Synthesizer
Platinum Member
- Feb 15, 2010
- 11,208
- 19,001
Tanzania haiishi vioja. Kimojawapo ya kioja kinachoendelea, ambacho huenda kikatuingiza kwenye Guiness Book of World Records of Ridiculousness, ni hili linalofanyika kwenye airport za Tanzania kwa sasa, ambapo abiria wanaosafari safari za ndani ya Tanzania, wanapowasili wanapokwenda, wanatakiwa wakaguliwe mizigo waliyotoka nayo mwanzo wa safari yao ndani ya Tanzania!
Yaani mtu anasafiri kwa ndege kutoka Mwanza kwenda Dar, au Dar kwenda Arusha, Dar kwenda Mwanza, na akifika mwisho wa safari yake, anaambiwa mizigo yake lazima ikaguliwe! Na hata anaulizwa umebeba nini ndani ya begi. Kumbuka kwamba hili si kwa ajili ya usalama wa ndege, maana mtu unakuwa umewasili na kushuka toka ndani ya ndege ndio unakaguliwa mizigo!
Ukiwauliza wafanyakazi wa airport kwa nini wanakagua mizigo ya domestic flight arrivals, na ni nini wanachotafuta, wanakuambia "wanatekeleza maagizo toka juu".
Sasa ninachojiuliza ni kama haya maagizo toka juu ni kutoka kwa Raisi Magufuli katika busara zake za kuiongoza Tanzania. Je, ni katika mkakatati wa kuzuia usafirishaji wa madawa au madini? Ni kama ndivyo, je haijaingia akilini kwamba hizi ni domestic flights ambazo kama nina mali ya magendo na nikijua kuna ukaguzi airport nitatumia mabasi au usafiri mwingine? Kama wanadhani kuna umuhimu wa kukagua mizigo ya domestic flights, tufikirie kwamba kuna siku katika stand za mabasi ya mikoani tutaanza kukaguliwa mizigo tunapowasili kutoka Mbeya, Mwanza, Tabora nk?
Kwa kweli vitu vingine havihitaji uwe na elimu ya PhD kuona kwamba ni vitu vya kijima, vya kukurupuka, havina lojiki, vinaleta usumbufu usio na maana na vinaamuliwa bila kuwa na uwezo makini wa kufikiria mambo.

Nakumbuka aliporudi mara ya pili JKNIA kumtafuta yule mkaguzi mwanamke aliuliza kwa nini internal arrivals hawakaguliwi. Na akaagiza hapohapo ukaguzi uanze mara moja.