Hodi jamii forums

Joined
Dec 30, 2012
Posts
5
Reaction score
4
Nafurahi kuwa sehemu ya jukwaa hili kama mwanachama rasmi sasa. Hapo nyuma nilikuwa mtu wa kuangalia yanayojiri hapa pasi kuwa na uwezo wa kuchangia chochote. Kwa sasa naamini ni fursa kujadili na kutoa fikra na misimamo binafsi na ile ya itikadi ambayo ninaiamini na kuipigania pale inapobidi.

Nina amini nitapata ushirikiano constructive kwa wanjamvi wote.

Asnateni sana.

Deogratias Munishi.
 
[Asnateni sana]

................. karibu sana, kwani itikadi yako ni ipi na unadhani inagombana na itikadi ipi humu!
 
karibu kijana swali je bavicha mnawachukulia hatua gani vijana wanakesha kwenye mitandao kupaka chama matope

je una mikakati gani mwakani chama kianze mpango wa kuandaa vijana watakao simamamia uchaguzi 2014-2015

je malengo ya m4c wamefikia wapi kwa mwaka huu

tupe malengo na mikakati ya vijana wa chadema mavyuoni
je kama vijana hamuoni ni wakati muafaka wa bavicha kuanzisha miradi ya maendeleo ya chama
 

Nashukuru kwa ukaribisho wako Majanikv.

Ninaomba nisijibu maswali yako ambayo kimsingi ni ya kutaka kujua mikakati ambayo haiwezi kuwekwa hapa ambako natambua kuna wanachama wa BAVICHA na kwa maana hiyo pia CHADEMA na wasio wanaCHADEMA kwa maana ya vyama vingine. Kuifahamu mikakati hiyo ni kuwa makini kuobserve utekelezaji wake.

Kama wewe ni mwanachma, natambua una haki ya kupata taarifa na kuna njia za kupata taarifa muhimu za chama hasa zile za ndani na za kimkakati zaidi.

Tofauti na maswali mengine, kwa swali la mwisho jibu liko wazi ambalo kimsingi kuwa na miradi ya maendeleo ni jambo muhimu kwa taasisi
 
Karibu sana kijana ila mbona hujatutambulisha kwenye itikadi yako?
 
Karibu sana kijana ila mbona hujatutambulisha kwenye itikadi yako?

Kama wewe ni mwanachama wa CDM, na pia kama wewe ni kijana basi huyu ndie katibu Mkuu wa BAVICHA. Itikadi yake nadhani utakuwa umeshaipata. Kamanda Munishi karibu Jamvini na tunafarijika kukuona hapa.
 
Kama wewe ni mwanachama wa CDM, na pia kama wewe ni kijana basi huyu ndie katibu Mkuu wa BAVICHA. Itikadi yake nadhani utakuwa umeshaipata. Kamanda Munishi karibu Jamvini na tunafarijika kukuona hapa.


Ningefurahi kama angenipa majibu japo nakushukuru sana kwa kunipa haya maelezo! Kumbe ndo huyu! Karibu sana kijana Munisi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…