Ukiondoa mkoa wa kigoma, mikoa ya kusini ndiyo mikoa iliyo baki nyuma kimaendeleo kwa muda mrefu, miaka ya huko nyuma ilikuwa mfanyakazi ukihamishiwa kusini , njia sahihi ya kujinusuru na adha za huko ilikuwa ni kuachana na hiyo kazi.
Barabara nzuri tumepata kwenye miaka ya tisini. Mungu akatuonea huruma kwa umaskini wetu akatuletea gesi, ambayo nayo iligeuka kuwa kama laana badala ya neema, kwani iliamsha mzozo mkubwa wa kuigombania, badala ya kujenga vinu vikubwa na kuwekeza pale Mtwara na kufungua fursa za ajira kwa wanchi.
Badala yake mitaro ikachimbwa na ikafirishwa kwenda Dar.
Hilo nalo likapita, tukasema potelea mbali, kaniki ni rangi yake hata uifue vipi itabaki kuwa nyeusi.
Tukahamia kwenye zao letu pendwa la KOROSHO , napo bei ikavurugwa , tukabaki kushuhudia mapambano kati ya wafanya biashara na serikali. Na hii imepelekea tumepata hasara kubwa sana, sasa hatujui tufanye nini, kwani kila linalo onekana kama mbaraka kwetu watu wa kusini serikali ya CCM inaligeuza kuwa laana kwetu, hivi na sisi tukiamua kusema kuwa CCM ni laana kwa mikoa ya kusini tutakuwa tumekosea kweli ?.
Sisi tunasema sawa, ila 2020 ndo CCM mtaifahamu vizuri uhalisia wa sura na tabia yetu, enough is enough.
Tuta wachezesha SINDIMBA mpaka basi.( Pungo kwa nchele, pungo kwa nchele, haishindi dona. )Eee Mwenyezi Mungu tunakuomba utupatie tena neema nyingine.