Hivi nyie watu, nini kinawafanya Mpende Pizza? sitaki hata kusikia

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,658
55,487
Habari yenu Wakuu,

Katika vyakula vinavyoongelewa na watu wengi ila mimi sielewi, ni hiki chakula kinaitwa Pizza. Hivi piza ina nini cha ziada? Nalijaribu kula mara sita sehemu tofauti hapa Dar, nikagundua pizza sio chakula ambacho kinanifaa. Ni chakula cha hovyo kwangu wala siwezi kuwa na hamu nacho.
__800x800_5481409718418.jpg

Hivi ni nini kinawafanya Mpende Pizza hadi mnashindwa kulala?

Naomba mnambie pizaa ina nini hasa hadi iwateke akili.

Mimi mwenzenu napenda Burger. Mabaga Mabaga ndo mwake. Nakula hadi najilamba vidole.

Halafu niwe na Pepsi bariiidiiii...acha kabisa.
burger.jpg

philadelhia.jpg

Napenda Burger
 
Mkikosa choo mnahangaika kwa Mzizi Mkavu kwa sababu ya ma junk food
 
  • Thanks
Reactions: BAK
We figganigga, umenikumbusha wakat nasomea Upadri nchini Uholanzi (1999 - 2004).
Ebana masista wa pale Amsterdam Cathedral walikua wanatengenezea mipiza mitamu hiyo... Unaweza kufa.
Padri wewe unachekesha hadi unakazia Uzi kwa kusema EBANA yaani umekosea sana kusema wewe ni padri.

Masista wanapika balaa acha tu.
 
wanaume wa dar wakijadili misosi yao!!

Hiyo ni misosi ya Wazungu.
Sisi Wanaume wa Dar tunakula embe kwa chumvi na limao. Chipsi zege, Mahindi ya kuchoma na pilipili, mchicha wa bonde la msimbazi, pweza na chachandu, ngisi, supu ya maharage na chapatti nk.

Karibu D'aslam......Huku Viongozi wako wakuu ndipo wanapoishi.
Hujawahi kuona kwenye tafrija zetu tunakunywa juice kwa pipi?

Kalaghabaho
 
Siwezi shangaa mtu kupenda kitu nisichokipenda ni utashi wa mtu binafsi. Ni sawa na kusema kwa nini umempenda flani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom