Karibu sana na akhsante kwa kubisha' mie na wenzangu tunawakilisha' mie nami nalifika kamba taratiibu yanikatika na wiki sasa nakamilisha' bado sijatoswa wala kupandwa presha zaidi ni kila siku nakoshwa' njoo ndugu ukihisi umefikia baridi nenda ile kona pamepashwa' nina hakika huwezi jutia na wala huta nyanyaswa' jitahidi sana kushika yanofundishwa na shika pano paswa' najua nawe ni mtu hasa na katu huwezi kuwa kasha' amani kwako tayari ushanasa
Sasa Rafiki shairi hili tunaliimbaje(Misololo mingine ipo tano kwa sita hivi ni vina kwenye Msololo mmoja na mingine nne kwa tisa ) any way karibu lakini usiwe mvivu kama mimi kuchangia ndani ya hili jamvi. Naipenda sana JF lakini muda wangu ni mdogo sana.
Basi ndugu;
Karibu ukaribie, Na kiti uketie
Vizuri tusimulie, Ya nyumbani tuyajue,
Hata hobi tuambie,na silika ifichue
Tujue sisi Tujue, Tujue jua tujue.