Hivi ya Membe yameishia wapi?

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Dec 6, 2006
3,020
577
Wale aliodai Membe kwamba wamemkariri ndivyo sivyo na akadai wakiri makosa, je wameshakiri? Sijawasikia bado na wala Membe mwenyewe sijasikia amechukuwa hatua gani. Au wameishiana kiana tu kama desturi ya CCM?

Makamba huyoo naye kaja ati CCM lengo lao ni moja tu: CCM kubakia na dola na sio vinginevyo, kesho akitangazwa atadai hakuwahi kusema hayo na atadai mabilioni, maana sasa watanzania wanawashitukia ccm kila wajapo na mbinu chafu zao kuwaibia wananchi.

Juzi nimeambiwa na mfanyakazi mmoja wa TANESCO kwamba bili za umeme sasa zinachakachuliwa sana ili kupata pesa ya kuilipa dowans, na kweli nilitoa 5000/= nikapata units 8 tu. Partamu hapo hata sina hamu, inabidi kutafuta mbinu muafaka ya kuwachomolea umeme TANESCO kufidia umeme wanaotuibia kila siku, maana uaminifu nchi hii ni balaa. Wizi ni sifa ya maisha bora kwa kila mtanzania.
 
Back
Top Bottom