Hivi wanaume wengine mkoje?

Hivi wanaume wengine mkoje?

Mbona kule juu umeandika kwa CAPS lakini hapa chini umeandika kwa herufi ndogo....au ulitumia kibodi tofauti yakhee?

Kumuhadidhia mtu akaamini seriously ni ngum maana hata sisi tumeona kama movie, na dada ndo kaachwa mwanaume hataki kujua lolote, shia inakuja hivi huko aliko ndo yule dada mwingine yupo sijui wataendelea? mh majanga
 
habari zenu wana mmu, nina jambo nataka kushare na nyinyi then wake kwa waume mseme ingekua wewe ungejiskiaje.

Nina jirani yangu ambaye ni mwanamke ambae yuko karibu sana na mungu, dada huyo ameolewa lakini mwaka jana mumewe alihamishiwa mkoa mwingine kikazi, kwakua dada anafanya kazi mkoa mwingine aliamua kuvumilia tu kwa kutohama na mumewe ili abaki na watoto na kuendelea na kazi anayofanya kwa kuepusha kuhama hama.

Kama tunavyofahamu maofisi kwetu watu tumechanganyikana na kuzidiana umri pia, lakini linapokuja suala la urafiki hua hatuchaguwi hivyo basi hata kwa jirani yangu huyo imetokea akawa ni rafiki na mama mtu mzima ambae ni boss wake pia. Mama amekua akimueleza mkoa alioko mumeo ndipo mwanangu wa kike anapofanyia kazi ipo siku utamuona.
Alimwambia hivyo kwakua maisha ya huyo dada na mumewe ni yakutembeleana kila weekend kwakua wako mbalimbali ndo makubaliano yao, sasa juzijuzi kikatokea kituko jirani alisafiri kikazi kurudi yule mama akamwambia mwanangu anatolewa mahari ningeomba usiache kuja, kweli dada akaenda kwenye sherehe akiwa kama ndo dada mkubwa wa huyo binti kwani mama ndo alivyomuomba, wakiwa chumbani wamejiandaa na sare zao wageni walifika, na taratibu zikaendelea, basi ikafika saa ya muolewaji kutolewa akiwa na mshenga wake ambae ndo jirani alieshika nafasi ya dada wamejifunika bwana harusi kufunua mwari akakosea, akatoa faini kufunua tena akapatia kila mtu akashangilia

hee jirani kutahamaki muoaji ni mume wake wa ndoa tena ya kanisani, dada akaishiwa nguvu, akakaa chini watu wakajua ni mgojwa kwakua alikua mjamzito mimba ikiwa ni ndogo, basi ikabidi apelekwe chumbani then dr akaitwa, mimba ikatoka kwa mshtuko na yule mume akajikausha kama sio yeye, badae jirani akaomba kabla hajaenda hosptal kusafishwa aongee na familia na muoji akiwepo, ndo akawaaambia huyu muoaji ni mume wangu wa ndoa na hawa watoto ni wakwetu, mama wa biharusi na biharusi mtarajiwa wakakosa nguvu na mama akalia kwa uchungu sana akiomba msamaha kwamba hakuwahi kumjua mume wa huyo dada kama angelijua hilo angekataa posa ilivoletwa, muoji akasema ndio mi ni mumeo ila sikutaki tena namtaka huyu, mama bi muolewaji akakasirika sana na wazee wakarudisha mahari na kumtimua huyo baba.

Naombeni michango yenu nyie mnalionaje hilo, ni haki kweli kama humtaki mtu kwanini usimwambie?

hiyo ni ajali kazini hakuna mbaya
 
Sioni kosa lake! si huyo mwanamke naye aolewe? mbona mnadai haki sawa nyie?
Kama munaona haiwezekani basi msidai haki sawa!!!!!!!!!!
 
Ukishangaa ya musa utaona ya firauni!!Dunia hii ya sasa haaa mi hoi hapa!!!
 
kwa hiyo umeandika kwa herufi kubwa kuonesha msisitizo?
tukushauri nini sasa?
au we ndo hiyo njemba iliyotaka kuoa tena huku ukijua ina mke na watoto kadhaa?
Ondoa utata sema usikike
 
kwa hiyo umeandika kwa herufi kubwa kuonesha msisitizo?
tukushauri nini sasa?
au we ndo hiyo njemba iliyotaka kuoa tena huku ukijua ina mke na watoto kadhaa?
Ondoa utata sema usikike



Ungesoma ungeelewa acha kupiga kelele, kama hujui kusoma herufi kubwa chapa mwendo huko hujaitwa kwa jina, na utakua wewe haswa ndo hiyo njemba mbona kime kuuma shame on you
 
Ungesoma ungeelewa acha kupiga kelele, kama hujui kusoma herufi kubwa chapa mwendo huko hujaitwa kwa jina, na utakua wewe haswa ndo hiyo njemba mbona kime kuuma shame on you

Una jazba?
Mbona hujibu swali?
Haya subiri basi huo msaada unaotafuta tuone kama utaupata
 
Back
Top Bottom