Hizi ndizo CHANGAMOTO ZA CHADEMA TANZANIA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hizi ndizo CHANGAMOTO ZA CHADEMA TANZANIA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MPAMBANAJI.COM, Apr 21, 2012.

 1. MPAMBANAJI.COM

  MPAMBANAJI.COM JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2012
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  HATMA YA CHADEMA TANZANIA

  Chadema- ni chama makini na chenye mrengo unaokidhi hisia za wengi kwa sasa ndani ya Taifa hili kubwa hapa hapa Afrika Mashariki lenye rasilimali nyingi sana ila kichekesho kwa kuwa miongoni mwa Nchi maskini sana hapa Duniani.

  Lazima tuuchambue ukweli juu ya mustakabadhi na uendelevu wa Chama hiki katika kipindi cha miaka 20 hadi 50 ijayo hapa Tanzania. Nimekua nikifuatilia na kuchambua mwenendo wa CHADEMA na kugundua kweli bado wanamapungufu kadha ya kimkakati.Kama kada wake wakawaida naomba Wadau wote wa CHADEMA tukihakiki chama hiki kwa Nyanja hizi rahisi kwanza ambazo zinahusu umma wa Watanzania na kioo cha CHAMA ndani na nje ya Tanzania.

  Tuanze na haya kwanza,mengine baadae.Uendelevu wa chama hiki utakua imara kama wakizingatia:· demokrasia pevu ndani ya chama hususani wakati wa uchaguzi wa ndani kwa mujibu wa katiba.Shaka yangu hapa kuna wachache ambao wanaamini hao tu ndio wanaweza na bila ya wao chama hakitaendelea.

  Swali la muhimu hapa ni kweli kwa mf.Mh. Mbowe atakubali kuachia nafasi ya Uenyekiti wa Chama pindi kipindi chake kwa ukomo kikatiba kitakapotimia? Na jee Dr. Slaa na viongozi wengine watakua tayari kukijenga chama na kutoa usimamizi wa kiushauri kupitia uongozi mpya au watakaa pembeni na kuangalia wengine?Wameandaaje Vijana kuelewa haya?

  Katiba inauwazi wakutosha?· Mapokezi ya kila anayetoka CCM au vyama vingine vya Upinzani: Hapa lazima CHADEMA wakubali ya kuwa wamekua ni mwiba kwa kusema ukweli na kuielimisha jamii ya kitanzania juu ya haki za kisiasa na Uraia katika kuihoji na kuwajibisha Serikali tata ya CCM.

  Hii inapelekea wengi kuvutiwa na chama hiki.Shauku hapa ni pale wanapowakumbatia watu hawa na kuwapa vyeo huku wakiwaacha wale makada misingi bila wajibu wowote.Baadaye hii itapelekea misigano katika ulafi wa kutaka uongozi na hivyo kujenga makundi ya kiuhasama na chuki..

  Kama CHADEMA hawatakubali kuchukua hatua madhubuti za kuwakaribisha watu hawa kwa umakini basi bila shaka mtayaona haya yanatimia miaka miwili ijayo.· Nguvu kazi za Uenezi Kikanda: Hatuna sababu ya kutumia watu walewale katika kukijenga chama kitaifa.ni vyema wakateuliwa wanachama maarufu na waliojengewa uwezo katika chama ambao watasimama kama Kikosi kaz.

  Kwa mfano JOHN CHIBUDA angeliweza kuwa nguzo muhimu ya chadema kanda ya Ziwa iwapo angetumika kama afisa mwenezi wa Kanda kulikoni alivyowekwa pembeni.La muhimu hata kama mashaka yapo dhidi yake lazima tuone utendaji wake na hii itadhihirisha nguvu kazi ya CHAMA kulikoni kuona kila mara the static Team.

  Zitto Kabwe:Huyu ni kijana makini na mchapa kazi ambaye baadhi ya Viongozi wa CHADEMA hawana imani naye..ila ni mtaji mkubwa sana katika siasa za jamii ya watanzania katka kuunganisha imani na wasiwasi wa utaasisi wa kikaskazini...Zitto Kabwe anaonekana na ndoto makini sana za hata kuwa Raisi wa Taifa hili..Inasikitisha sana kwa baadhi ya makada wa CHAMA kumpinga na hata wengine kumbeza.

  Je hana sifa? Au mnataka aseme ndoto zake akishakua mzee and out of use? Zitto ni kivutio kikubwa sana kwa vijana wa Tanzania,wasomi,Wakristo,Waislamu,Wakulima,wafanyakazi na watu wa kada mbalimbali.Zitto anasifa kubwa moja ambayo hata baadhi ya viongozi wa juu wa chama hawana... na hii ni "YEYE SIO MROPOKAJI" hajaonekana katika siasa za chuki na ni mtaaluma ambaye anaonekana amesoma na hakukremu..

  Je kwanini mawazo yake ndani ya chama yaonekane ni mwiba kwa baadhi ya watu?.Kama anaonekana affiliated na CCM members(some of) je how positive are those affiliation to the Party and personal learning processes? Au je ni kweli kwamba ukiwa CDM hauhitaji hata kutaniana na MwaCCM?.Laima tuchambue mtaji Jamii ktk siasa(Socio-Political Capital Analysis) na manufaa kwa CHAMA.·

  Utekelezaji wa Elimu ya Haki:CHADEMA ni makini sana katika kipengele cha ELIMU YA chimbuko la haki za Msingi za Binadamu(First Rights Generation)Hapa linahusu haki kisiasa na kiuraia ambapo faida yake san asana ni kupata kura na kujua haki kisiasa..Chimbuko hili ni lakufikirika kwa wakati mwingine kwani linavikwazo vingi kutokana na utashi tofauti wa watu(Ila si vipengele vyote).

  CHADEMA wanaonekana kuwa butu sana katika kuelezea hisia kina sana za haki za kiuchumi,kielimu,Afya,barabara ,kazi ,usimamizi wa rasilimali za Taifa kwa tafsiri ya kitakwimu kama chimbuko la pili la haki za binadamu...

  Hii inapunguza makali endelevu kwa Chama na mashabiki hususani pale mambo yanapozungumziwa juu juu tuuu....Kwa kutokufanya hivi ni pigo kwa CHADEMA yenyewe kwani hatokama wakipata ridhaa ya kuongoza Taifa hii teule na maskini, bado mambo yatakua magumu..kwani ni?,

  Watanzania wengi watategemea kufanyiwa kazi na ugumu wa maisha kupungua kupitia mgongo wa Chadema bila ya kuangalia namna serikali ya CHADEMA itakavyorahisisha upatikanaji wa huduma hizi.· Ushiriki wa Wananchi:Haijajulikana wazi kama kweli wananchi wengi wanaishabikia CHADEMA kwa ridhaa yao wenyewe baada ya kugundua matatizo yalipo ndani ya Serikali ya CCM au ni kwa mvuto wa kupata taarifa(participation by mobilization or participation by information).

  Hii ni hatari kama si by Mobilization kwani Wengi watategema makubwa kwa kupitia Participation by Information) yaani just to be informed.· Mizizi ya chama:Imeanza kwa ulegevu tena inajengwa na makada wengi ambao walikua ni wanaCCM kamili!Shida je wakikosa walichotegema ndani ya CDM na kurudi CCM hili halitakua pigo kwa CDM?· Kuunda mfumo mpya:

  Itambulike wazi kwamba Tanzania isitegemee kupata mkate mtamu na endelevu ndani ya kipindi cha miaka 5 iwapo CHADEMA itaingia madarakani:Sababu kuu hapa ni changamoto zitakazokuwepo kupitia chama pinzani CCM kwa wakati huo.

  Kuunda mfumo mpya wa kiutawala utawachukua si chini ya miaka 4 labda tu Katiba Mpya itaje maslahi ya kitaifa ambayo mifumo Fulani kamwe haitabadilika kupitia chama chochote kitakachounda serikali ndani Tanzania.·

  Ahadi zake kwa wananchi: CHADEMA inaonekana kutoa matumaini makubwa sana kwa wananchi wa Tanzania.Lamsingi kwanza wawaandae kukubali mabadiliko na wafahamu haki na wajibu wao na sio kutafuta MASS SUPPORT without Power to support thus anticipated outcomes.

  · Uchaguzi Mkuu 2015:Kama chama hiki kitavuka vyema katika chaguzi zake za ndazi zijazo na wapinzani wake CCM wakafanya vibayabasi CHADEMA kitakua na nafasi nzuri kisiasa ndani ya Tanzania.Na hapa CHADEMA hanabudi kuungana na vyama vyema sera sawa kakika ukombozi sahihi wa Nchi hii kiuchumi,kijamii na kidemokrasia.

  Ili hatma hii itimie ni lazima kuwe na mgawanyo wa uteuzi wa wagombea kulingana na namna kinavyokubalika ktka kona mbalimbali za Nchi hii. Au kama sivyo lazima waweke mgombea anayekubalika vyema pande zote za Tanzania.

  Mgombea atakayekubalika zaidi ni yule atakayepunguza hisia za mashaka kidini,kikanda na kiutendaji. Kinyume na hapa CHADEMA wakunali kuwa wataendelea kupata wabunge na madiwani ila si nafasi ya Uraisi.

  · Wapiga kura:Mtaji mkubwa wa CHADEMA ni vijana ambao kwa bahati mbaya wengi hawana makazi ya kudumu kutokana na shughuli wafanyazo hususani masomo.

  Mambo mengine yakiwemo kutokuboresha kadi za kupigia kura na kutokua tayari kusimama kwenye misururu mirefu.Lazima CDM waweke mkakati wa ushawishi kwa Vijana na wapiga kura wengine wote.

  Kwa sasa pongezi kubwa kwa siasa za kistaarabu,ushauri kwa vijana,uvumilivu wa rafu za siasa kutoka chama kinachounda serikali.Muhimu pia ni kujitahidi kutekeleza yaliyohaidiwa kwa wananchi katika maeneo mnayoongoza na pia muwe wasafi ktka matumizi ya rasilimali mlizonazo.

  Kwa wachambuzi makini watendelea kuongeza maoni yao ili CHAMA kifahamu haya, ila kwa wale wavivu wa fikra basi watakosoa japo pia ni haki yao kutoa maoni na maoni yao kuheshimiwa.Uongozi wa CHADEMA ni vyema wakaendelea kuchambua sera za millennium Development Goals na kuwaelimisha watanzania namna fursa zilizotumika na ukweli wake halisi hapa Tanzania.

  Hili ni rahisi sana kwani mambo yote yapo mtandaoni na wengi wanaona.Aksante sana kwa kusoma makala hii ndefu na karibu sana kwenye maoni yangu kwa CHAMA wakati mwingine.Unaweza pia ukanipm.
   
 2. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Kuna ukweli katika hoja lakina 'I smell a rat'
   
 3. juma sal

  juma sal Senior Member

  #3
  Apr 21, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  sawa nimekuelewa na nitayanyia kazi mawazo yako
   
 4. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Alafu mleta thread naomba nikukosoe kitu kimoja"
  "CHADEMA HAKUNA MAKADA BALI KUNA MAKAMANDA" so kwa hilo naomba usirudie makosa siku nyingine kuwahaibisha makamanda kwa kuwaita makada.
  Solidarity forever.
   
 5. K

  Kyambuko New Member

  #5
  Apr 21, 2012
  Joined: Apr 15, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante kamanda,uchambuzi mzuri sana.Tuendelee kujipanga huku silaha zikiwamkononi
   
 6. MPAMBANAJI.COM

  MPAMBANAJI.COM JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2012
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 704
  Likes Received: 159
  Trophy Points: 60
  Aksante kwa wazo...ila KAMANDA kwa Tafsiri ya siasa ndio hiyo hiyo Kada...Mzalendo wa mapambano na ufuasi...poa
   
Loading...