Hivi sote tunasomeshwa namba ile ile?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
20,411
38,703
Kwenye sayansi ya Hisabari tarakimu ndizo hufanya namba. Tarakimu inaweza kuwa tarakimu bila ya kuwa namba. Kwa mfano kwenye mambo ya uchumi wanaposema mfumko wa bei uko juu kwa tarakimu moja (single digit) hiyo tarakimu moja inaweza kuwa ni 1,4,8,2 au 5 na wakisema ni tarakimu mbili (Double digit) inaweza kuwa namba yoyote ile kuanzia 10 mpaka 99.

Ule wimbo wetu adhimu wenye kibwagizo cha "wataisoma namba" ndiyo umenifikirisha hiyo sayansi ya hisabati. Hivi waliposema kuwa tutaisoma namba walimaanisha hiyo namba itakuwa moja au kila mtu atasomeshwa namba yake kivyake vyake?

Waliobomolewa Nyumba zao kule "mabondeni" namba yao ni sawa sawa na wale wanaotakiwa kabla ya kusafiri kwenda nchi za nje wapate kibali toka Ikulu? Yule Maswi anayehamishwa hamishwa kila uchao kwa "kazi maalum" yuko namba moja na yule mkurugenzi wa Muhimbili aliyerudishwa wizarani ili "apangiwe kazi nyingine"?

Namba ya yule Mwalimu aliyesimamishwa kazi kwa kuwaambia watoto waje na mifagio ya chelewa, inafanana na ya waalimu Wakuu waliopewa shilingi milioni mbili na ushee kuendeshea shule zenye watoto zaidi ya 500? Wale wafanyakazi wa ile wizara waliofungiwa nje kwa "kuchelewa" kufika kazini wamewekwa kwenye namba moja na wafanyakazi wenzao wa Kilimanjaro walioambiwa kwamba hakuna ruhusa ya likizo?

Nataka kujua namba zetu tunazosomeshwa zinafanana?
 
Baada ya uchaguzi je namba ya CDM imewa-consider NLD kwenye viti maalum!
 
Kwa jinsi hali ilivyo kila mmoja anasomeshwa namba yake aisee....ndo maana vilio havifanani tune.
 
Tune lazima itofautiane
1... yaweza kuwa kubwa kuliko .....9
9.....yaweza kuwa kubwa kuliko.....1
Inategemea na mpiga drum anawaza nini
 
Back
Top Bottom