Hizi Sapraiz hizi...

Siku hizi kumekuwa na Tabia ya watu kukuahidi kabisa kwamba atakuletea Sapraiz,
Sasa najiuliza hivi nikiahidiwa kuwa nitaletewa sapraiz, bado ina uhalali wa kuitwa spraiz tena?
Sasa TANMO nimeahidiwa kuletewa Sapraiz na nimeshaisubiri vya kutosha, na inakaribia kuja. Nimeshaimajini (imagine) mpaka Gari hapa nilipo,, sasa nina wasiwasi hiyo Sapraiz ikiwa kitu ambacho kiko viwango vya chini ya matarajio yangu si huyu mleta Sapraiz ndiye atakuwa Surprised na reaction yangu Wajameni?

Ile habari ya Oooh My Goood,, au Waaaaoh,, au This is soooo swiiiti,, nikishindwa kuzitoa si nitamdisapoint mtu Jamani?
huu ushamba huu..

BTW: Umeshawahi ona Mmasai Sharobaro? Kwa kifupi ana swaga zote za kisharobaro mpaka mavazi. Wakati huo huo ametoga sikio, ameng'oa jino, anakula ugoro wake huku yupo kijiweni kwa Wamasai wenzake wanapiga stori..?

Mapendo,
TANMO

some one is inlove
 
Back
Top Bottom