Director D
Senior Member
- Feb 24, 2016
- 192
- 229
Mtandao wa kijamii wa Facebook,
ndio umetokea kuwa mtandao wa kijamii
wenye mashabiki wengi kuliko wowote
uliowahi kuanzishwa.
Wewe uliyejiunga,
katika mtandao huu utajikuta unakutana
na watu uliopotezana nao
miaka mingi iliyopita,
na wengine wapya ambao haungezani
kama utawahi kuwasiliana nao.
Kati ya watu hawa utakao kutana nao
wengine wanakuwa na tabia za ajabu
mpaka muda mwengine wanaumiza kichwa.
Hebu soma hapa uzijue hizo tabia kama
haujakumbwa na balaa hizo basi
ujipange.
1.KUWEKA UJUMBE WA AINA MOJA MARA
NYINGI KATIKA UKURASA WA MTU
Kitu chochote kinapozidi kiwango huwa
kinachefua hata kuangalia,
hata kama unamjali mtu
huwezi kuweka ujumbe mmoja
mara kibao utakuwa unamfanya apoteze
ladha ya ujumbe.
We mtu anaposti"duh!"x10 hadi
inachosha kusoma.
2.KU'LIKE' STATUS ZA HUZUNI
Yaani hata kama unashindwa kutofautisha
habari za huzuni na furaha
basi fikiria kabla huja'like'.
We mtu amepost picha ya
marehemu ndugu au mzazi
halafu wewe una'like',
ni heri uandike kitu kuliko 'like'
3.KUPOSTI KILA DAKIKA KITU UNACHOFANYA
Utakuta mtu anapoamka asubuhi anaanza
kuposti:
"Ndio naamka sasa wadau/marafiki"
baada ya muda kidogo;
"Napiga chai na chapati hapa karibuni
waungwana"
tena;
"Nasubiria basi pande hizi kwa
manyanya teja ana kelele huyo"
halafu;
"Dah! naingia ofisini hakuna hata mtu"
halafu;
"Natamani muda wa chakula ufike nina
njaa kinoma"
Nadhani watu aina hii ushakutana nao
sana tu na wanachosha kwa kweli.
4.KUWEKA VITU BINAFSI KATIKA UKURASA
WAKE
Lazima,
utambue kuwa facebook ni mtandao wa
kijamii kwa hiyo kila mtu
anayefungua ukurasa wako awe rafiki
asiwe rafiki ataona tu.
Sasa wewe,
unaweka mapicha yako ya chumbani tena
ukiwa umelala!!
jaribu kutofautisha vitu gani vya
kushirikisha kila mtu na vitu gani
unapaswa kushirikisha watu wako
wachache.
5.KUWEKA LUGHA ZA MATUSI
Lazima utambue,
kuwa si kila mtu anapendelea kukutana
na lugha za matusi juu
ya ukurasa wako.
Yawezekana unataka kufikisha hisia zako
kwa mtu fulani ni heri
utumie njia nyingine lakini si
kuweka matusi ya wazi juu.
6.KUWA'TAG' MARAFIKI PICHA CHAFU
Utakuta mtu anamtag rafiki yake,
picha chafu zisizofaa katika ukurasa
wake,
hata kama wewe
hakuna watu wa heshima wanaofungua
ukurasa wako,
jua kuna wengine wazazi wao
wanafungua kurasa zao wanapokutana
na hizo picha unafikiri
wanapata picha gani?
7.KUPOSTI KATIKA UKURASA WAKO STATUS
NDEFU KINOMA
Ni heri hata kama unaichukua mahali
hiyo status,
jua kuichuja basi kuliko unaposti
status kama insha'
unategemea nani anamuda wa kusoma
status ndefu hivyo
jali muda wa wenzako.
Ndio maana mwengine kabla haijamliza
kujua maana yake analike tu bila kujua
maana yake,
eeh!eeh! ushamchosa hivyo.
8.KUTAKA KUCHAT NA MTU KILA UNAPOMUONA
HEWANI
Si kila wakati,
mtu anaingia facebook kutaka kuchat
na watu, kuna muda,
anakuja kuchati na mtu maalumu,
lakini wewe unalazimisha kuchati
naye kila wakati,
unaandika
tu maujumbe mengi
ukiona hakujibu.
JAMANI HUU NI MTAZAMO,
TU JARIBU KUCHUJA VITU VYA KUFANYA
KATIKA UKURASA WAKO NA WA WATU
WENGINE.
ILI USIPOTEZE MARAFIKI KWANI RAHA YA
MTANDAO WA KIJAMII NI KUWASILIANA NA
WATU.
WATU WENGI TUPO KATIKA MKUMBO HUU,
TUJIREKEBISHE BASI ILI MAISHA YA
FACEBOOK YAWE MAZURI KWA KILA MMOJA
WETU. NAWASILISHAA.
ndio umetokea kuwa mtandao wa kijamii
wenye mashabiki wengi kuliko wowote
uliowahi kuanzishwa.
Wewe uliyejiunga,
katika mtandao huu utajikuta unakutana
na watu uliopotezana nao
miaka mingi iliyopita,
na wengine wapya ambao haungezani
kama utawahi kuwasiliana nao.
Kati ya watu hawa utakao kutana nao
wengine wanakuwa na tabia za ajabu
mpaka muda mwengine wanaumiza kichwa.
Hebu soma hapa uzijue hizo tabia kama
haujakumbwa na balaa hizo basi
ujipange.
1.KUWEKA UJUMBE WA AINA MOJA MARA
NYINGI KATIKA UKURASA WA MTU
Kitu chochote kinapozidi kiwango huwa
kinachefua hata kuangalia,
hata kama unamjali mtu
huwezi kuweka ujumbe mmoja
mara kibao utakuwa unamfanya apoteze
ladha ya ujumbe.
We mtu anaposti"duh!"x10 hadi
inachosha kusoma.
2.KU'LIKE' STATUS ZA HUZUNI
Yaani hata kama unashindwa kutofautisha
habari za huzuni na furaha
basi fikiria kabla huja'like'.
We mtu amepost picha ya
marehemu ndugu au mzazi
halafu wewe una'like',
ni heri uandike kitu kuliko 'like'
3.KUPOSTI KILA DAKIKA KITU UNACHOFANYA
Utakuta mtu anapoamka asubuhi anaanza
kuposti:
"Ndio naamka sasa wadau/marafiki"
baada ya muda kidogo;
"Napiga chai na chapati hapa karibuni
waungwana"
tena;
"Nasubiria basi pande hizi kwa
manyanya teja ana kelele huyo"
halafu;
"Dah! naingia ofisini hakuna hata mtu"
halafu;
"Natamani muda wa chakula ufike nina
njaa kinoma"
Nadhani watu aina hii ushakutana nao
sana tu na wanachosha kwa kweli.
4.KUWEKA VITU BINAFSI KATIKA UKURASA
WAKE
Lazima,
utambue kuwa facebook ni mtandao wa
kijamii kwa hiyo kila mtu
anayefungua ukurasa wako awe rafiki
asiwe rafiki ataona tu.
Sasa wewe,
unaweka mapicha yako ya chumbani tena
ukiwa umelala!!
jaribu kutofautisha vitu gani vya
kushirikisha kila mtu na vitu gani
unapaswa kushirikisha watu wako
wachache.
5.KUWEKA LUGHA ZA MATUSI
Lazima utambue,
kuwa si kila mtu anapendelea kukutana
na lugha za matusi juu
ya ukurasa wako.
Yawezekana unataka kufikisha hisia zako
kwa mtu fulani ni heri
utumie njia nyingine lakini si
kuweka matusi ya wazi juu.
6.KUWA'TAG' MARAFIKI PICHA CHAFU
Utakuta mtu anamtag rafiki yake,
picha chafu zisizofaa katika ukurasa
wake,
hata kama wewe
hakuna watu wa heshima wanaofungua
ukurasa wako,
jua kuna wengine wazazi wao
wanafungua kurasa zao wanapokutana
na hizo picha unafikiri
wanapata picha gani?
7.KUPOSTI KATIKA UKURASA WAKO STATUS
NDEFU KINOMA
Ni heri hata kama unaichukua mahali
hiyo status,
jua kuichuja basi kuliko unaposti
status kama insha'
unategemea nani anamuda wa kusoma
status ndefu hivyo
jali muda wa wenzako.
Ndio maana mwengine kabla haijamliza
kujua maana yake analike tu bila kujua
maana yake,
eeh!eeh! ushamchosa hivyo.
8.KUTAKA KUCHAT NA MTU KILA UNAPOMUONA
HEWANI
Si kila wakati,
mtu anaingia facebook kutaka kuchat
na watu, kuna muda,
anakuja kuchati na mtu maalumu,
lakini wewe unalazimisha kuchati
naye kila wakati,
unaandika
tu maujumbe mengi
ukiona hakujibu.
JAMANI HUU NI MTAZAMO,
TU JARIBU KUCHUJA VITU VYA KUFANYA
KATIKA UKURASA WAKO NA WA WATU
WENGINE.
ILI USIPOTEZE MARAFIKI KWANI RAHA YA
MTANDAO WA KIJAMII NI KUWASILIANA NA
WATU.
WATU WENGI TUPO KATIKA MKUMBO HUU,
TUJIREKEBISHE BASI ILI MAISHA YA
FACEBOOK YAWE MAZURI KWA KILA MMOJA
WETU. NAWASILISHAA.