Hizi ndio ofisi 23 ambazo waajiriwa hujisikia na wana nyodo sana

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,560
Wadau,

Kuna hawa jamaa wanaofanya kazi maeneo haya wanajisikia sana. Wanaona wamefika. Wana nyodo sana mtaani.

1. TISS

2. Bank

3. TRA

4. PCCB

5. Wizarani - Head Quarters

6. Uhamiaji / Boarder

7. Madini

8. TANAPA

9. Bandari

10. Airports

11. Lumumba

12. Ikulu

13. CAG

14. Bungeni

15. TANROADS

16. Traffic

17. Loan Board (HESLB)

18. Ubalozi

19. Madini

20. ' Central '

21. TFDA

22. TBS

23. NIDA

Aisee usiombe uingie 18 za hawa jamaa. Wanapenda sana kunyenyekewa. Wananyanyua mabega juu kama mbingu ni ya kwao.

Hovyo sana.
 
Kuna ka jamaa juzi kati nilienda kwenye ofisi flani hivi ya serikali nadhani yeye anaweza kuwa anaongoza kwa nyodo.

Yaani ananielewesha kitu kidogo sana lakini hizo nyodo sasa ni balaa mara sijui amechanganya vimaneno vya kiingereza hapa na pale ilimradi tu nimuone mtu wa maana kumbe boya tu
 
Mi nilifuata barua kwa balozi wa nyumba 10 kwa ajili ya utambulisho, aisee yule mzee alinisimanga, nikataka niondoke nikasema ngoja nivumilie tu

Mzee ananihoji kwanza nimehamia lini kwenye "mtaa wake"
Akadai nilitakiwa kwenda kujitambulisha kwake siku ya kwanza nilipohamia pale nimuonyeshe na mkataba wangu na mwenye nyumba
Kishq ananiambia hana muda, nikipenda nisubiri, huku anapiga story za umbea na majirani zake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom