Hoja 28 za Juma Duni Haji


kuna watu wanadhani mafanikio ya cuf au Cdm yalikuja miezi miwili ya mwisho , na si jitihada ya kila chama , mikutano waliofanya, na kuhamasisha watu kujiandikisha pamoja na Ccm kuchokwa hasa kwenye rushwa kila kona , serikali za mitaa mbona Cuf na Cdm walifanya vizuri tu chini ya viongozi wao wa asili
kulikuwa kuna haja gani lowasa kuletwa wakati wagombea walikuwepo wenye sifa, na je baada ya kusaini makubaliano je yaliheshimiwa hasa yale ya kuachiana majimbo je yaliheshimiwa? matatiro alikosa jimbo je mr. duni hilo halikuumizi kama kiongozi wa juu wa chama .
ni ujinga kwa mwanafunzi aliyejiandaa na mtihani kisawa sawa kwa bahati nzuri /mbaya mtihani ukavuja kapata alama 42 halafu akajisifia kuwa hayo ni mafanikio . kwangu mim naona CUF walitakiwa wafanye vizuri zaidi ya hapo kwa kuwa ccm ilikuwa taabani na wanapaswa wajilaum wenyewe kwa hilo
 
Aiseee sikuwahi kufikiri kama huyu mheshimiwa Babu Duni Hajji ana akili kubwa namna hii!
Baada ya Hashim Rungwe,Babu Duni anaingia ktk list ya wanasiasa walionifurahisha zaidi mwaka huu.
Ni makala ndefu lakini nimeisoma hatua kwa hatua,nukta kwa nukta.
Huyu Mzee alifaa kabisa kuwa makamu wetu wa Rais endapo haki ingetendeka.
Mungu akupe uhai Mzee wetu,2020 sio mbali.
 
Hapa ndio tofauti ya wazanzibar Na watanganyika inapoenekana. Wanzibar nje ya Zanziba wanakuwa pamoja.

Hoja za Duni zinawakuna waliojua Siasa baada ya Lowasa Na gia za angani. Babu Kama hajui Leo mchango wa Lipumba Na Slaa basi pasi nashaka Siasa Ni uongo Na ulaghai.
Babu duni akumbuke kauli zake mwenyewe Na serikali Yao ya kitaifa Na namna wananchi walivyochoka CCM kabla ya uchaguzi.
Lipumba wanamtumia Kama kafala Yao lakini Duni ndiye aliyevunja serikali ya kitaifa Zanzibar kwa kuwa kigeugeu Na haki ya mungu Kama Lipumba anatumika basi Na Babu duni anatumika the same way.
Babu duni alikimbilia Chadema kukidhi uroho wake wa kushika madaraka Na lazima wakubari watanzania giliba wameziona Na kukataa.
Waendelee kunyukana lakini wenyewe kwa hiyari zao wameamua kujipiga dole Na sasa wanataka kutushirikisha kujua linanukiaje.
 
Babu kashusha nondo. Na leo nimefahamu hazina ya wazee iliyopo upinzani. M
zee anajenga hoja huku akiongozwa na takwimu. Prof avuliwa nguo na kuinamishwa
Hana cha nondo wala nini! Tatizo ni ndumakuwili huyo Mzee. Sasa sijui yupo CUF au CDM?? Achana Kabisa na Profesa Lipumba!! CUF is finished under Seif Sharif Hamad. MTU gani wa kushindwa Urais Mara 5 !! Kila siku yeye tu hakuna wengine na safari hii alipoona hali mbaya akaamua kutunga matokeo na kujitangaza! Shame!!
 
Namba 22. "Akili za Watanganyika zimefinyangwa kwa miaka 50 kama unga wa chapati" hapa nakubaliana nae.
Kabisa

Nimesoma nikajisikia uchungu sana lakini haikunifanya nipingane na alichokisema.
Wazanzibar wametuzidi sana katika kujielewa.
Wana msimamo na umoja tofauti na sisi unafiki na uroho vimetuzidi.
 
Kama huelewi jambo ni bora kunyamaza na kujifunza. Duni hajaenda Chadema kwa uroho bali ni makubaliano ya vyama kukidhi matakwa ya sheria mbovu ya uchaguzi. Huyo Lipumba hata siwezi kumsema maana hata watoto wadogo wameshamuona ni babu jinga tuu. Ni mtu wa aina gani huyu ambaye anachafua CV yake ya kisiasa aliyoijenga miaka mingi kwa kukubali kutumika?
 
Lipumba ana lipi la kusea niachane nae kabisa? yeye kashindwa urais mara ngapi? Hoja ipi ya Juma Duni unaikataa? Tumia akili ktk kujadili hoja
 

Kwa tume ipi ya UCHAGUZI!? Ilichukua wiki na zaidi kuyatangaza Matokeo ya mshindi wa ubunge kinondoni huku watu wakiwa taabani kwa virungu na mabomu ya machozi ya Polisi.

Jee umeyasahau ya mbagala na kwa kingwendu!!???

CUF na upinzani watafanya vizuri zaidi siku Tanzania itakapopata tume huru ya UCHAGUZI na katiba mpya.
 
Siku hizi sipendi kusikia wala kusoma habari ya Prof. Mapumba, maana amekuwa kielelezo cha UJINGA.
Asante Mzee Duni kwa hoja zako makini, iko siku ccm itakuja kufa tu! Innalilaah Maaswabirina!
 
be the first to replay..yani niko baa na pombe yote imekata kwa hizi nondo 28 takatifu kutoka kwa babu duni
Msiwe mnataja taja bar hapa.Ona sasa umenipa mzuka wa kupiga masanga.Ngoja niende zangu junction pale nikapige zangu mbili tatu..Dhambi hii ya kunywa pombe itakuwa juu yako
 
Mpaka Leo hatuna mshauri Wa uchumi anayewasaidia watu mbalimbali nchini,Lipumba angejenga consultancy kubwa ya kiuchumi ambayo ningekuwa inashauri Governmental na non Governmental na non Governmental organi za nje na ndani na nje ya nchi,achilia mbali watu binafsi,angekuwa anafanya seminar mbali mbali ndani na nje ya nchi,angekuwa pia anaandika vitabu na kuviuza kwa watu mbalimbalj,Lipumba angekuwa millionaire na angekuwa na repute kubwa,nadhani angekuwa kama Kiyosaki kwa bongo hii,siasa imepoteza hadhi na heshima ya Lipumba,Leo hii teja ana heshimika kuliko Lipumba amepoteza followers wengi Sana aliokuwa anawashawishi kwa elimu aliyonayo
 
Maneno meeengi mpaka cjamaliza kusoma ila ww utakua ndio waleee
 
Siku hizi sipendi kusikia wala kusoma habari ya Prof. Mapumba, maana amekuwa kielelezo cha UJINGA.
Asante Mzee Duni kwa hoja zako makini, iko siku ccm itakuja kufa tu! Innalilaah Maaswabirina!
Hayo utajua mwenyewe kwanza lipumba hajui kama kuna mtu anaitwa Mapuma miyoga
 
Anayemshabikia Lowasa akapimwe akili ------Msigwa


Ni heshima kwa Mungu kumzomea fisadi Lowasa -------Lema


Kwa nini vibaka wanafungwa na kumuacha fisadi Lowasa akikamua mtaani?? --------Mbowe


Kama Lipumba ni pandikizi, basi lema, msigwa na Mbowe ni mababu wa mapandikizi duniani.

Babu duni anza na hao jamaa kwanza kuwanywesha kikombe cha loliondo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…