Hivi Rais Magufuli atahutubia Taifa kesho wakati tunaufunga mwaka?

Kama ni Redio ni hela ndogo sana. Kwa saa moja ama mbili hivi, haitatosha kununua Anti sumu ya nyoka kwa ma hospitali yote nchini. Tuacheni siasa.
Akiamua kutuhubia itakuwa bado si gharama!
Hoja yangu nzima ni kua ahadi na maneno ya mwisho wa mwezi/ mwaka hayatainua maisha yetu.
 
Imekuwa ni jambo la kawaida sana tokea enzi za utawala wa awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere, na awamu zilizofuatia za Mzee Mwinyi, Benjamin Mkapa na hatimaye Jakaya Kikwete, kuitumia siku ya mwisho wa mwaka kutoa hotuba kupitia vyombo vya habari kuelezea mafanikio ya utawala wa wakati huo.

Sasa kwa kuwa tumeingia utawala wa awamu ya 5 ambao ni utawala uliojipambanua kuwa ni utawala wa HAPA KAZI TU, utawala wenye kupambana na ufisadi,utawala wenye kubana matumizi, utawala wenye kuhakikisha kuwa unakusanya kodi to the maximum point na ni utawala ambao kama kiongozi wetu Mkuu Rais Magufuli alivyowahi kusema kuwa unataka watu waliokuwa wakiishi kama Malaika waishi kama mashetani.............

Sasa watanzania wote kwa ujumla wetu, tunayo kiu kubwa ya kumsikia Kiongozi wetu Mkuu, Rais Magufuli akilihutubia Taifa hapo kesho kwa kutumia vyombo mbalimbali vya habari vya kitaifa, akitufafanulia namna sera zake za awamu ya 5 zilivyopata mafanikio makubwa katika mwaka wake wa kwanza tu wa uongozi wake na namna wananchi kwa ujumla wetu tulivyoingia kwenye maisha ya neema kubwa na kufaidika na rasilimali za nchi yetu zilizokua zikitafunwa na kikundi kidogo cha watu ambao wanapaswa kuburuzwa kwenye mahakama maalum za mafisadi.

Kwa hiyo sisi wananchi tunaisubiri kwa hamu kubwa hotuba hiyo ya kiongozi wetu Mkuu Rais Magufuli kwa Taifa hili hapo kesho ambayo ninaamini atakapoitoa itaweza kusuuza roho zetu na kukata kiu za wananchi wanyonge wa nchi hii na kukata 'ngebe' za wapinzani!

Mungu ibariki Tanzania
unahitaji kusikia nini toka kwake ambacho kitakuwa kipya, labda.
 
Lakini Mkuu, watanzania tuliomweka madarakani ndiyo tuna hamu ya kumsikia Kiongozi wetu Mkuu akilihutubia Taifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari.

Sasa kwa nini wewe umkingie kifua na kusema siyo lazima alihutubie Taifa?
kawekwa na Lubuva sio wewe/nyie
 
Imekuwa ni jambo la kawaida sana tokea enzi za utawala wa awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere, na awamu zilizofuatia za Mzee Mwinyi, Benjamin Mkapa na hatimaye Jakaya Kikwete, kuitumia siku ya mwisho wa mwaka kutoa hotuba kupitia vyombo vya habari kuelezea mafanikio ya utawala wa wakati huo.

Sasa kwa kuwa tumeingia utawala wa awamu ya 5 ambao ni utawala uliojipambanua kuwa ni utawala wa HAPA KAZI TU, utawala wenye kupambana na ufisadi,utawala wenye kubana matumizi, utawala wenye kuhakikisha kuwa unakusanya kodi to the maximum point na ni utawala ambao kama kiongozi wetu Mkuu Rais Magufuli alivyowahi kusema kuwa unataka watu waliokuwa wakiishi kama Malaika waishi kama mashetani.............

Sasa watanzania wote kwa ujumla wetu, tunayo kiu kubwa ya kumsikia Kiongozi wetu Mkuu, Rais Magufuli akilihutubia Taifa hapo kesho kwa kutumia vyombo mbalimbali vya habari vya kitaifa, akitufafanulia namna sera zake za awamu ya 5 zilivyopata mafanikio makubwa katika mwaka wake wa kwanza tu wa uongozi wake na namna wananchi kwa ujumla wetu tulivyoingia kwenye maisha ya neema kubwa na kufaidika na rasilimali za nchi yetu zilizokua zikitafunwa na kikundi kidogo cha watu ambao wanapaswa kuburuzwa kwenye mahakama maalum za mafisadi.

Kwa hiyo sisi wananchi tunaisubiri kwa hamu kubwa hotuba hiyo ya kiongozi wetu Mkuu Rais Magufuli kwa Taifa hili hapo kesho ambayo ninaamini atakapoitoa itaweza kusuuza roho zetu na kukata kiu za wananchi wanyonge wa nchi hii na kukata 'ngebe' za wapinzani!

Mungu ibariki Tanzania
Amefanikiwa kutufanya tuishi kama shetani, kesho asituharibie siku yetu, aendelee na mapumziko yake
 
Maelezo ya uzi wako nimesoma aya ya kwanza tu, nakujibu kutokana na heading yako.

Asihutubie hizo hela za kurusha kipindi akanunulie antidote za nyoka ndugu zetu wa vijijini wasitozwe laki saba na nusu kwa antidote.

Au itoke taarifa ya kutuambia kua mazingira yaliyojengwa yamevutia wawekezaji na 2017 wanakuja kuanzisha viwanda, na ajira zitakuepo kufikia January 2017.

Na mahakama ya mafisadi imepata kesi.
Kwani hata television ya taifa Rais anatakiwa alipie airtime ?
 
Kwa hiyo ruzuku wanayoitoa serikali inawafaidisha nn serikali ? Basi haina haja ya serikali kutoa riziki

Hiyo ruzuku inatosha?

Chombo cha habari mapato yake hutokea kwenye matangazo ambayo nayo watu huyapeleka chombo husika baada ya kuona hiko chombo kina rate kubwa ya viewers. TBC hawana rate kubwa unatarajia wafanye nini?

TBC hiyo ni miongoni mwa mapato yake kwanini wasichaji?
 
Hana jibu ya maswali yetu atulie tu na kukurupuka kwake! Hatun haja kusikiliza porojo!!! Tumekosea sana na tusirudie tena kw vizazi vijavyo!!!
 
Back
Top Bottom