Mwanzoni mwa mwaka huu wa 2016 serikali kupitia waziri wa habari,Sanaa,utamaduni na michezo tuliambiwa kwamba serikali haitaendelea na kuonyesha bunge live kwa kuwa ni gharama.Baada ya hoja hiyo wamiliki wa vyombo binafsi vya habari walijitojeza wakasema kwamba wao watarusha matangazo live pamoja na baraza la habari wakasema wao watagharamia matangazo hayo ili wananchi wapate haki yao ya kupata habari na kujua wawakilishi wao bungeni wanasema nini.Kutoka kwenye bunge ni gharama magoli yakahamishwa na wakaja na hoja nyingine baada ya kwanza kuonekana na muflisi hoja yenyewe ni kwamba watanzania wanatumia muda mwingi kuangalia bunge kuliko kufanya shughuli za uzalishaji Mali na kujenga uchumi wa taifa hoja hii ilitolewa na pm akiwa uingereza mkanganyiko tayari na ukinzani wa hoja ndani ya serikali moja.Hivyo basi binge halikuoneshwa live badala yake tukawa tunapata recoded ambayo imeeditiwa tu.Kwa mantiki hiyo tulitarajia kwa kila kitu kinachoendelea bungeni kirekodiwe na baadae kurushwa kama ilivyo desturi.Maswali yangu ni haya. Je bunge livelinaangalia utashi wa serikali. Mbili kwann serikali isiendelee na msimamo huo kwa matukio yote yanayoendelea bungeni. Tatu kwanini serial I ilikiuka kauli yake na kuamua kurusha bunge live siku ya bajeti ya serikali kwann tusiendelee na utaratibu wetu ule ule wa giza. Nne je siku tuliponeshwa bunge live haikuwa cku ya kazi kwann tuliamua kuwaondoa watanzania kwenye uzalishali Mali na kuamua kurusha bunge live. Tano ni hasara kiasi gani ilipatikana kwa kurusha bunge live siku ile