Hizi ni dalili za HIV?

Ryzen

JF-Expert Member
Dec 6, 2012
7,301
8,693
eti wanajamii vipi dalili za HIV zinaweza kuwa kutokwa na vipele vinavyowashaa saana miguuni na mikononi au vipi yaani zile dalili za mwanzo (ARS)
 
Kapime tu ndio njia sahihi yakujua kama wewe ni ferouzi au prof jay
 
Daaah Mkuu Pole sana!Kula Vizuri,Fanya Mazoezi,Pumzisha Mwili utaishi kwa Matumaini,by the way Mkumbuke Mola wako tu
 
eti wanajamii vipi dalili za HIV zinaweza kuwa kutokwa na vipele vinavyowashaa saana miguuni na mikononi au vipi yaani zile dalili za mwanzo (ARS)
Swali lako haliko sawa kidogo.

Kuna dalili Mara baada ya MTU kuambukizwa HIV siku chache zilizopita

Na,kuna dalili za MTU kuanza kuumwa ugonjwa wa Ukimwi kutoka na HIV baada ya miaka kadhaa ya maambikizi

Sasa ulitaka kulitaka kujua lipo hapo
 
Nenda kapime Mkuu wacha kuishi na hofu kila siku iendayo kwa Mungu. Inawezekana kabisa hivyo vipele havina uhusiano wowote na HIV.

eti wanajamii vipi dalili za HIV zinaweza kuwa kutokwa na vipele vinavyowashaa saana miguuni na mikononi au vipi yaani zile dalili za mwanzo (ARS)
 
Pole Mkuu,chukua hatua ya kwenda hospitali kupima ili usiwe na hofu omba ufanye vipimo vyote muhimu ongea na daktari wako wazi kabisa kuhusu unavyojisikia,unachoona kwa macho kama hivyo vipele na kujikuna na hata uchovu usioisha,madaktari wana uzoefu mkubwa na ushauri mzuri sana,hutajuta,endelea kumuomba Mungu sana ukifanya toba na kuomba amani ili upokee kila kilicho mbele yako kwa uvumilivu,Mungu wetu anatupenda Sana na hakika utapokea majibu yako kwa amani yawe positive au negative maana maisha ni lazima yaendelee,Mungu akusaidie sana na akupe amani,utakuwa sawa tu ,ubarikiwe.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom