Hivi nikimuacha huyu mwanamke nitakuwa nimekosea?

Ok...jaribu kumpa muda labda hasira tu ndiyo anajikuta anakwambia hivyo,usikute hana hata mtu anatamani tu kulelewa.....we ukipata mihela mnunulie tu zawadi hata kama chupi ziwe nzuri mpe ,lotion anayopaka,mafuta,perfume utaona mabadiliko. Usiabase sana kwenye chakula na nyumba
ASANTE KWA USHAURI...
 
Wewe n king'ang'anizi mtu alishakuchoka na kukuacha toka zaman lakin wewe unajitia kuwa na upendo wa agape, toka kwenye kifungo hicho wewe n mwanaume tafuta hela, tafuta mwanamke mwingine, mtoto utalea hata akiwa hukohuko.

Ukijifanya kumpenda mwanamke utaumia tu, mwache aende

Sent using Jamii Forums mobile app
ASANTE KWA USHAURI...
 
Umeona hapo mara nyingi lakini hamuachani!??! anakupenda sema hasira zinamfanya aseme hivyo.
Unaonekana umzuri na unavutia sana mwanamke...umeandika kwa busara hadi kiroho cha huruma kimeniingia...ila sirudi nyuma bora nitafute mwanamke mwingine tu...mwenye akili kama zako
 
Mnamo mwaka 2015....nilipata mchumba mzuri ambaye tulipendana sana. alinipa nitakacho na nilimpa atakacho pia. kipindi nampata huyu mwanamke nilikuwa kwenye hali ngumu sana ya uchumi. alinivumilia sana na nilijiona mwenye bahati sana kumpata mwanamke mvumilivu. baada ya mwaka mmoja. alinitumia meseji kuwa ameshindwa uvumilivu na anaona bora tuachane kwasababu nimeshindwa kumuhudumia.….nilihudhuniika sana lakini tulisuluhisha yakaisha. (laitii kama ningewasikiliza wanajamiiforums walionishauri kipindi hiko yasingejirudia haya)

Mwaka 2017 nilibahatika kupata mtoto mmoja wakiume na huyu mwanamke. lakini bado Maisha yangu yalikuwa yakuunga unga, sikuwa na kazi ya maana, kwa kiasi kikubwa nilisjhindwa kabisa kumuhudumia mtoto wetu. ila kwa kuwa mwenzangu alikuwa amejishikiza kwenye shule moja hapa mjini vi jisenti vidogo vidogo vilikuwa avimpigi chenga. niliendelea kutafuta kazi bila mafanikio mwaka huo huo 2017 huyu mwanamke alinitumia tena meseji nyingine kuwa tuachane amechoshwa na mimi. roho ili niuma sana na nilihudhunika sana lakini uwezo wa kumuacha nilikosa kwani nilitamanani sana nipate kazi ili angalau nilipe fadhira zake za kunilelea mtoto wangu.
View attachment 1407640
mwishoni mwa mwaka 2019 nilibahatika kupata kazi ambayo ndio ninayoifanya hadi leo kiujumla hii kazi haina mshahala mkubwa. hivyo kuanzia mwezi wa 11 mwaka 2019 hadi mwezi huu 4 mwaka 2020 fedha yote niliyokuwa naipata ilikuwa haikidhi mahitaji, kuna kodi ya nyumba, umeme pamoja na kununua vitu vya ndani….ili ata nikiamua kuishi nae kuwe na vitu vinavyoeleweka.

Kwa ujumla wake namshukuru sana huyu mwanamke kwakuwa amenisaidia sana, amenizalia mtoto na kwa kipindi chote cha miaka 3 amekuwa akimlea mtoto wetu bila usaidizi wangu….nilitegemea sasa nimepata kazi japo si kubwa uwe ndio muda wa mimi na yeye kujipanga juu ya kujiwezesha kimaisha ila chaajabu jana amenitumia tena meseji nyingine kuwa "mimi na yeye mahusiano yetu yamefika mwisho niki penda niwe naenda tu kumuona mtoto"

Naombeni ushauri amenisaidia kweli na Zaidi ya mara 3 amekuwa akinitumia meseji za kuniacha….nimevumiliwa na nimevumilia sana...ungekuwa ni wewe upo kwenye nafasi yangu ungechukua uamuzi gani...naombeni ushauli tumia lugha yoyote ata matusi ukiweza…!
Haendi popote huyo anakupa nguvu ya kutafuta, angekuwa wa kwenda angeshachapa lapa kitambo sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom