Hizi sarakasi mnazofanya zitaisha lini?

Papushikashi

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
10,748
12,859
Salaam wana jf
Nimekuwa nikitafakari hii series ya serikali kuzuia mikutano ya kisiasa, nakumbuka mwanzoni Mh Pm alitoa tamko la kuzuia mikutano pale Edward lowasa alipotangaza kuzunguka nchi nzima kuwashukuru wananchi kwa kura walizompa.... Lakini hii ilikuwa kama trailer
Sasa tukija kwenye tamko la Mh Mkulu aliposema hakuna kufanya siasa mpaka 2020. Sasa kumbuka kipindi hicho mbeleni walikuwa na mkutano wa kumchagua mwenyekiti wao wa Chama, Bavicha wakaja na tamko la kwenda Dodoma kusaidia Police kuzuia mkutano huo sababu mikutano ya kisiasa ilikuwa imepigwa marufuku...,
Ghafla Serikali ikabadilisha maneno na kusema Mikutano ya ndani Inaruhusiwa na kumbuka wiki chache nyuma kuna mikutano ya ndani ya chadema ikiwemo graduation ya chaso Dodoma..
Baada ya kumchagua mwenyekiti walienda kumtambulisha kwenye mkutano wa hadhara na hapo wanabadirisha maneno na kusema Unatakiwa kufanya mkutano eneo ambalo umeshinda, na bwana mkulu akijitamba kuwa yeye ni kiongozi wa nchi nzima kwahiyo anaweza kufanya mkutano sehemu yoyote, wakati huo kwenye mikutano yake anawasimamisha viongozi wa kisiasa ambao sio wa eneo hilo.
Juzi tumetoka kumuoa Ole sendeka akifanya mkutano na wakati hajashinda eneo lolote na hakuna kiongozi wa serikali wala polisi waliotoa tamko kuhusu kitendo hicho.
Sasa huu uonevu wa wazi kwa wapinzani na sarakasi mnazofanya zitaisha lini?
 
Asante umeandika vizuri hizi ndio siasa za Afrika ni fitina kila siku.
 
Back
Top Bottom