Hivi tuna haki au uwezo wa kutaifisha mali ya nchi zingine

Mathias Raymond Nyakapala

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
2,181
1,493
Anaandika Wakili Msomi John Mallya.

...........................................................
Hivi tuna haki au uwezo wa kutaifisha mali ya nchi zingine?

Ni swali ambalo limegusa hisia na akili yangu iliyoathirika na taaluma yangu ya uanasheria baada ya kuona kipande cha video ambacho kimekuwa kikisambaa kwenye mitandao ya kijamii na kimekuwa ni sehemu ya habari katika magazeti yetu mengi hii leo kuhusiana na amri ya Mheshimiwa Rais wangu ya kutaka pasi ya kusafiria ya raia wa India, Rajendra Kumar, izuiwe, kufuatia sakata la kutoridhishwa na utekelezaji wa kandarasi huko Ng'apa, Lindi.

Imenilazimu kuchangia hili nanyi ndugu zangu. Inawezekana Kwa wengi wetu limepita tu kama jambo la kawaida tu na la kusifiwa kwani lkinasukumwa na nia njema ya kuhakikisha matatizo ya jamii yetu yanatatuliwa kwa haraka. Nia ni njema lakini utekelezaji unatia shaka. Kwangu, baada ya kile nilichoibua katika utafiti wangu wa haraka kisheria, utekelezaji unakiuka sheria na utamaduni wa kimataifa (international legal and customary norms). Unatia doa mahusiano yetu kimataifa na inawezekana tunajenga utamaduni mpya ambao utatugharimu sana.

Pasi ya kusafiria (passport) ni mali ya taifa lililoitoa kwa raia wake. Ni ushahidi kwamba, mwenye kuimiliki ni raia wa nchi husika aliyepewa kibali cha kusafiri kwenda atakako, kwa mujibu wa haki yake ya kimaumbile na kikatiba ya kwenda mahali popote atakako. Hivyo basi, pasi ya Rajendra Kumar ni mali ya serikali ya India. Kuitaifisha/kuikamata/kuzuia (confiscate/impound/seize) ni sawa na kutaifisha/kukamata/kuzuia mali ya India. Hili si suala la mzaha kimataifa. Lazima korido za kidiplomasia zitasuguliwa kama bado.

Hili ni tendo hasi kimataifa. Ni tendo ambalo kwa India, nchi inayochukuliwa kuwa ni demokrasia ya juu (great democracy), lina mipaka hata kwa serikali yenyewe ya India kuweza kunyang'anya/kuzuia/kutaifisha au vinginevyo, pasi ya raia wake. Wao walijitungia Sheria ya Pasi ya Kusafiria (Passport Act), 1967, ambayo ndiyo sheria inayoongoza huko kwao juu ya namna ya kutoa au kutaifisha/kunyang'anya pasi ya raia wa India ili kulinda haki yake ya kwenda atakako chini ya Ibara ya 21 ya Katiba yao. Kwa mujibu wa maamuzi ya mahakama za India (yenye ushawishi mkubwa katika mahakama zetu), ni ;polisi wa India na mamlaka za utoaji pasi za India na mahakama pekee ndio wenye uwezo wa aidha kuzuia kwa muda (seize) pasi au kuinyang'anya (impound) chini ya Kifungu cha 102 cha Sheria ya India Mwenendo wa Makosa ya Jinai, 1973 na Kifungu cha 10(3) cha Sheria ya Pasi, 1967, kwa mujibu wa Mahakama ya Juu (Supreme Court) ya India katika kesi ya Suresh Nanda Vs.C.B.I. (2008)3SCC674. Hivyo, kitendo chochote hasi dhidi ya pasi ya raia wa India lazima kifuate utaratibu uliowekwa kisheria huko kwao.

Suala hili lina mahusiano ya karibu sana na sakata la wafanyakazi wa Quality Group ambalo halijapokelewa vyema huko India kwa namna lilivyoshughulikiwa. Hili liko mahakamani bado. Tuishie hapo.

Hivyo, hata kama tuna nia njema kiasi gani, lazima tuheshimu sheria za kimataifa na sheria zetu za ndani. Inawezekana watanzania hatutendewi haki huko
India lakini, kwangu mimi Mkatoliki katika kipindi hiki cha kwaresma, nakumbushwa kuwa na upendo na matendo mema kwa wengine, nisiwatendee wengine kile ambacho sipendi kutendewa. Naamini pia kwamba, hii ni Torati, ambayo ni msingi wa imani zote kuu hapa kwetu. Kipimo tunachowapimia wengine ndicho kitakachotumika dhidi yetu.

Tuna Sheria ya Pasi hapa kwetu pia ambayo imetungwa ili kulinda haki ya Kikatiba ya Mtanzania kwenda atakako kama ilivyo India, nchi ambayo utamaduni wake wa kisheria hauko tofauti na wetu.

Masuala ya kimkataba yashughulikiwe kwa mujibu wa makubaliano ya kimkataba.

Natimiza wajibu wangu wa kikatiba na kisheria kushauri bila inda yoyote. Sitafurahi kuona kiongozi wangu yoyote anashindwa kutimiza malengo mema kwa nchi yetu lakini pia ninaumia ninapoona makosa ya wazi yakishabikiwa.

Tunaanza kupoteza marafiki zetu wa toka enzi na enzi. Kama wanatukosea tukae nao na kuelezana kwa misingi inayokubalika. Kwa mtindo huu siku si nyingi tutakuwa kichekesho cha kimataifa.
 
Kwani kaandika kipi hapo cha kijinga zaidi ya wewe kuwa na uchungu wako wa hedhi ndio unaleta humu..!
Kwani unafikiri waliomnyanganya pasi huyo kabachori hawajui yote hayo! Ujuaji tu unawasumbua!
 
Badala ya kuandika kwenye mitandao ya kijamii, nendeni mkafungue shauri mahakamani na mumtetee ili apewe pasi yake.

Hii nchi ina watu wa ajabu kweli!

Kwenye suala hili, the end justifies the means.
 
Back
Top Bottom