Jayspeed
Senior Member
- Feb 23, 2014
- 156
- 169
UBUNIFU
Tukiwa kama vijana ambao tunataka kujikomboa kutoka kwenye hali ya chini na kusogea kwenye mafanikio yetu na mafanikio yetu yadumu milele inabidi tuwe wabunifu, kuwa wabunifu inamaana kufanya jambo fulani kwa utofauti na wengine ili kuongeza thamani katika kazi, na biashara zetu....
Unapokua mbunifu ndani ya biashara yako au hata kwa bosi wako kazini ulipoajiriwa maisha yako yanakuwa ya furaha sana maana kila wakati unaonekana una thamani kuliko wengine....
sishangai kuona mtu mbunifu kazini anapandishwa cheo kazini kila baada ya mwaka na huku mwingine ambae sio mbunifu au hajataka kuwa mbunifu anashushwa kila baada ya mwaka hapo ndipo utaona faida ya kuwa mbunifu..
Kuwa mbunifu kunatofautisha kazi yako au hata bihashara yako na mtu mwingine hata kama ni za aina moja..
Hata kwenye makampuni baada ya nidhamu ya kazi kinachofata ni ubunifu wa kazi. Mtu yoyote yule mbunifu ni mchapa kazi sababu anapenda kuweka vitu tofauti ili aonekane tofauti...Akili za darasani ni za kufaulu mitihani lakini ubunifu ni akili za kufaulu mtihani wa maisha.
Swala la mafanikio halihitaji elimu ya digrii wala uzamili au hata filosofi ya udaktari yaani PhD, hata elimu ya msingi inatosha kukupa mafanikio zaidi kama ukiwa mbunifu tu...
Mtu mmoja ajulikanae kwa jina la Edward de Bono huyu ni mwanasaiokolojia alishawahi kusema kuwa "ubunifu ni kitu kinachohamasisha zaidi kwasababu hufanya watu wapende wanachokifanya zaidi, ubunifu huleta matumaini pale unapobuni kitu chenye manufaa zaidi, ubunifu unakupa uwezo wa aina tofauti za mafanikio, ubunifu hufanya kuwa ya raha na kuvutia zaidi"
Tunajifunza kwa de Bono kuwa mtu ambae anatumia ubunifu ndani ya maisha yake kila jambo analolifanya anaona mafanikio sababu anajua kubuni namna nyingi za kufanikiwa...
Fanikisha biashara yako kwa kuwa mbunifu na kama unaona giza ndani ya biashara yako tafuta mtu mwenye biashara kama yako mshirikishe mawazo yako akupe mawazo yake hii itakufanya kugundua mambo mengi na kuongeza ubunifu ndani ya biashara yako nina uhakika itafanikiwa...
By Jay Speed