Hivi TCRA mko wapi juu ya haya?

KIBURUDISHO

JF-Expert Member
Joined
Mar 28, 2011
Posts
1,002
Reaction score
278
WanaJF wenzangu habari za jioni natumai mu wazima wa afya njema.Niko hapa kuwajuza juu ya hii kero inayonikera sana mimi na hata watumiaji wengine kama mimi.

Kero yenyewe ni hii ya kupokea matangazo ya televisheni kwa njia ya satelite na hii ni kwa chaneli za hapa nchini ambazo ni ITV, EATV, CAPITAL, TBC1, CH10 na STAR TV ambazo zote ziko ktk band C-BAND. Yaani jamani imekuwa kero saana leo ziko sawa kesho asubuhi zinagoma keshokutwa ziko sawa hadi najiuliza kwa uelewa wangu mdogo kuwa wamiliki hao wa vituo hivyo vya kurushia matangazo huwa wanachajiwa gharama ya juu tena kwa masaa katika satelite wanayotumia kurushia matangazo.

Sasa swali langu najiuliza kama satelite wanayotumia haina nguvu kwa nini wasiiame wakaamia satelite yenye nguvu.Au ndio ile desturi yetu watanzania ya kuchakachua na kununua vitu chakavu kila siku matengenezo Mko wapi TCRA na baraza la ushindani.
 
Hawa TCRA si nasikia wana kitengo cha Mlaji sasa naona watapitia na wataifanyia kazi
 
TCRA jina tu hakuna lolote la maana wanalofanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…