Hivi sisi watu wa mikoa ya Kusini tuliwakosea nini nchi hii?

Kusini ndipo ilipo Hazina kubwa ya taifa na lazima ilindwe. Kuweka miundombinu ni kuhatarisha Hazina hizo adim ambazo wakusini wengi hawazijui. Kuna Mafuta, gesi, dhahabu, almasi, sapphire, ruby, uranium, Helium na madude mengi. So lazima tuzilinde kwa kuacha sehem kubwa sana kuwa pori na miundombinu mibovu hadi watu wapate akili.
 
Acha kulialia, huko si nche nkapa kawajengea daraja na barabara ya lami, mbona katavi hawajapata barabara ya lami kuunganisha na tabora, kila mtu akileta malalamiko ya huko alipo patakuwa hapatoshi hapa
 
Hakuna kulia lia hapa sote hali mbaya,kama ni mazao huko kaskazini pamba imepotea,kahawa haipo,mkonge kwisha kiufupi kilimo cha biashara kimeuawa!! Kwenu gesi huku kaskazini dhahabu geita,shinyanga yooote inapopatikana umeona imepaendeleza? Tanzanite mererani kapaangalie pameendelea? Rasilimali zooote nchini tumeshindwa kuzitumia maana hatuna mipango makini na wabunge wetu wamekuwa bure kabisa,ukiwaita dhaifu wanakutishia lkn embu waulize imekuwaje kwa rasilimali zooote za taifa?? Shame!!
Kupatwa kwa Jamhuri
tuandamane tukamtafute mchawi wetu
 
Ukiondoa mkoa wa kigoma, mikoa ya kusini ndiyo mikoa iliyo baki nyuma kimaendeleo kwa muda mrefu, miaka ya huko nyuma ilikuwa mfanyakazi ukihamishiwa kusini , njia sahihi ya kujinusuru na adha za huko ilikuwa ni kuachana na hiyo kazi.

Barabara nzuri tumepata kwenye miaka ya tisini. Mungu akatuonea huruma kwa umaskini wetu akatuletea gesi, ambayo nayo iligeuka kuwa kama laana badala ya neema, kwani iliamsha mzozo mkubwa wa kuigombania, badala ya kujenga vinu vikubwa na kuwekeza pale Mtwara na kufungua fursa za ajira kwa wanchi.

Badala yake mitaro ikachimbwa na ikafirishwa kwenda Dar.

Hilo nalo likapita, tukasema potelea mbali, kaniki ni rangi yake hata uifue vipi itabaki kuwa nyeusi.

Tukahamia kwenye zao letu pendwa la KOROSHO , napo bei ikavurugwa , tukabaki kushuhudia mapambano kati ya wafanya biashara na serikali. Na hii imepelekea tumepata hasara kubwa sana, sasa hatujui tufanye nini, kwani kila linalo onekana kama mbaraka kwetu watu wa kusini serikali ya CCM inaligeuza kuwa laana kwetu, hivi na sisi tukiamua kusema kuwa CCM ni laana kwa mikoa ya kusini tutakuwa tumekosea kweli ?.

Sisi tunasema sawa, ila 2020 ndo CCM mtaifahamu vizuri uhalisia wa sura na tabia yetu, enough is enough.

Tuta wachezesha SINDIMBA mpaka basi.( Pungo kwa nchele, pungo kwa nchele, haishindi dona. )Eee Mwenyezi Mungu tunakuomba utupatie tena neema nyingine.
Mkitaka muendelee;
1. Acheni ushirikina
2. Someni muuondoe ujinga
3. Anzeni kuwachagua viongozi thabiti wa kuwawakilisha na sio kuchagua chama.

Leo mkoa wa Mara alitotoka Nyerere CCM inamajimbo nadhani mawili, mengine yote ni upinzani hawakubali kumchagua mtu wa ndioo bila kuchanganya na zake.

Wamebadilika na leo wanamtaka mtu mwenyekujenga hoja sio mtu mwenye kuwahonga supu za ng'ombe vichakani.
 
Kwahiyo kuchagua upinzani ndio maendeleo !?.......kweli zakuambiwa changanya na zako !
Mkitaka muendelee;
1. Acheni ushirikina
2. Someni muuondoe ujinga
3. Anzeni kuwachagua viongozi thabiti wa kuwawakilisha na sio kuchagua chama.

Leo mkoa wa Mara alitotoka Nyerere CCM inamajimbo nadhani mawili, mengine yote ni upinzani hawakubali kumchagua mtu wa ndioo bila kuchanganya na zake.

Wamebadilika na leo wanamtaka mtu mwenyekujenga hoja sio mtu mwenye kuwahonga supu za ng'ombe vichakani.
 
Umeongea pointi tupu ila wakusini wenyewe sio waelewa mark my words wana kaujinga wa ccm ndo mama yao. Subiri 2020 utaona

Back
Top Bottom