Hofu ya Dk. Slaa

Hofu ya Dk. Slaa

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713


Slaa-31July2015.jpg

Katibu Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dr Wilbrod Slaa

Hofu imetanda ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na wananchi kwa ujumla kutokana na kutoonekana kwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Willibrod Slaa, katika matukio mawili makubwa ya kisiasa yanayohusu mustakabali wa chama hicho.

Dk. Slaa hakuonekana siku ya kihistoria Jumanne wiki hii, iliyokuwa maalum kwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, kutangaza kujivua uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga Chadema.

Kadhalika, Dk. Slaa hakuonekana jana makao makuu ya chama wakati Lowassa alipofika kuchukua fomu ya kuwania urais kupitia chama hicho akitarajiwa kuwakilisha Umoja wa Kutetea Katiba ya Wananchi (Ukawa), katika hafla iliyotikisa jiji la Dar es Salaam na kuhudhuriwa na viongozi wa juu wa Chadema.

Hata hivyo, Dk. Slaa alihudhuria kikao cha dharura cha kamati kuu ya Chadema Jumapili iliyopita ambacho kiliendelea hadi usiku wa manene na hoja kuu ikiwa ni kujadiliana na Lowassa na kumpokea katika chama hicho.

Dk. Slaa alionekana katika baadhi ya picha zilizovuja kutoka katika kikao hicho akiwa na viongozi waandamizi wa Chadema huku akijadili jambo na Lowassa, ambaye katika siku za hivi karibuni ambekuwa gumzo kubwa baada ya kubadili upepo wa siasa za Tanzania.

Tangu juzi kumekuwa na mijadala mirefu ndani ya mitandao ya kijamii, juu ya aliko Dk. Slaa, wengine wakibashiri kuwa ameamua kuacha siasa.

Hata hivyo, Dk. Slaa mwenyewe hajawa radhi ama kupokea simu yake au kujitokeza hadharani kujibu maswali ya umma juu ya kinachomsibu.

Mbali na kutokuonekana Chadema, Dk. Slaa pia hakuonekana kwenye mkutano wa Ukawa, uliofanyika Jumatatu wiki hii makao makuu ya Chama cha Wananchi (CUF), ambao wenyeviti wenza wa umoja huo walimkaribisha Lowassa kujiunga nao.

Wakati wa Dk. Slaa akiadimika kwenye hadhara, viongozi waandamizi wa Chadema kwa nyakati tofauti wameithibitishia NIPASHE kuwa kila kitu “kimedhibitiwa” kuhusu tetesi kwamba kiongozi huyo amesusa.

“Sikiliza brother Dokta yuko freshi. Kila kitu kinakwenda kama tulivyopanga. Hakuna ukweli wa lolote juu ya madai eti Dokta anakwenda CCM,” kilisema chanzo chetu kilichoomba kutotajwa kwa sasa.

Wakati hali ikiwa hivyo, kuna taarifa kwamba Dk. Slaa anashinikizwa sana na watu wa ndani ya familia yake ambao wanadaiwa kusumbuliwa zaidi na ubinafsi, hasa baada ya mabadiliko ya kisiasa ambayo yamekikumba chama hicho kufuatia kujiunga kwa Lowassa.

Watu hao wa ndani wa familia ya Dk. Slaa wanadaiwa kuwa walikuwa wamejiandaa kuwa sehemu ya harakati za katibu mkuu huyo kuwania tena urais mwaka huu kama ilivyokuwa mwaka 2010.

“Sisi tunawaza jinsi ya kuivunjavunja CCM, lakini wapo watu wanawaza jinsi ya kuwa sijui nini sijui nani?

Hapa tunatafuta njia ya kuing’oa CCM hata kama ni kwa kutumia nguvu ya shetani,” alisema kiongozi mmoja wa Chadema.

Lowassa aliamua kujiunga Chadema baada ya kuchoshwa na siasa zilizojaa chuki za kumzuia kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kusaka tiketi ya kuwania urais kupitia CCM.

Katika hatua nyingine, Mwanasheria wa Chadema, Tundu Lissu, aliliambia NIPASHE kwamba, Dk. Slaa alishiriki vikao vyote muhimu vilivyoafiki, Lowassa kujiunga na chama hicho.

“Jana (juzi) usiku nilikuwa naye na wiki hii alishirika kikao cha kamati kuu ambacho mliona picha kwenye mitandao,” alisema.

Alipoulizwa alipo, Dk. Slaa, Lissu hakutoa majibu ya moja kwa moja zaidi ya kusema kwamba akiwapo mwenyekiti kwenye kikao chochote inatosha na siyo lazima, viongozi wote wa kitaifa wawepo.

Kuhusu Naibu Katibu wa Chadema, Tanzania Bara, John Mnyika na yeye kutoonekana katika mikutano hiyo, alijibu kwa kifupi kwamba anaumwa.

Licha ya kutafutwa mara kadhaa kupitia simu yake ya mkononi juzi na jana, Dk. Slaa hakupatikana badala yake mtu mmoja mwanamke alipokea na kusema mpigaji amekosea namba.

Alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno ili aeleze kilichomsibu kushindwa kuhudhuria matukio muhimu ya kumkaribisha Lowassa pia hakujibu.

CHANZO: NIPASHE
 
Hofu gani nyie kwan yeye ndio wakwanza kuondoka ,zzk , mwigamba , shibuda , arfi ,sio watu hao
 
​Makene huu ni wakati wa kuweka mambo sawa na kutuambia kuwa Dr.Slaa yupo au katoka!!!!!!!!?????????
 
akiondoka si ajabu akaitwa naye ni msaliti... hofu yangu hiyo
 
Kwa Makamanda wote nchini...

Taarifa za kusema Dr.Slaa na John Mnyika wanataka kuhama chama ni propaganda zinazotengenezwa na CCM ili kuwachanganya wanachama wa CHADEMA.

Siyo taarifa za kweli hata kidogo, ondoeni hofu, jipangeni vizuri na uchaguzi wa madiwani. Kuweni Imara na Imani kwa viongozi wenu wa juu.

Hawa watu wawili wako bize sana na kazi ngumu ya kuandaa mkutano wa Kamati Kuu, Baraza kuu na kisha Mkutano mkuu.

Huu ni mwaka wetu wa ushindi kwa ngazi zote 3. Miruzi ya CCM isituondoe kwenye marengo yetu mwanana. Wamechanganyikiwa, wanaweweseka mchana wa jua kali.

Tuma kwa Kamanda mwingine
 
Kurugenzi ya Habari Chadema mko wapi hamjibu aliko katibu mkuu na makamu wake kwanini mnawapa jakamoyo Watanzani?
 
Kwa Makamanda wote nchini...

Taarifa za kusema Dr.Slaa na John Mnyika wanataka kuhama chama ni propaganda zinazotengenezwa na CCM ili kuwachanganya wanachama wa CHADEMA.

Siyo taarifa za kweli hata kidogo, ondoeni hofu, jipangeni vizuri na uchaguzi wa madiwani. Kuweni Imara na Imani kwa viongozi wenu wa juu.

Hawa watu wawili wako bize sana na kazi ngumu ya kuandaa mkutano wa Kamati Kuu, Baraza kuu na kisha Mkutano mkuu.

Huu ni mwaka wetu wa ushindi kwa ngazi zote 3. Miruzi ya CCM isituondoe kwenye marengo yetu mwanana. Wamechanganyikiwa, wanaweweseka mchana wa jua kali.

Tuma kwa Kamanda mwingine

Asante kwa taarifa ila huyu tumaini makene naona siku hizi kawa shida makene.
 
Kwa Makamanda wote nchini...

Taarifa za kusema Dr.Slaa na John Mnyika wanataka kuhama chama ni propaganda zinazotengenezwa na CCM ili kuwachanganya wanachama wa CHADEMA.

Siyo taarifa za kweli hata kidogo, ondoeni hofu, jipangeni vizuri na uchaguzi wa madiwani. Kuweni Imara na Imani kwa viongozi wenu wa juu.

Hawa watu wawili wako bize sana na kazi ngumu ya kuandaa mkutano wa Kamati Kuu, Baraza kuu na kisha Mkutano mkuu.

Huu ni mwaka wetu wa ushindi kwa ngazi zote 3. Miruzi ya CCM isituondoe kwenye marengo yetu mwanana. Wamechanganyikiwa, wanaweweseka mchana wa jua kali.

Tuma kwa Kamanda mwingine

Wajitokeze watuondoe hofu
 
the measure of intelligence is the ability to change mm namweheshimu sana dr slaa na ame ply part kubwa sana ktk kujenga chama bt kuna msemo unasema ukimtafuta chizi mtaani kwenu usipomuona jichunguze ww mwenyewe inawezekana ww ndo ukawa chiz mtaan hapo leo sio watu wanaipenda sana chadema bt watu weng wanataka mabadiriko na wamechoswa na mfumo ccm sasa kama anatokea m2 mwenye uwezo wa ku2ondolea jinamiz hili kwa nn 2cmpe nafasi ? kwanza 2ondoe ccm then mengne yanafata leo 2likuwa 2namwona lipumba ndo tatizo kwa umoja we2 bt kumbe c kwel mzee wangu dr slaa pls back onbord au hata sema k2 watu wakuelewe kumbuka ww ni padre je lowassa angekuja kanisani kutubu ungemsusa kama unavyofanya kumbuka ktk fitna kubwa dunian ni mke na watoto leo JK mtoto wake kamtafutia maadui weng kuliko marafk sasa kama ni ndugu au mke ndo wanataka ww uwe rais bt watanzania tunataka kuutoa mfumo ccm rais hata awe mzee jangara
 
Dr yupo.......siku nilipomuona Lissu akiwa na LOWASA wakati wa kuchukua fomu nikaridhika moyoni kuwa Kamanda SLAA bado yupo ulingoni maana usiku wake najua LISSU NA SLAA walikutana mara tu baada ya LISSU kutoka jimboni kwake, nikafarijika kuwa maongezi yao yalikwenda vyema na waliafikiana kuwa LISSU ahudhirie na DR kwa makusudi maalum atulie kwanza.
CCM wasipokuwa makini watazidi kupotea maana hawajui kama huu mi mpango maalum, wanaeneza propaganda za Slaa kutoka CDM sasa sijui simu akitokea wataficha wapi sura zao.
 
Back
Top Bottom