Hili la efd mashine limeshawaumiza watu wengi, hadi inaonekana kama vile kuendesha gari nchi hii ni usaliti mkubwa.
Hii yote inatokana na kuwafanya polisi traffic kuwa wakusanya kodi wakubwa badala ya kuwa wasimamizi na waelimishaji wa sheria za barabarani. Wanapewa malengo na kutangaza mabillioni wanayokusanya. Ambayo kwa sehemu kubwa ni uonevu.
Si vibaya kuwa wakala wa kukusanya kodi kwa haki kwa ajili ya maendeleo ya nchi. Swali la kujiuliza, ni utaratibu gani au ni chombo gani kimeandaliwa Ku regulate matumizi ya efd mashine walizopewa polisi traffic, hawa waliojaa uonevu, chuki, fitina na ubabe. Ili wasizitumie kwa kuwanyanyasa wananchi kwa manufaa yao?. Wahusika waliangalie hili.