Hivi ni sahihi kumuita mwanangu jina la x girl wangu?

tang'ana

JF-Expert Member
Apr 3, 2015
11,928
15,803
Habari za siku nyingi enyi watanganyika wenzangu?mpenzi wangu kajifungua mtoto wa kike,nilikua naomba kujulishwa kama ni sahihi kumuita jina linalofanana na la x wangu ambaye tuliachana in good terms baada ya kushindwana mambo flani flani.
 
Jina ni jina tu mkuu, lakini kama unaona litaleta mtafaruku kwa huyo mzazi mwenzio tafuta lingine tu yapo mengi.
 
usithubutu kumfanyia huo ukatili mkeo/mpenzio mimba abebe mwenyewe jina la mtoto apewe la x hivi unafikiri akijua itakuwaje, wengine huwa mnachokaga kuwa na amani then mnaanza kusema ndoa ndoa ni changamoto!!
 
Nipe namba ya Mke wako kwanza halafu ntarudi kukushauri, na usije ukaniita mie mmbea, hilo ni swali gani unakuja kuuliza?? ingekuwa yeye amezaa wa kiume halafu akamuita x wake ungejisikiaje? wanawake ni wa kimya ila wana visasi vibaya mno, wewe utaleta jina la X yeye ataleta Mtoto wa pili wa X wake, hapo utakoma.
 
usithubutu kumfanyia huo ukatili mkeo/mpenzio mimba abebe mwenyewe jina la mtoto apewe la x hivi unafikiri akijua itakuwaje, wengine huwa mnachokaga kuwa na amani then mnaanza kusema ndoa ndoa ni changamoto!!
Hivi kwanza haoni kama ni laana...
Yanii demu aliyekua anamla kumbukumbu ibakie kwa mtoto wake wa kike.... huu ni ubakaji mkubwa wa haki za watoto
 
Back
Top Bottom