Hivi ujenzi wa kituo kikuu cha mabasi ya mwendo kasi Jangwani ulifanyiwa "environmental impact assesment(E.I.A)"?

Aug 23, 2016
61
144
Nimeangalia taarifa ya habari jana na kumuona Waziri wa Tamisemi akiwa ametembelea hiko kituo na kuelezwa hasara na uharibifu mkubwa uliojitokeza kutokana na kituo hiko kuzingira na maji yaliyotoka mto Msimbazi uliopo mita chache kutoka kwenye kituo hiko.

Swali ambalo nilitarajia kulisikia kwa Mh waziri na hakuliuliza ni kuwa ni Nani aliyehusika kufanya utafiti wa madhara ya kimazingira yanayoweza kujitokeza kutokana na ujenzi wa kituo hiko?.

Na kwa nn asiwajibishwe kwa hasara iliyojitokeza maana wahusika walitanabaisha kuwa zaidi ya mabasi 30 yameharibika na wanasubiri vipuri kutoka Japani.

Na ninavyofahamu ni kwamba serikali ina mkono wake kwenye hii kampuni hivyo ina chembe za umma ndani yake.
 
Waulize CCM ndio waliotoa vibali.Kikwete Kuna wakati naye alishangaa Kama wewe Sasa sielewe Nani alitia kibali na kukubaliwa.Ila wamepata hasara ya mabasi kadhaa kuharibika ,ofisi kuingia maji nk.wanabomolea watu wengine za kwao wanaziacha Mungu Ni mwema naye anaonyesha ukuu wake
 
Hamnaga EIA Bongo, wanaweza anzisha hata kiwanda posta, kariakoo au popote pale watakapoamua.
 
EIA ndio Msamiati gani...!
Mjeambiwa hakuna kufanya Siasa hadi 2020.

Hapa ni Kazi tuu.
 
Waulize CCM ndio waliotoa vibali.Kikwete Kuna wakati naye alishangaa Kama wewe Sasa sielewe Nani alitia kibali na kukubaliwa.Ila wamepata hasara ya mabasi kadhaa kuharibika ,ofisi kuingia maji nk.wanabomolea watu wengine za kwao wanaziacha Mungu Ni mwema naye anaonyesha ukuu wake
Mabasi 30 kama sijakosea
 
Ndio pale ambapo MANJI alitaka kujenga WEMBLEY ya Yanga?
 
Nimeangalia taarifa ya habari jana na kumuona Waziri wa Tamisemi akiwa ametembelea hiko kituo na kuelezwa hasara na uharibifu mkubwa uliojitokeza kutokana na kituo hiko kuzingira na maji yaliyotoka mto Msimbazi uliopo mita chache kutoka kwenye kituo hiko. Swali ambalo nilitarajia kulisikia kwa Mh waziri na hakuliuliza ni kuwa ni Nani aliyehusika kufanya utafiti wa madhara ya kimazingira yanayoweza kujitokeza kutokana na ujenzi wa kituo hiko?. Na kwa nn asiwajibishwe kwa hasara iliyojitokeza maana wahusika walitanabaisha kuwa zaidi ya mabasi 30 yameharibika na wanasubiri vipuri kutoka Japani. Na ninavyofahamu ni kwamba serikali ina mkono wake kwenye hii kampuni hivyo ina chembe za umma ndani yake.
Basi ya mchina vipuri vitoke japan kweli! !
 
Back
Top Bottom