Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,742
- 215,933
Bi shost aliolewa na mzungu miaka mitano iliyopita, wakaenda kuishi Uingereza. Ingawa hawajanikiwa kupata mtoto, wanaishi kwa mapenzi makubwa sana. Walinialika nikawatembelee kipindi cha Noeli. Mzii akiwa ametoka shost akaanza kunipa michapo.
Miaka miwili iliyopita bibie alipata kazi mpya, lakini kabla ya kuanza kazi walitaka the most uptodate medical history ambayo ni full check up. Bidada alipata mshutuko majibu yalipokuja ni HIV+. Baada ya kurudi nyumbani na masikitiko akamueleza mumewake ambae nae alikuwa na mstuko mkubwa. Kesho yake na mume akaenda kupima lakini akakutwa negative.
Ilibidi akawaambie kule kwenye kazi mpya, akijua kibarua kimeota mbawa tayari, lakini cha ajabu wakamwambia aanze matibabu na Dr wake awahakikishie kwa maandishi kuwa yuko kwenye matibabu hawana sababu ya kutokumuajiri.
Bishost akaanza matibabu, ingawa hakuwa mgonjwa lakini anasema alikuwa anahisi kuchoka mara zote, na ugonjwa ulikuwa umedhoofisha sana ndani pasi yeye kujijua. CD4 zilikuwa chini sana na viral load ilivuka laki moja.
Alianza matibabu na combination ya vidonge vitatu, baada ya miezi miwili akaenda kupimwa, viral load ilikuwa haionekani. Baada ya miezi sita kupimwa CD4 zimepanda kwa kiasi cha kuridhisha, baada ya mwaka mmoja Dr wake akaanza kumpunguzi dawa moja, lakini akawa anapima damu kila baada ya miezi mitatu, baada ya miezi mitatu mingine akapunguziwa dawa moja akawa anakunywa kidonge kimoja tu, baada ya miezi mingine mitatu akaambiwa aache kunywa dawa waangalie, ananiambia ni mwaka mmoja sasa tangu ameacha kunywa dawa na hakuna viral load.
Siwezi kumsimulia mtu mwingine hii story, maana ameniambia hata ndugu zake hawafahamu. Sasa jamani ni kuwa wazungu wamegundua dawa lakini hawatuambii?