Hivi ni uzembe wa mdomo au maksudi?

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,840
Huwa nachukia sana ninaposoma na kukutana na maneno haya
Lula badala ya Rula
Mologolo-morogoro
Foreni-Foleni
Ugari-Ugali
Kula-Kura
Nimekuwa nikijiuliza tatizo ni nini kwa watu kama hawa
Nashauri tuanze kuwapiga vita kuboresha lugha yetu ya kiswahili
Tulipiga vita X kuwa S na tumefanikiwa
Kuna mkuu anaitwa LEGE kaanzisha topic anaandika ABILIA wa makongo,Kaharibu utamu wa UZI jirekebishe MKUU
Usichukie mkuu LEGE hapa ni sehemu ya kurekebishana jombaa!
Inawezekana ni watu wavivu wa kubadilika huwezi kuwa kiongozi mkubwa wa nchi then unatumia kuongea au kuandika kwa mfano niliotoa hapo juu.
 
Last edited by a moderator:
LEGE njoo huku useme unajisikia je unavyoandika au kutamka maneno hayo!
 
Last edited by a moderator:
Tiba kama ulikuwa na mimi huyu jamaa kaaribu huo uzi mpaka nimeanzisha uzi wa kulalamika wajirekebishe eti (abilia)
 
Last edited by a moderator:
Matamshi yanatabia ya kuadhiriwa na geographical location ya mzungumzaji ila linapokuja suala la uandishi napata taabu kidogo kuelewa ni bahati mbaya ama ni mbwembwe za uandishi!
 
fungi kwa nafasi aliyonipa Kibo10 ya makamu mwenyekiti naomba urekebishe neno ilo kuwa hilo na Zamaulid tafadhali fanya marekebisho katika post yako maana makosa yamezidi
 
Last edited by a moderator:
Hao wengine naweza kuwatetea kwamba athari za mazingira na makabila zina waathiri kuongea na kupelekea hata uandishi wao kuwa hivyohivyo kama wanavyozungumza. Makabila mengi ni jambo la kawaida kabisa kuweka R ilipostahili L wanapozungumza kiswahili.

Tatizo langu kubwa ni wale wanaotumia xaxa wakimaanisha sasa. Inanipa shida kujua lengo ni kufupisha au ni kitu gani.
Kwanza naona haingii akilini kufupisha sasa kwa kuandika xaxa.
 
Back
Top Bottom