Hivi soka la Bongo litafika!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi soka la Bongo litafika!!

Discussion in 'Sports' started by Bob K, Jun 20, 2009.

 1. B

  Bob K Member

  #1
  Jun 20, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  jamani hakuna kitu kinachoniuma roho kama watanzania tunavyokuwa wepesi kuchangia sherehe za harusi na kampeni za siasa ambazo zingeweza kufanyika katika mazingira ya kawaida! hebu fikiria hizi neema za soka zilizopo sasa kama Mh,rais kikwete akiondoka madarakani zitakuwepo? kwanini sisi tunaojiita wadau wa soka kassim dewji,Fransis kifukwe,abbas tarimba dr leaky na wengineo wengi hatutaki kusoma alama za nyakati,kama mkapa alituachia uwanja mkubwa vile kwanini tusitumie wakati huu kutengeneza nguvu ya umoja ya kweli tupate walau shule nne za kweli za soka kwa kanda kaskazini,kusini nyanda za juu,kati na kanda ya ziwa.

  sisi ni kujenga kuendesha tutabinafsisha hata kwa klabu kuwa kama za uholanzi sidhani kama hili litashikana.

  hebu jiulize ikiwa theo wallcolt wa Arsenal katika umri huu mdogo anacheza kiwango kile je unategemea leo hii wale wachezaji wetu walio katika ile timu ya serengeti boys wanaweza kuja cheza soka ya kulipwa kwani wengi katika umri wao wa miaka 14-17 mwenzao wallcolt alikuwa katika kiwango gani je huyo keran gibbs ambaye anamkaba mpaka ronaldo! ana miaka 19 tu vile jamani soka hapa kwetu tunaifanya siasa zaidi.

  nimejaribu kuwashawishi juu ya wa hili watu wanaoheshimika katika soka la hapa bongo lakini nawaona wanakuwa na moyo wa kukata tamaa ama wanaogopa kila kitu Tff mhh!! mi naoana kama pale bado watu wa ftina wapo michezo inayopedwa ni kutengeneza tikikiti za ziada na ndio maana kila kukicha kelele za mapato haziishi,hapo bado kila kitu sasa hivi wanafadhiliwa hawa nao wanatia mashaka katika suala la maendeleo ya soka sioni umakini wao haddithi nyingi kuliko vitendo na ndio maana safari hii katika uchaguzi uliopita walitaka kufagiliwa wote kwa mapinduzi ya kisayansi, kasoro tenga.

  angalia leo hii nilitegemea mtu kama bakhersa anayezungumzia soka ya kulipwa na uwakala wake wa fifa kaingia kwenye game hii kwanza nilitegemea kuona anaanza na ujenzi wa shule ya soka kwani Robinyo nimemwona katika futibol mundia siku nyingi akiwa bado mtoto analelewa hapo kwa maana ya malazi,chakula sasa huwezi leo hii kuniambia azam anashule ya soka kila mtoto atoke kwao halafu aje uwanjani kwako hutegemee katika haya mazingira ya kitanzania atakuja kuwa kama wallcolt ni nadra kama una watoto mia kwa stahili hii utaambulia mmoja.

  kama kweli tuna nia ya kulikuza soka letu ni lazima tuanze toka darasa la kwanza mpaka lasaba kwani wataalamu wanasema kuwa mtoto anatakiwa kukaa katika shule ya soka kuanzia miaka 8 mpaka 15.

  mi naona njia ni kutengeneza panel ya wadau wa soka wazito tena kwa bahati sasa tunao mpaka wabunge mweka hazina waziri mkuu michango kwa kwenda mbele sisi umma wa soka tukielekeza nguvu zetu huku wafadhili watatufuata kwani sisi ndio watumiaji wa bidhaa zao haya ni lazima tuyafanye kabla Mh Jakaya mrisho kikwete hajaondoka upepo huu ni wetu kwa sasa tuzinduke!! sijui wenzangu mnaonaje lakini mimi kwa stahili hii tunayo kwenda nayo nina mashaka kwamba siku moja tutarejea katika foootball fitina naomba mchango wenu katika hili
   
Loading...