Hmm... Wapigwe tu!

hilo tofali la huyo mjeshi likimdondokea hafiki huko wanakompeleka
 
Hapo ni AFRIKA YA KATI na usiombe kuuliza ni jeshi upande gani.
Muhimu,tuelewe kuwa amani ni kila kitu.
 
Huu ni ushenzi


mankachara;
Huo si ushenzi ni matokeo ya walala hoi wakichoka. Ni dalili za mapinduzi siku si nyingi. Unajinyima angalao ununue radio dudu proof, anakuja msela anaichukua na kwenda uza apate kishushio. Ukienda policcm wanakudai pesa za kununulia karatasi ya kuandika ripoti.
Nakwambia ukimbamba huyo msela, hilo ni dogo. Watu wamechokaaaaaa kila mtu na lwake.
 
Hiyo adhabu aliyopewa ni kubwa sana haijalishi ametenda kosa gani
 
Ant-baraka hao central africa-MIAFRICA NDIVYO TULIVYO.
 
Daah, ni kosa gani alofanya huyu binadamu kiasi cha kustahili adhabu hii?!
 
Afrika tu hiyo, we unafikiri itakuwa wapi.
Afrika kubwa nilitaka kufahamu eneo, nchi, au hata kama ni moja ya mikoa ya Tz si unajua picha kuna eneo hata kama umefika unaweza usione ndani pia, ila kuna mkuu ameshajibu hapo juu Afrika ya kati
 
mmmh!! Hilo jeshi lenye kofia nyekundu ni la waasi au! Na ni wapi hiyo?
 
Hata kama ana kosa lolote lile on earth, sio hivi. Ushenzi na ukatili uliopitiliza!

Yategemea alifanya nini. Ni kweli huu ni ukatili ulopitiliza. Ila kwa mfano, alimbaka mke wangu mbele yangu na mbele ya watoto wangu, kisha kuwateketeza nami nikiwa sijiwezi, washanipa kipigo. Sitamuonea huruma hata kidogo. Huko kwa waasi vitu kama hivi vinatokea. Hivyo yategemea na alichofanya. Mambo ya human rights yatasubiri. Sasa sijajua kwenye picha muasi ni nani. Je ni raia mwema anaonewa na waasi au anaonewa na majeshi ya kulinda amani?? Sijajua.
 
Huyo atakuwa ni Boko haramu akipata kichapo kutoka jeshi la Nigeria!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…