Hivi unadhani ni kwanini vyeti ni muhimu katika ulimwengu wa leo?

Hivi unadhani ni kwanini vyeti ni muhimu katika ulimwengu wa leo?

The redemeer

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2025
Posts
4,780
Reaction score
8,155
Kama umefanya upembuzi yakinifu juu ya suala la Ajira na fursa za kiuchumi, basi utakubaliana na mimi kuwa jamii ya sasa imefungwa katika fikra ya Vyeti.
Huwezi pata Kazi isipokuwa una cheti kinachodhihirisha kuwa umepata maarifa kutoka taasisi fulani.

Katika ulimwengu wa sasa, cheti kimekuwa ndio kigezo kikuu (Main Credential) cha Kuhakiki kama mtu ana elimu ama lah!
Serikali na taasisi zimeunda mifumo ya sheria na leseni ambapo huwezi kufungua biashara fulani au kutoa huduma fulani bila kuwa na cheti (mfano: udaktari, ualimu, uhandisi n.k).

Yaani ni kama wanatumia mbinu hii kujiridhisha na Ujuzi wako– huna vyeti, huna sifa!

LAKINI, kwanini vyeti?

Hakika Kuna siri kubwa nyuma ya vyeti.
Hii hutumika kama njia mama ya kudhibiti mawazo ya jamii.

watu wengi wenye vyeti katika fani fulani—ndani ya elimu ya kijamii , ama kidini—wanashiriki mtazamo mmoja. Hii si ajali, bali ni sehemu ya mbinu iliyopangwa na watawala wenye maslahi.

Mifano halisi kabisa:

Udaktari: Kwanini Vyeti vya udaktari vimejengwa kulingana na mtindo fulani wa matibabu unaoendana na maslahi ya sekta ya dawa na viwanda vya afya? Hii inafanya wataalamu wa afya kuwa na mtazamo ule ule kuhusu magonjwa na tiba, huku wakichukulia "matibabu ya dawa" kuwa ndio suluhisho pekee, na kutishia maoni mbadala ya tiba asili au mbinu nyingine.

Elimu: Kwanini Waalimu wenye vyeti wanapata miongozo rasmi kutoka kwa taasisi zinazoshikilia urithi wa elimu—ambazo mara nyingi ziko chini ya udhibiti wa serikali au mashirika makubwa? Hii inawafanya kufundisha kidogo tu kile kinachohitajika, na kuepuka kufundisha mawazo yanayoweza kubadili mtindo wa kijamii au kiuchumi. Hivyo, wanafunzi wanakuwa na mtazamo sawa wa ulimwengu, ambao unapatikana tu kupitia mfumo huo rasmi wa elimu.

Dini: kwanini Viongozi wa dini, ambao mara nyingi wanapata vyeti au kupewa mamlaka na taasisi fulani, wanajikita katika mafundisho ya kidini yaliyosimamiwa na watu wachache? Huu ndio mtindo unaodhibiti imani za waumini, na kuiweka jamii katika mwelekeo wa kidini unaodhibitiwa kwa maslahi ya wachache.

UKWELI NI KUWA

Vyeti ni mbinu ya kudhibiti Jamii. Hii ni mbinu ya udhibiti wa mawazo, ambapo jamii inazalisha watu ambao wanaamini tu kile kinachohusiana na vyeti vyao na wale walioweka mifumo ya elimu ama dini.

Wasio na vyeti huonekana kama washenzi tu katika jamii, wasio na maarifa ya kina yenye tafiti.

Lengo la Uongozi wa "Systematic Uniformity" ni kuimarisha udhibiti wa jamii kupitia udhibiti wa fikra.
Vyeti vinakuwa ni kama ufunguo fulani unaokupa Nafasi ya kuingia na kukubalika kirahisi na mifumo iliyowekwa na wachache kwa ajili ya maslahi ya wachache ndani ya Jamii.

Jamii humtukuza mwenye vyeti kana kwamba ndiye mjuzi wa mambo, isitambue kama mtu huyo ni programmed machine iliyoandaliwa kuipumbaza jamii.

Mindset uniformity ni njia bora ya kudumisha utawala kwa kudhibiti jinsi watu wanavyofikiria, wanavyoshughulika na changamoto za kimaisha, na wanavyoshirikiana na dunia.

Tunaishi katika ulimwengu wa kibeberu ambapo vyeti vinaonekana kama jambo jema sana na la manufaa.
Ulimwengu wa kibeberu umejengwa kwa misingi ya udhibiti, ubaguzi, na mifumo ya nguvu zinazoshikilia watu wengi katika hali ya kutokujua. Huu ni mfumo ambao unaunda mtindo wa maisha ambapo haki na uhuru wa kifikra unadhibitiwa na wachache walio na uwezo wa kujua na kudhibiti mambo makubwa ya kijamii, kiuchumi, na kidini.

Kwa hiyo, watu wengi wanakuwa na mawazo yanayokubaliana na hali fulani iliyopangwa, na hivyo wanafanana kimawazo bila kujua kwamba wanaangukia katika mtego wa udhibiti wa kimawazo (Imperialism.)

Nikiwa nahitimisha makala yangu, niseme kuwa Vyeti ni silaha ya kimawazo inayowaweka watu katika mzunguko wa mawazo wa kisheria na kiufundi, na hivyo kudhibiti jamii kwa kiwango kikubwa. Uzalishaji wa watu waliokomaa kifikra na wenye kujitegemea katika mawazo yao unahitaji kuvunja miongozo hii, na kuhamasisha ubunifu na tafakari huru.

Katika Gnosticism, hii ndiyo maana ya kutafuta gnosis – kutafuta ukweli wa kipekee wa mtu mwenyewe, bila kuzingatia mifumo ya nje inayojaribu kudhibiti mawazo yako.

UKITAKA KUMFANYA MTU AENDELEE KUWA MFUNGWA, USIMFANYE ATAMBUE KUWA YEYE NI MFUNGWA
 
Ajira ni madawa ya kulevya ukiyaonja uachi baada ya kustaafu ndo utagundua umetumika bure
 
Dah Maisha sio magumu hivo Mzee, Watu tuna vyeti vya ubatizo, UKWATA, sijui JKT, Kuzaliwa, Elimu, Uongozi. nk.

Nothing serious on that, just appreciation for accomplishing certain task.
 
Back
Top Bottom