Hivi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Geza Ulole, Jan 5, 2012.

 1. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2012
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,079
  Likes Received: 4,022
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Pumbavu kama hili linavyotetea posho ya laki mbili??????

  Ndugai amshukia Frederick Sumaye [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Wednesday, 04 January 2012 21:09[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD]0digg

  [​IMG]Naibu Spika wa Bunge,Job Ndugai

  ASEMA HANA USAFI WA KUBEZA NYONGEZA YA POSHO
  Fredy Azzah
  NAIBU Spika wa Bunge, Job Ndugai amemjia juu Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye kuhusu kauli yake ya posho za wabunge, akisema hakupaswa kuitoa kwani aliwahi kufanikisha kupitishwa sheria ya malipo kwa viongozi wakuu wastaafu ili kujinufaisha akistaafu.Juzi, Sumaye pamoja na mambo mengine, alizungumzia mwelekeo wa taifa kwa sasa na kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015 huku akisema mpango wa ongezeko la posho za wabunge unapaswa kuachwa kwani unaweza kufanya makundi mengine ya utumishi wa umma kudai nyongeza.

  Kauli hiyo ilijibiwa vikali jana na Ndugai ambaye aliwatahadharisha viongozi wastaafu kuwa makini na kauli wanazotoa na kuwataka wale ambao wanataka urais wa 2015 ikiwa ni pamoja na Sumaye waseme sasa badala ya kuwababaisha Watanzania kwa kuzungumza mambo mbalimbali ili wawapende.

  Alisema wakati Sumaye anazungumzia posho za wabunge, sheria ya kuwalipa viongozi wastaafu mafao ilipitishwa wakati akiwa kiongozi wa shughuli za Serikali bungeni na hakuipinga kwa kuwa alikuwa anajiandalia mazingira ya kustaafu.
  "Kwa sasa analipwa asilimia 80 ya mshahara wa waziri mkuu aliyepo madarakani, ni fedha nyingi kuliko hata mshahara wa Naibu Spika (Ndugai kwa sasa), wakati sheria hii inapitishwa alikuwa kiongozi wa shughuli za Serikali bungeni (Waziri Mkuu), alikuwa anajiandalia mazingira ya kustaafu," alisema Ndugai na kuongeza:

  "Sitaki kuendelea kusema sana jinsi ambavyo ananufaika, lakini ninachosema viongozi wastaafu duniani kote inatakiwa wawe makini na kauli zao. Wakianza kwenda kwenye vyombo vya habari na kusema maneno haya haipendezi."
  Alifafanua kwamba badala ya kuzungumzia posho za wabunge pekee ni vyema pia likazungumziwa suala la posho kwa viongozi wote wa umma.

  "Kwa watu wanaotaka kugombea urais mwaka 2015 ni bora waseme sasa. Waache kutubabaisha Watanzania… nasema viongozi wastaafu lazima wawe makini kwa kauli zao, mimi Sumaye ninamheshimu sana na ninatambua haki yake ya kikatiba ya kujieleza," alisema na kumshauri kuwa makini na kauli zake anapozungumza juu ya Bunge kwa sababu yeye pia alikuwa sehemu ya mhimili huo.

  "Yeye ni kama mchezaji mstaafu wa timu hii (Bunge), inatakiwa awe makini sana hawezi kuizungumzia hii timu kama mshabiki mwingine," alisema Ndugai.

  Ndugai alisema posho zilikuwepo tangu enzi za Sumaye akiwa mbunge, naibu waziri na hatimaye waziri mkuu na kwamba kama hoja ni kiasi cha fedha... "Aseme ni kiasi gani wabunge wanapaswa kulipwa."
  Sumaye aliingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 1985 baada ya kushinda ubunge katika Jimbo la Hanang na mwaka 1987, aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Kilimo na Maendeleo ya Mifugo hadi mwaka 1994 alipoteuliwa kuwa waziri kamili katika wizara hiyo.

  "Mimi nakwambia kitu ambacho nakijua na wakati huo nilikuwa bungeni kama mbunge na Sumaye alikuwa akizipokea hizi posho, Rais (Ali Hassan) Mwinyi aliwahi kusema kila zama na kitabu chake, hebu na yeye (Sumaye) atuache na sisi tuandike kitabu chetu," alisema Ndugai.

  Dk Bana abeza
  Akizungumzia kauli ya Sumaye, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana alisema mambo aliyozungumza si mapya na huku akimtaka kutazama kila neno linalotoka mdomoni mwake.

  Dk Bana alisema kauli ya Sumaye kuhusu matumizi ya taasisi ya urais, inaweza kutafsiriwa kwamba inatokana na yeye kuwa na uchungu wa kuikosa alipogombea na Rais Jakaya Kikwete katika uchaguzi wa ndani wa CCM.

  Sumaye katika kinyang'anyiro cha kupenya kura za maoni kwa ajili ya kupeperusha bendera ya CCM baada ya Mkapa, alishika nafasi ya tano na kushindwa kuingia hata tatu bora ambayo waliingia Rais Kikwete, Dk Salim Ahmed Salim na Profesa Mark Mwandosya.

  "Kwanza anavyozungumzia taasisi ya urais hatujui kama ni hii au ni zilizopita, lakini ikumbukwe kuwa aligombea nafasi hiyo akaikosa kwa hiyo kuna uwezekano kuwa ni roho inamuuma," alisema Bana.

  Kuhusu suala la rushwa katika uchaguzi alisema: "Suala hili lilikuwepo kwa muda mrefu na limepigiwa sana kelele, yeye hakuweza kumshauri Rais (Benjamin) Mkapa kuwa watunge sheria ya kupambana na hali hii, lakini sasa hivi Serikali imejaribu inatakiwa aipongeze kwa hilo," alisema Dk Bana.

  Alisema hata baada ya kuundwa kwa sheria hiyo, viongozi wengi wakubwa ikiwa ni pamoja na wale wastaafu hawaonekani kuipigia debe.

  Dk Bana alisema kuundwa kwa sheria ni jambo moja na kinachotakiwa sasa ni utekelezaji wake kufanyiwa kazi.
  Alisema pia ingekuwa jambo jema endapo viongozi wastaafu wangeunda taasisi yao ili waweze kushauri Serikali ili busara zao ziweze kutumika vyema huko... "Yeye ana nafasi kubwa sana ya kuzungumza haya mambo ndani ya chama na pia hata kumshauri Rais moja kwa moja."

  Kuhusu suala la posho kwa wabunge, alisema Sumaye alilizungumza vizuri na inatakiwa aungwe mkono na watu wengine.

  Alichosema Sumaye
  Akizungumza kupitia kipindi cha dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha ITV, Sumaye alisema ongezeko la posho za wabunge linaweza kuchochea makundi mengine kama wanajeshi, polisi, Mahakama na walimu nao kutaka nyongeza, hivyo kumweka Rais katika wakati mgumu kufanya uamuzi.

  "Mwanasiasa mzuri akifanya jambo akiona limewaudhi wananchi anatakiwa aliache, lakini pia kwenye hili huu mkanganyiko wa Spika na Katibu wake na huu ukimya wa Ikulu ni tatizo, tungependa waseme ili umma ujue hali ikoje?" alisema Sumaye.

  Alisema hatua ya Bunge kujipandishia posho ya kikao kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 kwa siku haliingii akilini na kwamba, inakiuka utaratibu uliowekwa na Serikali katika kulipa gharama kwa maofisa wake ikiwa ni pamoja na gharama hizo za fedha za kujikimu.

  "Siyo kwamba napinga posho, wabunge wanastahili posho, lakini kwa kweli kujiongezea kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 siyo sahihi," alisema Sumaye.

  Alisema wakati alipoteuliwa na Rais Benjamin Mkapa kwa Awamu ya Pili kushika wadhifa wa Waziri Mkuu, aligoma kwa sababu alikuwa amekwaruzana na wabunge kuhusu nyongeza ya posho.

  "Nilimwambia wabunge watanikataa kwa sababu nimegombana nao sana juu ya suala la posho lakini akasema lazima uwe na mimi ndipo nikakubali, lazima hili suala liangaliwe mara mbilimbili… leo wabunge mmejiongezea kesho jeshi, polisi na walimu nao watataka, tutafanyaje tusifanye mambo ambayo yatamuweka Rais pabaya," alisema Sumaye.

  Alisema posho ni jambo ambalo kwa sasa limekuwa tatizo kwa serikali na kwamba imefika wakati ofisi za Serikali zimehamia hotelini, lengo likiwa ni watumishi wa umma kutafuta mwanya wa kulipana posho.
  http://www.mwananchi.co.tz/component/content/article/37-tanzania-top-news-story/19058-ndugai-amshukia-frederick-sumaye.html

  WAKATI wengine?????

  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Mgomo wa madaktari nchi nzima wanukia [/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"] Send to a friend[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Wednesday, 04 January 2012 20:57
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]0digg

  Tausi Ally na Nora Damian
  CHAMA cha Madaktari Tanzania (MAT), kimeipa Serikali saa 48 za kutoa malipo ya madaktari wote mara moja ili waweze kuendelea kufanya kazi ya kuwahudumia Watanzania.Wakati MAT ikitoa onyo hilo, mgomo wa madaktari 229 walio katika mafunzo ya vitendo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), jana uliendelea huku madaktari hao wakisisitiza kwamba hawatakuwa tayari kurejea kazini hadi hapo watakapolipwa fedha zao.

  Akizungumza Dar es Salaam jana, Rais wa MAT, Dk Namala Mkopi aliitaka Serikali kuheshimu kazi ya udaktari na huduma za afya zinazotolewa kwa wananchi na iepuke kuwa chanzo cha migogoro ya mara kwa mara katika sekta ya afya.

  "Iwapo wizara itashindwa kushughulikia malipo haya ndani ya saa 48, basi itatulazimu kuitisha mkutano wa dharura kwa madaktari wote nchini ili kutafakari mustakabali wa jambo hili nyeti na yote yanayohusu fani ya udaktari katika taifa letu," alisema Dk Mkopi.

  Dk Mkopi aliwataka viongozi wa wizara na taasisi kuacha kutumia lugha za vitisho wakati kama huu hasa baada ya kushindwa kuwalipa madaktari stahili zao.

  Alisema wamesikitishwa na migogoro na migomo inayoendelea katika hospitali mbalimbali nchini kwa madaktari wanaofanya kazi chini ya usimamizi ‘Interns' na kwamba, Serikali haijawalipa malipo yao kwa kipindi cha mwezi mmoja hadi mitatu.

  Dk Mkopi alifafanua kwamba hali hiyo imewafanya washindwe kuendelea na kazi yao ya kuokoa maisha ya Watanzania wasiokuwa na hatia.

  "Ikumbukwe kwamba madaktari hawa walio chini ya uangalizi ndiyo uti wa mgongo wa utoaji huduma katika hospitali wanazofanya kazi, hasa ikichukuliwa kuwa wao ndiyo wa kwanza kumwona mgonjwa na kumpa matibabu kabla ya kuonwa na madaktari bingwa walio wachache," alisema Dk Mkopi.

  Aliongeza kwamba baada ya kufanya utafiti wa kina, chama hicho kimebaini kuwa hospitali tano za rufaa nchini tayari madaktari hao wameshindwa kufanya kazi kutokana na kutolipwa fedha zao.Dk Mkopi alizitaja hospitali hizo kwamba ni pamoja na ile ya Muhimbili, Hospitali ya Bombo, Tanga; Mount Meru Arusha, Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na Hospitali ya Manispaa ya Temeke.

  Katika maeneo ambayo madaktari wanaendelea kufanya kazi alisema imebainika ni kutokana na vituo, hospitali au halmashauri husika kuamua kuwakopesha wataalamu hao ili kuwawezesha kuendelea na maisha yao ya kila siku huku wakitoa huduma wakati ufuatiliaji ukiendelea kwenye Serikali Kuu.

  Chama hicho pia kimebaini kuwa hali hiyo inaenea katika hospitali nyingine zenye madaktari na inaleta mzigo kwa madaktari bingwa na waandamizi na kuonya kuwa inaweza kuleta mgogoro katika fani yote ya udaktari nchi nzima."Chama kinatafsiri kitendo cha kutowalipa madaktari malipo yao na kuwafanya waishi kwa shida kwa muda huo wote kuwa ni kitendo cha dharau kwa fani ya udaktari na huduma wanazotoa kwa wananchi," alisema na kuongeza:

  "Pia ni udhalilishaji wa hali ya juu kuwaacha madaktari waishi kwa kuombaomba huku wakitoa huduma kwa wananchi. Ni jinsi gani Serikali isivyojali huduma za afya kwa wananchi inaowaongoza."

  Alisema chama kinalaani kitendo cha Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa jamii, kutowalipa madaktari malipo yao halali hadi kufikia mgomo unaowafanya wananchi kukosa huduma stahili za matibabu.

  Dk Mkopi aliitaka jamii na Serikali ielewe wazi kuwa madaktari kuwepo kazini bila malipo kwa muda mrefu ni uvunjifu wa haki za binadamu, kinyume na kiapo cha udaktari na kusababisha utoaji wa huduma hafifu na vitendo vya uvunjifu wa sheria kama kukaribisha mazingira ya rushwa.

  Alisema sehemu ya kiapo cha udaktari inayozungumziwa inasema: "Wakati nikishika kiapo na ijaliwe kwangu kufurahia maisha na kazi yangu, jamii inikumbuke na kuniheshimu nikiwa hai au nimekufa."

  Alisema wanapinga unyanyasaji unaofanywa na wizara kwa wataalamu wake na kwamba Serikali iwe na mipango endelevu na ya muda mrefu katika kulipa stahili za wafanyakazi ili kuepuka kufanya kazi kwa zimamoto kama inavyofanya sasa. Dk Mkopi alisema chama kinaona wataalamu hao hawana hatia ya uvunjifu wa kiapo chao katika kutoa huduma kwa Watanzania kutokana na Serikali kutokutimiza wajibu wake kama inavyoelezeka kwenye kiapo na makubaliano ya kazi.

  Hata hivyo, alisema wanasikitishwa na matokeo yanayotokana na mgogoro huo kwa wananchi wasio na hatia na taifa kwa ujumla na kuzipongeza hospitali na halmashauri zilizoamua kuwalipa malipo yao ili kuepusha migogoro isiyokuwa ya lazima.

  Mgomo Muhimbili
  Kwa upande wa Muhimbili, hali bado ni tete baada ya madaktari wanafunzi kuendeleza mgomo wao kushinikiza Serikali iwalipe posho zao. Mgomo huo ulioanza juzi unahusisha madaktari 229 katika kada za tiba ya vinywa, wafamasia, maabara na dawa ambao wanaidai zaidi ya Sh176 milioni.

  Jana katika hospitali hiyo kulikuwa na kundi kubwa la madaktari hao wakiwa wamekaa katika jengo lao huku wengine wakiwa wamejikusanya katika makundi tofauti.

  Mmoja wa viongozi wa madaktari hao, Jackson Nyabusani alisema hadi jana malipo yao yalikuwa hayajafanyika kama ambavyo Serikali iliahidi.

  Ahadi ya Dk Mtasiwa
  Juzi, Mganga Mkuu wa Serikali, Deo Mutasiwa aliwaahidi madaktari hao kuwa posho hizo zingeanza kulipwa jana na kwamba zilichelewa kutokana na taratibu za Serikali katika malipo.

  "Tuliahidiwa leo (jana) tungeanza kulipwa posho zetu lakini hadi sasa hakuna kitu, kila nikienda kwa mhasibu mkuu ananiambia bado," alisema Nyabusani.
  Alisema suala hilo licha ya kuwaathiri wao, pia linawaathiri wagonjwa kwani kwa kiasi kikubwa madaktari wanafunzi ndiyo wanaotoa huduma katika hospitali hiyo.

  Alisema idadi kubwa ya madaktari hao wametoka mikoani huku wengine wakiwa na familia zao na kwamba wanategemea posho hizo kwa ajili ya kutafuta makazi pamoja na gharama nyinginezo.

  Kiongozi huyo alisema kati ya madaktari wanafunzi 229 wanaohudumia hospitalini hapo, madaktari 50 tu ndiyo wanaokaa katika hosteli zilizopo hospitalini hapo na wengine wanaishi mitaani.
  http://www.mwananchi.co.tz/habari/4-habari-za-kitaifa/19056-mgomo-wa-madaktari-nchi-nzima-wanukia

  Na wengine.......

  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Madeni yasipolipwa shule hazifunguliwi asema Mkoba [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Wednesday, 04 January 2012 20:53 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  Gedius Rwiza
  MVUTANO kati ya Chama cha Walimu Tanzania (CWT) na Serikali ,kuhusu malipo ya madeni ya walimu, unaonekana kushika kasi baada ya Rais wa chama hicho, Gratian Mukoba, kupinga kauli ya Serikali kwamba wamekubaliana kusitisha mgomo wa walimu uliopangwa kufanyika Januari 9 mwaka huu.

  Jana Naibu Waziri Tamisemi anayeshughuliki Elimu, Kasim Majaliwa aliliambia gazeti hili kuwa mgomo huo umesitishwa baada ya Serikali kukutana na viongozi wa CWT Desemba 25 mwaka jana na kukubaliana wafanye hivyo.

  Hata hivyo kwa upande wake, Mukoba alipinga kauli hiyo ya waziri."Ni kweli tulikutana na Serikali lakini sisi hatukukubali kusitisha mgomo kwa sababu madai yetu hayajatekelezwa," alisema Mukoba.

  Alisema Serikali imekiuka makubaliano kwamba fedha za walimu zingelipwa kati ya Novemba na Desemba mwaka jana.Huko nyuma Serikali ilikuwa imekubaliana na CWT, kwamba fedha hizo kiasi cha Sh49.6 bilioni zingelipwa katika Novemba na Desemba lakini baada ya kufanya tena uhakiki ilibaini kuwa fedha hizo zimeongezeka hadi kufikia Sh52 bilioni.

  Uhakiki huo ulikamilika Desemba 2 mwaka jana baadaye Serikali ilitangaza kuwa fedha hizo zitalipwa kwa awamu mbili,Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mfunzo ya Ufundi, Selestin Gisimba, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, sababu za kusogeza mbele malipo hayo ni kutaka kufuata utaratibu wa makato ya kodi ikiwemo mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kupitia katika akaunti zao.

  "Tumeishagundua ujanja wa Serikali wamefanya makusudi kusogeza siku mbele ili walimu wafungue shule na mgomo uyeyuke lakini napenda kusema kwamba tayari ujanja huo tumeufahamu na kama ikishindwa kulipa fedha hizo mwezi huu shule hazifunguliwi,"alisema Mukoba.

  Alisema kwa sasa makubaliano hayo hayawezi kubadilika kwa sababu suala la uhakiki limeishamalizika na kwamba kinachotakiwa ni kulipa fedha za walimu.[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  http://www.mwananchi.co.tz/news/4-habari-za-kitaifa/19053-madeni-yasipolipwa-shule-hazifunguliwi-asema-mkoba.html
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Has this country gone to dogs?????????????


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Ganja bhana
   
 3. Tai Ngwilizi

  Tai Ngwilizi JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2012
  Joined: Apr 20, 2010
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  mwenye kisu ndio mla nyama...sasa wasipofanya hivyo hela za kampeni watazirudisha vipi? na faida juu lazima ipatikane, imebaki miaka minne and counting, who knows kitakachotokea 2015....
   
Loading...