Hivi tunajua bei ya umeme imepanda?

Hivi tunajua bei ya umeme imepanda?

kalongo kalongo

New Member
Joined
Mar 11, 2019
Posts
1
Reaction score
1
Wananchi wa Tanzania tumekuwa na changamoto za kimaisha kwa muda mrefu hasa katika kupanda kwa bei za bidhaa muhimu kwa matumizi ya kila siku. Ukiangalia bei za vifurushi katika mitandao yetu ya simu inapanda kila uchwapo, mafuta ya diesel, petrol, na nishati mubadala yaani gesi bei juu. Sasa na TANESCO wanaona wasiachwe nyuma katika kupandisha bei ya unit kinyemela . Kila Mtanzania yuko kimya kama haya mambo hayatokei nchini mwetu. Nashauri kuazishwa kwa vikundi vya utetezi mfano chama cha watumiaji wa umeme, au simu, gesi na mafuta ili pale mashirika haya yakipandisha bei, wawepo kututetea na kupinga ongezeko lolote la bei ili hali kipato cha Mtanzania kinazidi kushuka kutokana na kushuka kwa sarafu yetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nasikia uchumi unapaaa !!!!

Umeme wa 10k unapata 28.1 units sasa sijui umepandaje....
Hebu check vyema mkuu mimi nmenunua jana umeme.

Sent using Jamii Forums mobile app
Screenshot_20190325-071938.png

Na mimi nimenunua jana. Sijaona bei kupanda!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haujapanda! Nimenunua jana na nimepata units zile zile za siku zote!

Malipo yamekamilika.37*********
GEPG23EMDB***32301
Units 84.3KWH

Token 1131 1962 8007 6776 1203

Cost 24,590.17
VAT 18% 4,426.22
EWURA 1% 245.90
REA 3% 737.71
TOTAL 30,000.00 24/03/19 13:12
 
Mpuuzi Kama huyu anayeleta mada bila ushahidi apigwe Ban. Anatuchonganisha na Rais wetu Mpendwa JPM

Hamisa 3 - 0 Zarina
 
Slim5 slim5 slim5.....

Izo token umeziacha full pasipo kuzificha...

Kama mtu anaitaji kukutia mkononi ni kwepesi sana....yaani anachukua tu izo token anakwenda tanesco kuuliza ziliingizwa kwenye mita gani

Wakishapata namba ya mita basi watapata information zote kuhusu wewe

Kwenye ulingo wa security tunasema be aware be secure

Unaweza kujisahau kitu kidogo sana but kinaleta majanga...

Uwezi jua mleta mada nae kalenga nini myb nia yake sio kuhusu umeme kabisa..

But kukusanya taarifa kama ivyo

Nimemaliza....

Twende na jpm2020
 
Wakuu hata mm zaidi ya mwezi Sasa nanunua umeme napewa unit ndogo kuliko nilizokuwa nimezoea, mleta maada ana hoja au yawezekana ni kwa baadhi ya watu?
 
Mpuuzi Kama huyu anayeleta mada bila ushahidi apigwe Ban. Anatuchonganisha na Rais wetu Mpendwa JPM

Hamisa 3 - 0 Zarina

Kijana Hamisa na Zarina ndiyo nini aka ya Taifa Stars ni Hamisa acha kuwadhalilisha vijana wetu,Shida yote ni akina Makonda.
 
Slim5 slim5 slim5.....

Izo token umeziacha full pasipo kuzificha...

Kama mtu anaitaji kukutia mkononi ni kwepesi sana....yaani anachukua tu izo token anakwenda tanesco kuuliza ziliingizwa kwenye mita gani

Wakishapata namba ya mita basi watapata information zote kuhusu wewe

Kwenye ulingo wa security tunasema be aware be secure

Unaweza kujisahau kitu kidogo sana but kinaleta majanga...

Uwezi jua mleta mada nae kalenga nini myb nia yake sio kuhusu umeme kabisa..

But kukusanya taarifa kama ivyo

Nimemaliza....

Twende na jpm2020
Acha kumtisha ulijuaje kama atachangia huu Uzi,Mshindwe kuwapata waliomteka Mo unakuja na upuuzi kama huu
 
Ukiondoa VAT 18%, EWURA 1% na REA 3% pia kuna Trx Fee ambayo imepanda kwa asilimia 1.1% (ilikuwa 0.00%) mathalani umenunua umeme wa elfu mbili (Tsh. 2,000/=) hapo kwenye VAT utakatwa Tsh. 291.83, EWURA Tsh. 16.21, REA Tsh. 48.64 wakati hii mpya sijui niite "transaction fee" (Trx) Tsh. 22.0,,,,,,kwa hivyo, jumla itakuwa Tsh. 2,100/= kwa makadirio ya shilingi elfu 2,000/=,,,,mleta mada nadhani kwa wale wanaonunua umeme kwa "mawakala" makhususi nadhani hiyo "fee" inawahusu, wengineo sidhani...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani jf ni kikosi cha ugaidi mpaka muogope kujulikana
Slim5 slim5 slim5.....

Izo token umeziacha full pasipo kuzificha...

Kama mtu anaitaji kukutia mkononi ni kwepesi sana....yaani anachukua tu izo token anakwenda tanesco kuuliza ziliingizwa kwenye mita gani

Wakishapata namba ya mita basi watapata information zote kuhusu wewe

Kwenye ulingo wa security tunasema be aware be secure

Unaweza kujisahau kitu kidogo sana but kinaleta majanga...

Uwezi jua mleta mada nae kalenga nini myb nia yake sio kuhusu umeme kabisa..

But kukusanya taarifa kama ivyo

Nimemaliza....

Twende na jpm2020
 
Haujapanda! Nimenunua jana na nimepata units zile zile za siku zote!

Malipo yamekamilika.37*********
GEPG23EMDB***32301
Units 84.3KWH

Token 1131 1962 8007 6776 1203

Cost 24,590.17
VAT 18% 4,426.22
EWURA 1% 245.90
REA 3% 737.71
TOTAL 30,000.00 24/03/19 13:12
oke ushafahamika tayar bora utoe fyekelo lako mana hadi nyumba unayoishi ishajulikana na sasa utulie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiondoa VAT 18%, EWURA 1% na REA 3% pia kuna Trx Fee ambayo imepanda kwa asilimia 1.1% (ilikuwa 0.00%) mathalani umenunua umeme wa elfu mbili (Tsh. 2,000/=) hapo kwenye VAT utakatwa Tsh. 291.83, EWURA Tsh. 16.21, REA Tsh. 48.64 wakati hii mpya sijui niite "transaction fee" (Trx) Tsh. 22.0,,,,,,kwa hivyo, jumla itakuwa Tsh. 2,100/= kwa makadirio ya shilingi elfu 2,000/=,,,,mleta mada nadhani kwa wale wanaonunua umeme kwa "mawakala" makhususi nadhani hiyo "fee" inawahusu, wengineo sidhani...

Sent using Jamii Forums mobile app
Transaction fee inakatwa humo humo kwenye Tsh 2000...
 
Thamani ya Us Dolar inavyopanda Vs TSH , unategemea nini kama sio kupanda kwa bei za bidhaa.
 
Back
Top Bottom