Hizi milioni mbili taslimu

Hizi milioni mbili taslimu

Wakuu kuna mdau kanipa mil.2 taslimu nimuwekee kwa muda wa miezi mitatu,sasa kilichopo akilini mwangu imenijia idea kuwa within this time hivi hakuna mishe naweza nikaifanyia ijizungushe ili wakati wa kuja kuzichukua na mimi niwe nimebakia na masalia?

Maana kuziweka tu zivunde naona sio sawa,sababu ya kuandika hapa ni kuomba msaada wa kimawazo kwa mwenye uelewa wa nini naweza nikakifanya kuzizungusha hizi pesa zizaliane kwa kipindi tajwa?

Nitalichukua na kulifanyia kazi lolote nitakaloona litanifaa na lina uhalisia ili nisile hasara,maana mwenyewe hajui nikiwazacho hapa afu ni mbabe pia atanivuruga!
Tatu mzuka ndo mwekaji mzuri
 
Mkuu cheza tatu mzuka lazima utusue
3000000*200=600000000 Toa mil 3 zake
600000000-3000000=597000000 faida
 
Biashara ni ngumu sasa hivi return ya muda mfupi hakuna, ndo unachokiwaza wewe
 
Taaaaatu mzukaaaaa, bikooo mshiko nje nje, bet kistaarabu na mkeka bet, hizo ni tatu moja itakufaa jichagulie
 
bado naona hasara sana kuziweka tu idle,ingawa maoni ya wengi humu yamejaa visirani utadhani na mimi ni za kwangu,nipeni michongo wadau ili niizungushe hii hela,kwa wale wanaume wenzangu najua hawawezi kuanza taarabu kama baadhi ya waliotangulia...
 
USIJARIBU KUTUMIA PESA ZA WATU KWA LOLOTE ! Kwanza jiulize: Kwa nini huyo jamaa hajaziweka kwenye M-pesa au Tigo pesa n.k.? Kwa nini akuwekee wewe? Huoni anakujaribu? Kitendo cha wewe kuomba ushauri humu kinaonyesha wazi huna uzoefu wa biashara yoyote. Kwa hiyo, inaelekea ukijaribu chochote na hizo fedha utakuwa umejimaliza. Labda huyo jamaa yako anataka akufungulie kesi ya wizi wa kuaminiwa. Be very careful.
 
Back
Top Bottom