Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,049
Imekuwa ni jambo la kawaida sana tokea enzi za utawala wa awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere, na awamu zilizofuatia za Mzee Mwinyi, Benjamin Mkapa na hatimaye Jakaya Kikwete, kuitumia siku ya mwisho wa mwaka kutoa hotuba kupitia vyombo vya habari kuelezea mafanikio ya utawala wa wakati huo.
Sasa kwa kuwa tumeingia utawala wa awamu ya 5 ambao ni utawala uliojipambanua kuwa ni utawala wa HAPA KAZI TU, utawala wenye kupambana na ufisadi,utawala wenye kubana matumizi, utawala wenye kuhakikisha kuwa unakusanya kodi to the maximum point na ni utawala ambao kama kiongozi wetu Mkuu Rais Magufuli alivyowahi kusema kuwa unataka watu waliokuwa wakiishi kama Malaika waishi kama mashetani.............
Sasa watanzania wote kwa ujumla wetu, tunayo kiu kubwa ya kumsikia Kiongozi wetu Mkuu, Rais Magufuli akilihutubia Taifa hapo kesho kwa kutumia vyombo mbalimbali vya habari vya kitaifa, akitufafanulia namna sera zake za awamu ya 5 zilivyopata mafanikio makubwa katika mwaka wake wa kwanza tu wa uongozi wake na namna wananchi kwa ujumla wetu tulivyoingia kwenye maisha ya neema kubwa na kufaidika na rasilimali za nchi yetu zilizokua zikitafunwa na kikundi kidogo cha watu ambao wanapaswa kuburuzwa kwenye mahakama maalum za mafisadi.
Kwa hiyo sisi wananchi tunaisubiri kwa hamu kubwa hotuba hiyo ya kiongozi wetu Mkuu Rais Magufuli kwa Taifa hili hapo kesho ambayo ninaamini atakapoitoa itaweza kusuuza roho zetu na kukata kiu za wananchi wanyonge wa nchi hii na kukata 'ngebe' za wapinzani!
Mungu ibariki Tanzania