Hivi watu wa Mbeya ni vichwa sana?

Mmmmh!! Maybe!!!
Unaweza ukawa na point hapa! Watafiti wa mambo wa lishe na udaktari na wafanye utafiti. Katika kusoma kwangu shule ya msingi hadi UD, wengi wa watu wa Kilimanjaro, Bukoba na Mbeya walikuwa wanawaka sana darasani, mara nyingine kwa jinsi ya kutisha. Sasa nagundua kwamba hawa jamaa wana one thing in common - wanatoka mikoa yenye kulima ndizi!

Jamani, labda kula ndizi kunaongeza brain power!
 
He kumbe!!!
Mara baada ya Uhuru mwaka 1961, serikali iliamuru shule ya st. Michael's and st. George's Iringa iliyokuwa mahususi kwa watoto wa kizungu ichukue pia vijana wa kiafrika waliokuwa na uwezo kuchuana na wale watoto wa kizungu; wengi wa wale waliochaguliwa kutokana na mitihani waliofanya nchi nzima walikuwa wa kutoka mikoa ya Mbeya, kilimanjaro na Kagera!!Ukweli ndio huo mpende msipende na ndio maana Nyerere alikuwa anawabania sana watu wa kutoka huko na kuwashabikia watu wa makabila madogo kwa kuogopa watamfunika!!
 
wanakwambia aaaa we huwezi ukanizalau hata kama we ni kiongozi mkubwa na unahela. Hivyo ni vitu vyako mwenyewe

Kulikuwa na jamaa wa Mbeya nilisoma naye Tabora, akiwa darasa moja na Harun Kimaro Raisi wa wanafunzi UDSM aliekimbia nchi wakati wa mgomo wa enzi za Mwinyi. Huyu jamaa wa Mbeya, pamoja na Harun Kimaro na wenzao kama watatu hivi, wakati wanakaribia kabisa kumaliza form four, waliamua kutetea haki za wanafunzi wengine waliobaki, japo wao walikuwa wanamaliza shule. Walifukuzwa shule na kuruhusiwa tu kurudi kufanya mtihani wa mwisho. Na bado jamaa wakafaulu sana! Tulikuwa tunawaita "watu wenye siasa kali" katika kutetea wanafunzi.
 
Aaah, Mwakasendo! Huyu jamaa alikuwa judge nadhani. Nakumbuka kulikuwa na issue kubwa tu juu yake. Hebu tukumbushane jamani.

Hee, kweli nae jaji Mwakasendo alipata maradhi ya ajabu ajabu tukampoteza wakati huo kulikuwa na tetesi kuwa angekuwa CJ!!! Watawamaliza; watu wa Mbeya afadhali muamue nchi yenu iwe Malawi!!!
 
Hee, kweli nae jaji Mwakasendo alipata maradhi ya ajabu ajabu tukampoteza wakati huo kulikuwa na tetesi kuwa angekuwa CJ!!! Watawamaliza; watu wa Mbeya afadhali muamue nchi yenu iwe Malawi!!!

Malawi? Acha kuwapoteza watu wa Mbeya. Unataka wahamie Malawi halafu warudi Tanzania kama shamba boys na walinzi? Maana najua hapa mjini Dar wapo Wamalawi wengi tu wameimbia kwao!
 
Unajua nimekuwa nafuatilia jinsi ambavyo hadi sasa nimeona watu wa Mbeya wanakuwa na mwamko sana katika kupigania haki za watu, sijui kama wana kitu fulani kinachowafanya wawe hivyo. Ajabu ni kwamba mara nyingi wanakuwa victimised

1. Gibson Mwaikambo - alitaka kujiengua CCM kuingia Chadema, akapata "accident" iliyomuua siku usiku wa wa kuamkia kutangaza kujivua gamba kuingia Chadema

2. Prof. Mwandosya - tunajua yasiyojulikana yaliyomkuta

3. Dr. Mwakyembe - Tunajua yale ambayo hakuyaweka wazi yaliyomkuta na jidihada zake

4. Dr. Ulimboka - tunajua yaliyomsibu

5. Mfianchi
 
Watu wanaoweza kuiongoza hii nchi na kutupeleka kwenye nchi ya maziwa na asali ni wa kutoka mikoa mitatu tuu,MBEYA, KAGERA na KILIMANJARO nadhani hata kwenye baraza la mawaziri la sasa mnaona utendaji wao.
mmh!huu ukabila sasa.kwa hili mwanJF Mwenzangu hata sikuungi mkono.ukishaanza kusema hivyo wasukuma,wahaya,wazaramo.....na sisi wangoni tukianza itakuwaje.tusife huko jamani.
 
Labda Nyerere aliwabania hawa jamaa kwa sababu alijua tabia yao ya kubebana aka ukabila,wakipewa kitengo nyeti basi watajaza ndugu zao hata kama hawaqualify kushika hizo nafasi.
 
Labda Nyerere aliwabania hawa jamaa kwa sababu alijua tabia yao ya kubebana aka ukabila,wakipewa kitengo nyeti basi watajaza ndugu zao hata kama hawaqualify kushika hizo nafasi.

Labda wameona wakifanya kazi na makabila mengine wanawaangusha. Kumbuka hata Wachaga na Wahaya wanatuhumiwa ukabila. Basi labda sie makabila madogo kuna sifa wanaona tunakosa je?

Nakumbuka Mwaikambo pale NIC aliwahi kusemwa mkabila. Unajua alijibu nini? Zunguka ofisi zote uniletee Mnyakyusa ambaye hana sifa za nafasi aliyopewa nitamfukuza kazi!
 
Mpaka Nyerere anaondoka madarakani,sehemu kubwa ya wafanyakazi wa Ikulu wakiwemo usalama wa taifa walikuwa ni kutoka Mbeya.Inaaminika watu hawa ni watunza siri wazuri.
 
Hivi Mbunge wa Jimbo analo toka Dr Steven Ulimboka Mbeya ni nani? na Dari salama Mbunge wake ni nani wa kinondoni au wa Ilala? na wanasema nini kuhusu hali ya mpiga kura wao/
 
pride & prejudices..kama wao ni vichwa sie wengine ni shingo au vidari? ficheni upumbavu wenu.
 
Mmhh...kuna kaukweli hapa. Sikuwahi kusoma na mtu kilaza kutoka mikoa hiyo kuanzia sekondari hadi chuo kikuu!!

you prove it right...yaaan jamaaa yana uwezo wa asili ubongon mwao,inshort wanajua kutumia mentality yao!
 
Back
Top Bottom