Hivi Profesa Baregu bado yupo CHADEMA?

ego

JF-Expert Member
Apr 10, 2013
1,620
1,407
Miaka hiyo kipindi nasoma ingawa sikusoma "ungwini" lakini nilisikia mangwini enzi hizo wakisema kuna Profesa Baregu anajua kujenga hoja.

Nilijua Profesa Baregu alikuwa CHADEMA lakini hoja yangu ni kuona CHADEMA inaonyesha wazi umuhimu wa kuwatumia watu kama Profesa Baregu.

Kwa uelewa wangu mdogo ninaamini moja ya majukumu ya Katibu Mkuu wa chama ni kuongoza mwenendo wa chama.

Chama hakiwezi kuendeshwa kwa kila mtu anachokifiri kwa ufikiri wake anasimama kwenye majukwaa au vyombo vya habari na kusema hicho na sasa iwe kazi ya chama kutetea hoja wanachama wanazosema.

CHADEMA kwa sasa wanaonekana kutokuwa na mpishi jikoni, watoto wakitoka mara utamuona anatafuna maandazi barabarani, yule akitoka anakula mihogo ya kutafuna n.k

Chama cha siasa unawezaje katikati ya uchaguzi unatoa matamshi makali kwa imani na ni mtu zaidi ya mmoja

Chama cha siasa unawezaje kuchalenji good performance kwa vitu vinasound kama jokes " mfano atapigiwa kura na miradi"

Chama bila kuwa na think tank ya kutazama sera za chama, mwelekeo wa siasa zetu na kutoa gavana kwa wananchama kuwa tunakwenda kwa mtizamo huu.

Hata akitokea mmoja akapotoka basi chama kinatoka kuomba radhi na kunyoosha maneno bila kumfedhehesha msemaji lakini kwa staili ya kulinda heshima ya chama.
 
..umri umeenda kwa Prof.Baregu ku-play the role he did miaka iliyopita.

..siasa za Tz kwa upande wa upinzani zimekuwa ngumu sana, hivyo zinakatisha tamaa wasomi ambao ni established kujiunga na vyama vya upinzani.
 
Ukweli ni kuwa alipishana na mwenyekiti wa chama, akaamua akae pembeni. Ni kama alivyofanya prof.safari.
Nilichowapendea hawa hawakutukana mtu wala kutoa lugha za kejeli kwa chama chao au kwa mwenyekiti wao, bali waliambua kukaa pembeni kimya
 
Nadhani atakuwa ni kama consultant nyuma ya pazia. Hii mipango ya CHADEMA ilivo murua lazima kuna akili kubwa ipo nyuma.
 
John Mnyika ni product ya kina Prof. Baregu..

Ni kijana wa nyumbani...ndiye mwenye kujua chama kitapigaje hatua moja baada ya nyingine ili kusoma mbele...ndiye mbeba dira ama focal point ya chama.

CDM ni msingi tayari..sasa CDM inakwenda kupauliwa ili sasa watu wahamie...imeiva..

Ukitaka kujua namaanisha nini subiri kipenga ili ushuhudie mtiti..!!
 
Miaka hiyo kipindi nasoma ingawa sikusoma "ungwini" lakini nilisikia mangwini enzi hizo wakisema kuna Profesa Baregu anajua kujenga hoja.

Nilijua Profesa Baregu alikuwa CHADEMA lakini hoja yangu ni kuona CHADEMA inaonyesha wazi umuhimu wa kuwatumia watu kama Profesa Baregu.

Kwa uelewa wangu mdogo ninaamini moja ya majukumu ya Katibu Mkuu wa chama ni kuongoza mwenendo wa chama.

Chama hakiwezi kuendeshwa kwa kila mtu anachokifiri kwa ufikiri wake anasimama kwenye majukwaa au vyombo vya habari na kusema hicho na sasa iwe kazi ya chama kutetea hoja wanachama wanazosema.

CHADEMA kwa sasa wanaonekana kutokuwa na mpishi jikoni, watoto wakitoka mara utamuona anatafuna maandazi barabarani, yule akitoka anakula mihogo ya kutafuna n.k

Chama cha siasa unawezaje katikati ya uchaguzi unatoa matamshi makali kwa imani na ni mtu zaidi ya mmoja

Chama cha siasa unawezaje kuchalenji good performance kwa vitu vinasound kama jokes " mfano atapigiwa kura na miradi"

Chama bila kuwa na think tank ya kutazama sera za chama, mwelekeo wa siasa zetu na kutoa gavana kwa wananchama kuwa tunakwenda kwa mtizamo huu.

Hata akitokea mmoja akapotoka basi chama kinatoka kuomba radhi na kunyoosha maneno bila kumfedhehesha msemaji lakini kwa staili ya kulinda heshima ya chama.
Profesa Baregu ni mgonjwa wa kiharusi muda mrefu sasa.
 
Back
Top Bottom