Baada ya Tanganyika kupata uhuru mwaka 1961, Hayati Mwalimu J.K Nyerere alimuita kinara wa kupigania uhuru wa msumbuji Dk. Edwardo Mondlane na alimpa nyumba Msasani iliyokuwa karibu na nyumba yake kwa lengio la kumsaidia kupigania uhuru wa Msumbiji.
Mwalimu Nyerere alimsaidia Dk. Mondlane kuanzisha Chama cha ukombozi cha Msumbiji (FRELIMO). Chama cha FRELIMO kilianzishwa katika ukumbi wa Karemjee jijini Dar Es Salaam, inawezekana vijana wa sasa wa msumbuji hawalijui hili au uhuru walionao leo umewalevya na kusahau walikotoka.
Tanzania iliwapa mafunzo ya kijeshi vijana wa msumbiji katika kambi mbalimbali nchini Tanzania zikiwemo za morogoro, Iringa, Mbeya nk, Tanzania iliwapa hifadhi ya makazi pamoja na elimu dunia wapinia uhuru wengi sana wa msumbiji ili baada ya kupata uhuru watu wa msumbiji waweze endesha serikali yao wao wenyewe.
Tanzania imetoa sadaka ya damu ya wanajeshi wazalendo wake katika nchi ya msumbiji ili msumbiji liwe taifa huru, kwa Lugha Nyepesi uhuru wa Msumbiji walionao leo umekamatwa na damu ya watanzania. Hayo ni machache kati ya mengi tuliyowafanyia Msumbiji.
Kwa yanayoendelea Msumbiji kwa sasa dhidi ya watanzania hayapaswi wala hayakupaswa kufanya na watu wa msumbiji. Sikatai kuwa msumbiji ina taratibu zake za kukaa nchini humo ila je kweli ndo mtuue, mtubake,mtunyang’anye mali zetu na kutufanyia unyama wa kila aina tena bila kubagua wenaoishi kwa halali na wele wasioishi kwa halali, hapana hii haikubaliki hata kidogo.
Inawezekana Msumbiji wamesahau fadhila za Tanzania kwao ila je wamesahau pia kuwa kuna ndugu zao tunaishi nao Tanzania? ..isije baadae ikawa mkuki kwa nguruwe.
Najua serikali inafuatilia sana jambo hili na wanafanya kila liwezekanalo katika hili ila tafadhali sana tuongeze kidogo ukali katika hili na ikiwezekana tuwashtaki msumbiji kwa kutuulia raia wetu, kuwabaka na kuwadhalilisha watanzania katika mahakama za kimataifa.