Hivi ni nani alaumiwe endapo vijana wengi hawataoa na kuolewa?

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,215
3,682
Katika maisha ya sasa kila kijana ana ndoto za kuoa na kuolewa kwa yule anayempenda.

Lakini kuna kautafiti nimekafanya kanaonyesha dhahiri ni kwamba vijana wengi wa kiume wamekuwa waoga kuingia katika maswala ndoa kutokana na hali halisi ya maisha.

Sio hivo tuu vijana wengi pia wamekuwa waoga kuanzisha mahusiano na wakina dada na hii inatokana na mifumo ya kimaisha ya wadada wengi kuwa tegemezi kwa mwanaume ambapo kila kitu anategemea kumuomba mwanaume ikiwemo swala la fedha ambapo vijana wengi wenye kipato kidogo huwa linawashinda kuhudumia.

Hali ya maisha kuwa ngumu pia na vijana wengi wa kiume kuogopa majukumu toka kwa watoto wa kike ambapo wengi vijana hukimbia majukumu kutokana hali ya uchumi wa kipesa ilivyokuwa ngumu na vijana wengi wa kiume kuogopa kusalitiwa na wapenzi wao kutokana uchumi kuwa mgumu.

Wakati hayo yakiendelea wadada wengi miaka ya hivi karibuni wamekuwa wakionekana kukesha katika nyumba za ibada kuomba kupata mke mwema, lakini pia kuna wengine wadada wamefikia hadi hatua ya kwenda kwa waganga ili waweze kupata mume kuna wengine wanafikia hatua hadi kutongoza wanaume.

Sasa shida inayokuja ni kwamba kwa wanaume wamekuwa wakiogopa majukumu na wadada nao wamekuwa wakitafuta mume

Je huko tunakoelekea hali inaonyesha dhahiri mambo kubadilika?

Je unadhani ni nani wa kulaumiwa endapo ndoa zitazidi kupungua siku hadi siku?
 
c1b6a5be829fddcb21919f8ee036725c.jpg
 
Nini kinasababisha mtu kuoa au kuolewa...ukisha faham kisababishi...utapata jibu lako
 
Kwa tabia hizi za kuchepuka zimekuwa kama fasheni haswa huku mjini mimi binafsi nimeachana na wife baada ya kuthibitisha kuwa amezini na jamaa aliekuwa nae mwanzoni kabla sijamuoa,sasa jiulize mtu nimeishi nae ktk ndoa miaka kumi kumbe mke nna share na jamaa aisee nawashauri vijana kama unataka mrithi tieni mimba mlee watoto wanawake hawafai msioe.
 
sasa hapo mbona unakatisha watu tamaa kuhusu ndoaaa
 
Kwa tabia hizi za kuchepuka zimekuwa kama fasheni haswa huku mjini mimi binafsi nimeachana na wife baada ya kuthibitisha kuwa amezini na jamaa aliekuwa nae mwanzoni kabla sijamuoa,sasa jiulize mtu nimeishi nae ktk ndoa miaka kumi kumbe mke nna share na jamaa aisee nawashauri vijana kama unataka mrithi tieni mimba mlee watoto wanawake hawafai msioe.

Hapo ndio wanawake wanapoharibu
 
Tatizo akina dada wanataka kuolewa na wenye fedha, hawataki shida ingawaje wengi wao wamezaliwa na kukulia kwenye shida!!
ni kweli kabisa usemalo ila shida ni kwamba muda wa kuoa unafika lakini watu tumekuwa tukiogopa ndoa
 
lakini kaka hivi unafahamu kuna umri ukifikka kama hutaonekana umeowa au kuolewana jamii huwa inakuchukulia wewe kama muhuni
Huo ni mtazamo wa jamii na ndio wengi huwa tunakosea yanapotokea majanga jamii haikusaidii kitu unabaki wewe na mkeo msikubali kuoa kwa shinikizo la jamii naongelea ndoa nyakati hizi hazina mpango wanawake wamebadilika
 
Kwa tabia hizi za kuchepuka zimekuwa kama fasheni haswa huku mjini mimi binafsi nimeachana na wife baada ya kuthibitisha kuwa amezini na jamaa aliekuwa nae mwanzoni kabla sijamuoa,sasa jiulize mtu nimeishi nae ktk ndoa miaka kumi kumbe mke nna share na jamaa aisee nawashauri vijana kama unataka mrithi tieni mimba mlee watoto wanawake hawafai msioe.
lakini kaka hivi unafahamu kuna umri ukifikka kama hutaonekana umeowa au kuolewana jamii huwa inakuchukulia wewe kama muhuni
ndoa imepoteza maana japo zinaa mungu hataki
 
Yanayoendelea kwenye ndoa nyingi hakuna mwenye uharaka wa kukimbilia kuoa cku hizi,ukipata majanga jamii haitakusaidia utapambana na hali yako.
 
lakini kaka hivi unafahamu kuna umri ukifikka kama hutaonekana umeowa au kuolewana jamii huwa inakuchukulia wewe kama muhuni
hupaswi kuishi kwa kuangalia jamii unakuangalia vipi...hapa ndo wengi wetu tunafeli...tunaishi kisaniii......Ishi kiuhalisia,,, wewe ndo unaejijua....unataka kuoa/kuolewa coz fulani ameoa/kaolewa.... vijana wengi mtaishia kulia sana,,, kuwa halisi, ishi in real.....jamii itakukubali tuu....
 
Back
Top Bottom