Hivi sukari ya Mtibwa inauzwa wapi?

Truth Matters

JF-Expert Member
Apr 12, 2013
1,612
2,603
Najua kuna kiwanda cha sukari cha Mtibwa, Morogoro. Lakini sijawahi kuiona popote sukari inayotengenezwa na kiwanda hicho.

Je kuna mtu amewahi kuiona sukari ya kiwanda hiki?
 
Juzijuzi kwenye taarifa ya habari walionyesha eti mashamba yao yamevamiwa na ng'ombe lakini ukiangalia kwa umakini nadhani changa LA macho,
 
1. nauzwa kwa nembo ya Ilovo.
2. Naomba kuuliza, je sukari ya TPC - Moshi inauzwa wapi? Nimefika miji kadhaa mikubwa sijawahi hata kuona kifungashio chake. Ili hali pale kiwandani kuna malri yanapanga foleni.
 
Karibu asiimia 80 ya sukari inayopatikana ktk maduka mengi ukanda wa kaskazini ni TPC suger, then MANYARA suger halafu aina kampuni nyingine zinafuata
 
1. nauzwa kwa nembo ya Ilovo.
2. Naomba kuuliza, je sukari ya TPC - Moshi inauzwa wapi? Nimefika miji kadhaa mikubwa sijawahi hata kuona kifungashio chake. Ili hali pale kiwandani kuna malri yanapanga foleni.
Hiyo ya Illovo ni ya Kilombero. Kanda ya kaskazini tunatumia ya TPC. Ya Mtibwa sijawahi kuiona sokoni, labda wanauza nje.
 
Mwenye picha hata ya sukari inayosafirishwa nje kutoka kiwanda cha Mtibwa atuwekee
 
1. nauzwa kwa nembo ya Ilovo.
2. Naomba kuuliza, je sukari ya TPC - Moshi inauzwa wapi? Nimefika miji kadhaa mikubwa sijawahi hata kuona kifungashio chake. Ili hali pale kiwandani kuna malri yanapanga foleni.
Ilovo ni sukari ya Kilombero... By the way, sukari zote (isipokuwa za viwandani) zinafanana so sio rahisi kujua mtengenezaji wa sukari hiyo husika ni nani...
 
Najua kuna kiwanda cha sukari cha Mtibwa, Morogoro. Lakini sijawahi kuiona popote sukari inayotengenezwa na kiwanda hicho.

Je kuna mtu amewahi kuiona sukari ya kiwanda hiki?
Ukiona sukarj imeandikwa ILOVO ujue ya mtibwa. Halafu sukari huwa zinauzwa kwa mikoa maalum mfano huwezi ona sukari ya Kagera inauzwa Arusha
 
Sukari iliyoandikwa ILLOVO inazalishwa na kiwanda cha Kilombero.. Kilombero ina viwanda viwili, kimoja kiko upande wa Kilombero (K1) na kingine kipo upande wa Ruaha (Wilaya ya Kilosa, K2)
 
Basi labda wanatengeneza kwa ajili ya viwanda
 
Back
Top Bottom