Hivi tumeshindwa kumbaini aliyepandikiza magugu ziwa Viktoria ayaondoe Kwa gharama zake?

Rabbon

JF-Expert Member
Apr 16, 2022
16,710
25,285
Salaam, Shalom!!

Nilipokuwa katika ziara ya Utalii wa ndani, nimekumbana na kero hii ya magugu maji ziwa NYANZA. Ziwa NYANZA lilikua ziwa la kuvutia sana.

Wataalam wasema, haya magugu ziwa NYANZA hayakuwepo miaka ya nyuma, ni mradi umetokea miaka ya hivi karibuni,

Serikali na wanavijiji kuzunguka ziwa NYANZA wamekuwa wakihangaika kutokomeza magugu hayo.

Magugu hayo yamechangia kupunguza kuzaliana Kwa Samaki ziwa NYANZA Kwa kadri siku zinavyoenda. Historia ya Kutokea magugu hayo ziwa NYANZA inasemaje na hatua zipi zinachukuliwa kukabiiana na uharibifu huo wa kutengeneza?

Swali: Ni nani waliyehusika kupandikiza magugu ziwa NYANZA?

Na wakibainika, ni Bora washtakiwe, walipe fidia, na wayaondoe Kwa gharama zao, ni akina nani hao?

Karibuni 🙏
 
Salaam, Shalom!!

Nilipokuwa katika ziara ya Utalii wa ndani, nimekumbana na kero hii ya magugu maji ziwa Viktoria.

Wataalam wasema, haya magugu ziwa Viktoria hayakuwepo miaka ya nyuma, ni mradi umetokea miaka ya hivi karibuni,

Serikali na wanavijiji kuzunguka ziwa Viktoria wamekuwa wakihangaika kutokomezwa magugu hayo.

Magugu hayo yamechangia kupunguza kuzaliana Kwa Samaki ziwa Viktoria Kwa kadri siku zinavyoenda. Historia ya Kutokea magugu hayo ziwa Viktoria inasemaje na hatua zipi zinachukuliwa kukabiiana na uharibifu huo wa kutengeneza?

Swali: Ni nani aliyehusika kupandikiza magugu ziwa Victoria?

Na akibainika au wakibainika, ni Bora ayaondoe Kwa gharama zake/ zao, ni nani huyo au ni akina nani hao?

Karibuni 🙏
Ccm hao kama walivyoleta kunguru wa Zanzibar kulinda muungano
 
Hapo CCM nadhani wanasingiziwa!!
Wanasingiziwa vipi? Baada ya TANU nani mwingine alikabidhiwa utajiri wa nchi hii aulinde zaidi ya ccm
Wanasingiziwa vipi? Baada ya TANU nani mwingine alikabidhiwa utajiri wa nchi hii aulinde zaidi ya ccm?
Ccm saa hizi wako bizy na kuteletea wachina .Nyoka na mbwa pamoja na mijusi vinamalizika kwa kasi sana
 
Yaezakuwa adui alitoka nje na kujiingiza kupitia Utalii, na kama tujuavyo, ziwa Viktoria lipo Nchi tatu,

Yaezakuwa yameingia tokea Nchi Jirani.
Siyo kweli,ccm walikuwa na dhamana a kulinda mipaka yetu kama walikuwa awawezi wangekaa pembeni.Mtu mnyonge hukimbilia dini siyo ufalme.Utawezaje,utawezaje kuwalinda watu wakati wewe mnyonge?
 
Yaezakuwa adui alitoka nje na kujiingiza kupitia Utalii, na kama tujuavyo, ziwa Viktoria lipo Nchi tatu,

Yaezakuwa yameingia tokea Nchi Jirani.
Siyo kweli,ccm walikuwa na dhamana a kulinda mipaka yetu kama walikuwa awawezi wangekaa pembeni.Mtu mnyonge hukimbilia dini s
Siyo kweli,ccm walikuwa na dhamana a kulinda mipaka yetu kama walikuwa awawezi wangekaa pembeni.Mtu mnyonge hukimbilia dini siyo ufalme.Utawezaje,utawezaje kuwalinda watu wakati wewe mnyonge?
Ccm tayari umewauzia upinde wa mvua wale jamaa.
 
Magugu maji yaliwahi kuwepo ziwa Victoria miaka ya 90 yakiathiri bandari zote za mwambao wa ziwa, kuanzia Mwanza, Bukoba na Kisumu. Juhudi za pamoja ndio zilizowezesha kudhibitiwa kwa magugu hayo kwa miaka yote hiyo, hadi sasa yanapojitokeza tena.
Magugu maji ustawi wake ziwani unaashiria kuwepo kwa vinyesi vya binadamu na wanyama ambacho ndio chakula na virutubisho vya magugu maji.
Kudhibiti ukuaji wa magugu maji ndani ya ziwa Victoria, Tanganyika na hata bahari ya hindi, kunahitaji Serikali kuwekeza kwenye vyombo vya kusafisha mifereji, mito na maziwa lakini pia kuhakikisha kuwa wanamazingira wanafanya kazi zao walizozisomea kwa weredi mkubwa.
 
Asili ya magugu maji ni nini?
 
Back
Top Bottom