Hodi hodi naingia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hodi hodi naingia

Discussion in 'Utambulisho (Member Intro Forum)' started by mdanganyika2009, May 1, 2009.

 1. m

  mdanganyika2009 Member

  #1
  May 1, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hodi hodi ,naingia ndani
  Jina langu, ni siri yangu
  Mdanganyika2009, ndivyo nimeitwa
  Hodi hodi naingia ndani.

  Hodi hodi, naingia ndani
  Kaka dada, baba mama
  Nawasihi mnipokee, mdanganyika2009 naingia
  Hodi hodi naingia ndani.
   
 2. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Karibu mkuu jamvini....naona umeshatinga hadi sebuleni! Tupe mamichango yako mkuu!
   
 3. Mongoiwe

  Mongoiwe JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 521
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Karibu lakini usiwe unakuja kwa kazi maalum
   
 4. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #4
  May 1, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,586
  Likes Received: 440
  Trophy Points: 180
  Karibu hadi ndani mdanganyika2009, Inaoneka hauko vibaya sana kwenye mashairi.

  Jisikie uko Nyumbani; The Home of Great Thinkers
   
 5. Swahilian

  Swahilian JF-Expert Member

  #5
  May 2, 2009
  Joined: Apr 28, 2009
  Messages: 585
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Karibu sana na akhsante kwa kubisha' mie na wenzangu tunawakilisha' mie nami nalifika kamba taratiibu yanikatika na wiki sasa nakamilisha' bado sijatoswa wala kupandwa presha zaidi ni kila siku nakoshwa' njoo ndugu ukihisi umefikia baridi nenda ile kona pamepashwa' nina hakika huwezi jutia na wala huta nyanyaswa' jitahidi sana kushika yanofundishwa na shika pano paswa' najua nawe ni mtu hasa na katu huwezi kuwa kasha' amani kwako tayari ushanasa
   
 6. K

  Kizito Member

  #6
  May 2, 2009
  Joined: Feb 23, 2008
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa Rafiki shairi hili tunaliimbaje(Misololo mingine ipo tano kwa sita hivi ni vina kwenye Msololo mmoja na mingine nne kwa tisa ) any way karibu lakini usiwe mvivu kama mimi kuchangia ndani ya hili jamvi. Naipenda sana JF lakini muda wangu ni mdogo sana.
  Basi ndugu;
  Karibu ukaribie, Na kiti uketie
  Vizuri tusimulie, Ya nyumbani tuyajue,
  Hata hobi tuambie,na silika ifichue
  Tujue sisi Tujue, Tujue jua tujue.
   
Loading...