Hivi yanga na simba mwenendo huu mpaka lini..? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi yanga na simba mwenendo huu mpaka lini..?

Discussion in 'Sports' started by kajukeg, Jul 27, 2010.

 1. kajukeg

  kajukeg Member

  #1
  Jul 27, 2010
  Joined: Jul 22, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni miaka kadhaa sasa imepita migogoro ya usajili ktk vilabu vya simba na yanga imekuwa ni hadithi zisizokuwa na mwisho.

  nakumbuka miaka ya nyuma kidogo usajili wa victor costa ulivyosumbua akili za watu baada ya costa kusaini form mbili za usajili,za yanga na za simba.kutoka hapo tukasikia ya Athumani Idd,then ya uhuru selemani na John njoroge mwaka jana.

  kilichonisikitisha kabisa jana katibu mkuu wa yanga lawrance mwalusako anasema yanga wanakubali kwamba ni kweli wamewaacha wachezaji watano akiwemo john njoroge,wisdom ndlovu na wengineo kimakosa kwani walikuwa bado wana mkataba na klabu hiyo,huku akitoa visingizio kibao juu ya TFF kwamba walibadili taratibu za usajili kwa haraka mno.

  swali langu linakuja uongozi wa yanga haukujua hilo? hivi usajili wa bongo una taratibu kweli au bora liende. na hawa viongozi waliopewa dhamana ya kuzisimamia klabu hizi hivi wanaelewa umuhimu na maana ya dhamana zao au na wao ndo bora liende cha mfukoni kiingie?

  Jamani kwa mtindo huu soka la bongo litakuwa kweli kama hata mfumo wa usajili tu ni mbovu...
   
Loading...