Hivi ni nini maana ya mwanaharakati? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi ni nini maana ya mwanaharakati?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Jembe Wa Majembe, Aug 10, 2012.

 1. J

  Jembe Wa Majembe New Member

  #1
  Aug 10, 2012
  Joined: Aug 9, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimejiuliza swali hili kutokana na unafiki wa hali ya juu ambao wanaojiita wanaharakati wamekua wakiuonesha.
  Kipindi cha mgomo wa madaktari, hawa wanaojiita wanaharakati walikaa kimya huku wakishuhudia wananchi mamia kwa mamia wakifa kwa ajili ya mvutano kati ya serekali dhaifu ya CCM na Madaktari wauaji chini ya uongozi wa Dr. Ulimboka. Lakini siku Ulimboka alipokutwa mabwepande akiwa kapigwa na kung'olewa meno, ni hawa hawa wanaharakati waliokuwa mstari wa mbele kulizungumzia hili jambo kama vile Ulimboka ndio alozaliza sana na mwanamke. Hivi wale wagonjwa walokufa kule mahospitalini kwa sababu ya huu mgomo walijambwa halafu ulimboka ndo alizaliwa saana? Si mngekaa kimya kama mlivyokaa kimya toka awali?Halafu kuna huyu mama anayeitwa Hellen Kijo Bisimba ndo mnafiki na opportunist wa kwanza.
  Hivi, maana halisi ya uanaharakati ni nini kama siyo kupigania haki ya kuishi ya mwanadamu? Nilichotegemea siyo hawa wanaharakati waisapoti serikali wala madaktari, bali at least wangelaani kitendo cha serikali na mdaktari kuwaacha wagonjwa wasio na hatia wafe kwa ajili ya wao kutunishiana misuli.Lakini hawa wanafiki wetu ndio walikua mstari wa mbele kuhamasisha migomo ya madaktari ili watu wazidi kufa.
   
 2. N

  Nali JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2012
  Joined: Mar 31, 2010
  Messages: 826
  Likes Received: 248
  Trophy Points: 60
  Mwanaharakati maana yake ni mtetezi wa haki za binadamu! Upo?

  Wanaharakati nikiwemo mie na huyo ulomkashfu Mama kijo bisimba walitumia haki yao ya kikatiba kabisa kuhakikisha serikali inawapatia madaktari mahitaji yao ya msingi ili kuepusha migomo isiyo ya lazma! Serikali dhaifu, dhalimu na ya mauaji ya ccm ikakataa matakwa na mahitaji ya madaktari! Sasa kwa mujibu wa katiba ya nchi yetu; haki moja wapo ni haki ya kuandamana kudai haki. Hilo limefanyika baada ya gvnmnt kukataa madai ya madaktari! So hapakuepo na njia nyingine ya kufanya zaidi ya kuandamana kudai haki hiyo! So km hii serikali ingekua sikivu basi hayo yoote yasingetokea hakika!

  So, mwanaharakati ni mzalendo, mpigania haki za watu,mtetezi mwema na mkweli! Wewe ni nani na unasimama katika ukweli upi katika hoja yako?!!!!
   
Loading...