaji na kwenda lipa TRA viwanja vinatolewa watu hawavifuatilii lawama iende serikalini, wao ndio wajenge nyumba ili ziwatosheleze wananchi wote
mfano miji ya Kigoma, Kondoa, Bagamoyo, Tanga, Korogwe, Lushoto ukijenga nyumba ww maisha yako yapo hatarini.
Kwa nini miji yote ya mijini watu wanawekeza katika majengo? (maguest, maduka mahoteli na nyumba za kupanga) na hata ukienda Mkoa wa kagera Mbeya Kilimanjaro zipo nyumba tele vijijini zinazoachwa wazi mwaka mzima baada ya mwenyeji kuja mara moja kwenye likizo kwa hiyo asipangishe ili mtu aiweke katika usafi sasa kwanini muwalazimishe kuwapangia kodi
Makamba hapo kachemsha bora Zitto
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom