Hofu Kuu ya Wana CCM

Sir R

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2009
Posts
2,175
Reaction score
300
Katika michango mingi ya wana CCM, asilimia kubwa ni kumshambulia Dr Slaa kuliko hata Mbowe. Nimetafakari sana ni kwanini Dr Slaa anashambuliwa sana. Haiwezekani mtu mmoja ashambuliwe kiasi hiki bila sababu.

Naamini CCM wamegundua Dr Slaa ana nguvu ya kuiangusha CCM kama atagombea katika uchaguzi ujao. Njia walioona ni sahihi kumdhoofisha ni kumtukana na kumchafua kwa namna yoyote ile. Tunakumbuka vizuri walianza kupambana Dr Slaa wakati wa uchaguzi wa 2010 lakini hawakufanikiwa kama walivyotarajia.

Hofu kuu ya CCM ni uchaguzi unaokuja. Wanatamani Dr afe kabla ya uchaguzi. Wanamwombea kila aina ya balaa. Wanachoshindwa kuelewa ni kuwa Dr ni mtu mmoja ndani chama kikubwa.

Tufuatilie michango ya wana CCM hapa JF, kila post linamtaja Dr Slaa kwa kejeli. Nafikiri wamemkoza Dr Slaa kwa matukano yao kuliko kumdhoofisha.

Nawasilisha.
 
CCM wanahangaika sana na Dr Slaa.Inaonekana uwezo wao wa kujenga hoja ni mdogo,mfano Mwigulu anayetema mate ndani ya ukumbi wa kisasa wa bunge.Shame on you,utaambukiza wenzako magonjwa. Wamebaki kutukana tu.Watanzania hatuhitaji matusi,jibuni hoja zinazoibuliwa na Dr Slaa kwenye mikutano yake,tatueni kero za maisha yetu.
 
Mtu yeyote atemae mate sehemu kama bungeni ana hulka ya kichawi.wanaoujua utabia wa uchawi wanayajua haya.
 
weka picha tuone vinginevyo ni uongo mkubwa sana.
 
Ngoja lukosi na mageti6 waje tuthibitishe hilo
 
weka picha tuone vinginevyo ni uongo mkubwa sana.

Tatizo ccm wengi mnatumia vichwa vya samaki kama alivyosema kiongozi wenu,"CHADEMA CHAMA KUBWA NA CHAMA MAKINI LAZIMA KIWASHIKE PABAYA KWANI KINATWANGA HUKU NA HUKU".'mtataga'.
 
Wengi wameiba na kufisadi na anayewalinda ni CCM. Kwa Slaa wanaona atahamasisha ushindi kwa CDM, CDM ambao wamedhamilia kurudisha kwa umma mali za umma zilizoko mikononi mwa wanachama wa CCM mfn nyumba za serikali, au mali zilizo hodhiwa na CCM yenyewe kama viwanja, majengo, nk
 
Jamani kama Wenye ccm wenyewe wamekili chama kuanguka thats y ad leo wanakwambia wanajenga chama. Yaani kifupi CCM iliyokua nyumba ya zege leo imekua kichuguu cha mchwa kilicho jengwa katikat ya bahari baada ya bahari kupwa. Haya sasa Maji ndo ayo yanakuja 2015.(CHADEMA Vunjaaaaaaaaaaaaaa Mchwa dhaifu hao)
 
Vijana wa CCM humu ndani ni matusi tu, tujiulize katika post za wana CCM ni mara ngapi wana taja CCM na mara ngapi wanataja CDM;
 
Najivunia kuwa Mtanzania

Mtu mmoja alifariki na kwenda kuzimu. Akiwa huko aligundua kwamba kuna kuzimu tofauti kwa nchi tofauti na akaamua kuchagua mojawapo yenye maumivu kidogo kwa ajili kufaidi ufalme wa kuzimu. Akaenda kuzimu ya Ujerumani na kuuliza “hapa wanafanya je?”

Akajibiwa "kwanza unakalishwa kwenye kiti cha umeme kwa muda wa saa moja.Halafu unalazwa kwenye kitanda chenye misumali kwa muda saa moja nyingine.Halafu anakuja shetani wa Kijerumani na kukucharaza bakora kutwa nzima”.Hakukubaliana na hali hiyo akaondoka.

Akaenda kuzimu ya Marekani,Urusi na nyingine nyingi.Akagundua kwamba zote zinafanana na kuzimu ya Ujerumani. Baada ya hapo akaenda kuzimu ya Tanzania, huko alikuta kuna misururu mirefu ya watu wanaosubiri kuingia ndani,akashangaa,akauliza wanafanya nini humo?.

Akajibiwa, "kwanza unakalishwa kwenye kiti cha umeme kwa muda wa saa moja.Halafu unalazwa kwenye kitanda chenye misumali kwa muda saa moja nyingine.Halafu anakuja shetani wa Kitanzania na kukucharaza bakora kutwa nzima. " Akauliza,Lakini hii inafanana kweli na kuzimu za nchi nyingine mbona kuna misururu mirefu ya watu namna hii?

"Akajibiwa ,kwa sababu hakuna umeme hivyo kiti cha umeme hakifanyi kazi na misumali iliyonunuliwa haijaletwa, kwa hiyo kitanda ni kizuri kulalia.Na shetani wa kitanzania ni mtumishi wa umma,ambaye anakuja asubuhi,anasaini kwenye kitabu na kurudi nyumbani kuendelea na shughuli zake binafsi.

Wanajamii naomba tutafakari na kujadili ili tuone kama haya yanayoendelea leo nchini kuhusiana na sakata la mawaziri kama kufukuza na kujiuzulu kwa baadhi yao itakuwa suluhisho la matatizo ya Watanzania kwa sasa.

Epiphan C.P.Kasililwa
0759 440 802,0784 754 963
epiphankasililwa@gmail.com
 

Tanzania ni vituko, shetani wa Tz ni mzigo.
 
CDM ipo ndani ya mioyo ya watz.kuna mjomba wangu mstaafu yupo bunda mtaa wa nyasura ambapo febr kutafanyika uchaguzi mdogo wa diwani kanishangaza sana kusema kuwa KWA BUNDA KUJITAMBULISHA KUWA WEWE NI M-CCM NI AIBU KUBWA NA KUJITAFUTIA MABALAA.Hongereni sana WanaBunda kwa kujitambua.
 
Wanadhani Dr.SLAA ndio CDM,ndo maana kutwa kucha wanamshambulia kwa matusi!
 
ccm ni wagonjwa hivyo wanamuogopa Dr. Slaa asiwachomeme sindano
 
Njua hapa pichahaitakosekana, tuwekeeni tumuone mjinga huyo

 
ccm ni wagonjwa hivyo wanamuogopa Dr. Slaa asiwachomeme sindano

Huu ni ukweli, haiwezekani watu watu wazima wamepewa nchi kuiongoza lakini usiku na mchana ni Dr Slaa na CDM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…