Hivi zile posho/bonasi za milini 60 walizojilipa jamaa wa TANESCO zipo kisheria?

mbere

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
6,897
2,000
Kwamba sheria na taratibu zinawataka kujilipa bonasi kama walivyofanya?
Maana wamegombezwaaa kweli!!
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
24,953
2,000
Kwamba sheria na taratibu zinawataka kujilipa bonasi kama walivyofanya?
Maana wamegombezwaaa kweli!!
Sheria ya ajira na mahusiano kazini inaruhusu Mkataba wa hali bora ya kazi, therefore iko kisheria.
Kitu kama hiki hapa
MKATAB A WA HIARI WA HALI BALI BORA KATI YA MAMLAKA YA MAJI SAFI NA MAJITAKA MWANZA (MWAUWASA) CHAMA CHA WAFANYAEAZI WA SERIKALI KUU NA APYA (TUGHE) TAWI LA MWAUWASA
1.0 UTANGULIZI
Sisi Wanachama wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) Tawi la MWAUWASA tujulikanao hapa kama "Chama cha Wafanyakazi" na Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mwanza ijulikanayo hapa kanha Mwajiri, kwa hiari yetu na katika hali ya maelewano tumefikia makubaliano katika masuala yaiiyomo katika Mkataba huu ambayo yanaweka hali bora zaidi za kazi kwa Wafanyakazi walioajiriwa na Mamlaka hii.

2.0 UTAMBUZI
Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE) kinatambua Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mwanza (MWAUWASA) KAMA Mwajiri, kadhalika uongozi wa Mamlaka unakitambua Chama cha TUGHE kama chombo maalum cha kutetea haki na maslahi ya Wafanyakazi.

3.0 TAFSIRI
1. Familia -Itazingatia Tafsiri ya sharia ya kazi Tanzania

2. Mwajiri - Mamlaka ya Maji safi na Maji taka Mwanza.

3. Mfanyakazi -Mwajiriwa yeyote wa kudumu na wa mkataba katika Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mwanza kwa mujibu wa sharia

4. Menejimenti -Menejimenti ya Mamlaka kwa mujibu wa kanuni za uundaji wa Mamlaka

5. Mamlaka - Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mwanza.

6. PPF - Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma.

7. NSSF - Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii.

8. LAPF - Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mtaa.

4.0 WAHUSIKA
1. Mkataba huu utawahusu wafanyakazi wote walioajiriwa katika masharti ya kudumu kwenye Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mwanza.

2. Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mwanza.

5.0 MUDA WA KUANZA MKATABA
1. Mkataba huu utaanza kutumika kuanzia tarehe ya kusainiwa utadumu kwa muda wa miezi 24 kuanzia tarehe hiyo.

2.Mkataba unaweza kufanyiwa marekebisho ndani ya kipindi kilichotajwa na kipengele cha 5.1 ili mradi tu upande wowote wenye kusudio la kufanya hivyo uwe umetoa taarifa ya miezi mitatu kwa maandishi na pande zote ziwe zimekubaliana na kusajili marekebisho hayo.

6.0 KAMATI YA MAJADILIANO
1. Kutakuwa na Kamati ya Majadiliano ambayo itaundwa na wajumbe 4 watakaoteuliwa na Mwajiri na wajumbe 4 kutoka Tawi la Wafanyakazi. Kamati itachagua Mwenyekiti kutoka miongoni mwa wajumbe. Maamuzi ya Kamati yatafanyika kwa kufuata wingi wa kura. Endapo kura zitalingana, Mwenyekiti atakuwa na kura ya ziada ya uamuzi.

2. Kazi kuu ya Kamati itakuwa kama ifuatavyo: -

(i) Kupokea na kufanyia kazi maoni ya marekebisho ya Mkataba huu.

(ii) Kujadili na kuafikiana juu ya utaratibu wa upunguzwaji wa wafanyakazi.

7.0 AJIRA
Wafanyakazi wa Mamlaka wataajiriwa kwa mshahara wa mwezi katika masharti ya kudumu na ya mkataba kwa kufuata taratibu zinazofafanuliwa na kifungu hiki.

1. Kipindi cha Majaribio:

Wafanyakazi watakaoajiriwa watakuwa katika kipindi cha majaribio cha mwaka mmoja (miezi 12) kabla ya kuthibitishwa katika Ajira.

2. Malipo ya Uzeeni:

(i) Kila mfanyakazi atapaswa kujiunga na kuchangia kwenye mfuko wa hifadhi ya jamii au pensheni kama ifuatavyo: -

(a) NSSF, kwa watumishi walioajiriwa katika masharti ya 'Operational Services' au Mkataba.

(b) PPF, kwa watumishi walioajiriwa katika masharti ya kudumu na pensheni.

(ii) Endapo mtumishi atabadilishiwa masharti ya Ajira atakuwa na haki ya kuchagua kuendelea kuchangia katika mfuko wa awali au mfuko stahili kutokana na mabadiliko hayo.

3. Haki ya Wafanyakazi katika mabadiliko:

(a) Endapo Mamlaka itafanyiwa marekebisho ya kukodishwa au kuuzwa viwango vya mshahara na haki za Wafanyakazi watakaobaki kwenye Ajira katika Taasisi mpya itakayoundwa kwa wakati huo, zitatambuliwa na kuheshimiwa na Mwajiri mpya kwa mujibu wa mkataba huu hadi hapo Taasisi hiyo itakaposaini Mkataba mpya na wafanyakazi hao.

8.0 KUACHA KAZI
Iwapo mfanyakazi ataamua kuacha kazi kwa hiari yake, hatahusika na haki zilizoainishwa kwenye kifungu cha 11.

9.0 UPUNGUZWAJI WA WAFANYAKAZI
Kila mfanyakazi aliyepunguzwa atapewa mkono wa kwa heri kwa kulipwa mishahara ya miezi minne (4) kwa wafanyakazi walio kwenye masharti ya muda usio maalum (Unspecified Period Contract) na kwa wale walio kwenye mkataba wa miaka 4 na 5 watalipwa mishahara ya miezi 5 (mitano).

10.0 LIKIZO YA MWAKA / DHARURA
1. Kila mfanyakazi atawajibika kwenda likizo kila mwaka.

2. Mfanyakazi atalipwa Tshs. 50,000.00 (elfu hamsini tu) kama posho ya likizo kila mwaka anaoenda likizo.

3. Mwajiri atathibitisha utoaji wa likizo ya dharura kwa wafanyakazi na itakatwa katika likizo ya mwaka.

11.0 KIINUA MGONGO
1. Mfanyakazi aliyeajiriwa katika masharti ya muda usio maalum na wa mkataba kuanzia miaka 4 (minne) na kuendelea anayestaafu kwa mujibu wa mkataba huu au sheria ya kazi atakuwa na haki ya kupewa mkono wa kwa heri kama ifuatavyo: -


Umri kazini Kiasi
Miaka 3-7
Miaka 8-15

Miaka 16 - 21

Miaka 22 na kuendelea

Mshahara miezi 5
Mshahara miezi 7

Mshahara miezi 10

Mshahara miezi 12

12.0 TIJA / UFANISI
1. Pande mbili zitaweka mipango ya kazi iliyo mizuri na kutoa elimu kwa wafanyakazi wa ngazi zote kuhusu utendaji bora wa kazi pamoja na jinsi wafanyakazi walivyo na jukumu kubwa la kuongeza ufanisi na tija ndani ya Mamlaka na Umma kwa ujumla.

2. Mwajiri na Tawi la Chama cha Wafanyakazi watakubaliana juu ya vigezo vya kuchagua wafanyakazi hodari na viwango vya ufanisi na motisha.

13.0 RAMBIRAMBI
Rambirambi wakati wa misiba itatolewa na Mwajiri kama ifuatavyo: -

(i) Mfanyakazi akifariki, familia itapewa rambirambi ya Tshs. 500,000.00 (Laki tano tu).

(ii) Mke/Mme na mtoto akifariki mtumishi atapewa rambirambi ya Tshs.300,000 (Laki tatu tu).

(iii) Baba au Mama akifariki mtumishi atapewa rambirambi ya Tshs. 200,000 (Laki mbili tu).

14.0 MOTISHA
1. Mwajiri atamchangia mfanyakazi kodi ya nyumba na usafiri kwa asilimia ambayo kwa ujumla wake haitazidi asilimia 10 ya mshahara wa mfanyakazi husika. Motisha hii haitawahusu wafanyakazi wanaostahili kupewa nyumba kwa gharama za Mamlaka kwa mujibu wa Kanuni za utumishi za Mamlaka.

2. Kila mfanyakazi atapata posho kwa ajili ya malipo ya maji. Kiwango cha posho kitakuwa sawa na mita za ujazo 24 za maji kwa mwezi isipokuwa kwa wale wanaostahili kulipiwa gharama za maji.

3. Malengo yanapovukwa kwa mwaka, itatolewa motisha itakayogawanywa sawa kwa watumishi wote baada ya kutoa gharama za uendeshaji. Suala la kiwango na namna ya kutoa motisha hii itaamuliwa na Bodi baada ya Menejimenti kupeleka mapendekezo. Kwa vyovyote vile motisha hii haitazidi kiwango kilichoidhinishwa kwenye 'Memorandum of Understanding’ ya wakati husika kati ya Mamlaka na Wizara inayoshughulikia Sekta ya Maji.

15.0 HATI SAFI YA UKAGUZI
Ikiwa Mamlaka itapata Hati Safi ya Ukaguzi wa Mahesabu yake, wafanyakazi watastahili kupata Motisha. Suala la kiwango cha motisha hii litaamuliwa na Bodi baada ya Menejimenti kupeleka mapendekezo. Menejimenti itapanga namna bora ya kuitumia motisha hiyo.

16.0 SARE ZA KAZI
1. Wafanyakazi wote watastahili kupata jozi mbili za sare kila mwaka.

2. Vifaa vya kinga kwa ajili ya shughuli za kazi kulingana na aina ya kazi vitatolewa kwa watumishi wanaostahili.

17.0 POSHO YA KAZI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU
1. Wafanyakazi wa Kitengo cha Majitaka na Kitengo kidogo cha Madawa watapewa posho ya Tshs. 20,000.00 (elfu ishirini tu) kwa mwezi kwa sababu ya kufanya kazi katika mazingira magumu pamoja na 1/2 lita ya maziwa kwa siku zote za kazi.

2. Wafanyakazi wengine (mfano; mafundi mitambo, mafundi bomba na madereva) watalipwa posho ya Tshs. 5,000.00 (elfu tano tu) kwa utaratibu wa kazi maalum iwapo itawalazimu kufanya kazi katika mazingira magumu.

18.0 TUZO LA UTUMISHI WA MUDA MREFU
(a) Mfanyakazi wa Mamlaka ambaye atakuwa amemaliza miaka 15 katika utumishi wa Mamlaka atatunukiwa tuzo ya utumishi wa muda mrefu kwa kupewa cheti pamoja na saruji mifuko 50 na 'bundle' 3 za mabati ya kuezekea nyumba.

19.0 HITIMISHO, MAKUBALIANO NA SAINI
Mkataba huu utatekelezwa pamoja na Sheria ya Kazi iliyopo na Kanuni za Utumishi wa Mamlaka. Aidha, Mkataba huu hautamzuia Mwajiri kuboresha

zaidi hali za kazi.

Kwa ajili ya kukamilisha makubaliano na hiari yetu pande zote mbili katika Mkataba huu tunaweka saini zetu kama ilivyooneshwa hapa chini: -

Kwa niaba ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Mwanza (MWAUWASA)

Kwa niaba ya Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE)

MENEJA UTAWALA NA UTUMISHI
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom