Hivi ni lini viongozi wetu wataona umuhimu wa kujiuzulu madudu yakifanyika?

Ustaadh

JF-Expert Member
Oct 25, 2009
413
19
Bosi Takukuru atakiwa ajiuzulu

MBUNGE mteule wa Wawi, Hamad Rashid Mohamed (CUF), amesema hatua ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kumsafisha Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Serikali, Andrew Chenge, ni aibu kwa Taifa na kwa taasisi hiyo, hivyo Mkurugenzi wake Mkuu, Dk. Edward Hoseah anatakiwa ajiuzulu.

Akizungumza jana na waandishi wa habari mjini hapa, Hamad alisema ilichofanya Takukuru ni aibu na inawafanya wananchi wakose imani na taasisi hiyo yenye majukumu makubwa ya kupambana na ufisadi nchini.

"Hiki kilichofanywa na Dk. Hoseah ni aibu kwa Taifa, hatuwezi kwenda hivi kama Taifa lililodhamiria kupambana na ufisadi...huyu mtu lazima aachie ngazi," alisema Hamad.

Alisema kama Dk. Hoseah atakataa kuachia ngazi kwa hiari yake, ni vyema Rais Jakaya Kikwete amwajibishe ili kuongeza imani kwa wananchi juu ya taasisi hiyo nyeti.

Aliongeza kuwa kitendo cha Takukuru kutangaza kuwa Chenge hana hatia katika kashfa ya ununuzi wa rada, kinaonesha taasisi hiyo ilivyo tayari kuwasafisha wanasiasa hasa wale ambao wanatuhumiwa na makosa mazito ya ufisadi.

Alisema hii ni mara ya pili kwa Takukuru kuwasafisha wanasiasa na alitoa mfano wa kashfa ya kampuni ya kufua umeme wa gesi ya Richmond ya Marekani namna ilivyoitia hasara Taifa; lakini taasisi hiyo ikatangazia umma kuwa hakukuwa na harufu ya rushwa wakati wa zabuni ya kununua mitambo ya kufua umeme.

Hata hivyo, Bunge lililazimika kuunda Kamati Teule ya Bunge baada ya vyombo vya habari kutangaza ufisadi uliokuwapo katika kuipa kampuni hiyo zabuni ya kuzalisha umeme wa megawati 100.

Kamati hiyo teule iliwatia hatiani baadhi ya mawaziri na maofisa wa Serikali hatua iliyosababisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu kwa kuwajibika.

Hamad alisema Rais Kikwete ni lazima apunguziwe mizigo ya viongozi wabovu kwani wanachofanya ni kulinda maslahi ya baadhi ya wanasiasa na kuweka ukweli pembeni.

"Sasa hivi wananchi wanaona kama Takukuru hawaisaidii katika kupambana na ufisadi, umefika wakati tunataka kuona watu wanawajibika," alisema Hamad ambaye katika Bunge lililopita alikuwa ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani inayoelezwa kufanya vizuri katika kupinga mambo ya ufisadi.

Hivi karibuni taasisi hiyo ilitoa taarifa kwa vyombo vya habari ikimsafisha Chenge kuwa haikuona ushahidi wowote unaotosheleza yeye kutiwa hatiani katika kashfa hiyo ya ununuzi wa rada.

Taarifa hiyo ilitolewa na Ofisa Habari wa Takukuru, Doreen Kapwani kwa niaba ya Dk. Hoseah.

Takukuru ilitoa taarifa hiyo siku moja baada ya Chenge kukutana na wahariri wa vyombo vya habari na kutangaza nia yake ya kuwania uspika na alipoulizwa juu ya tuhuma za ufisadi zinazomkabili hasa kashfa ya ununuzi wa rada, alitamba kuwa tayari Takukuru na SFO ya Uingereza wameshamtakasa.

Hata hivyo, Ubalozi wa Uingereza nchini juzi ulitoa taarifa kwa vyombo vya habari ukieleza kuwa kwa sasa haifai kusema kuwa Chenge hana hatia, kwani suala hilo liko katika hatua za awali za kufikishwa mahakamani taarifa ambayo inapingana na ya Takukuru.

My take:
Ukiondoa Mzee Mwinyi ambaye alijiuzulu miaka ya nyuma kutokana na mauaji ya Shinyanga kama sikosei, hakuna kiongozi aliyewahi kuwajibika kwa madudu yaliyofanyika chini ya 'himaya' yake. Lowassa nadhani yeye alilazimishwa kujiuzulu si kwa hiari yake. Kuna haja ya viongozi wetu kuiga viongozi wa mataifa mengine ambapo likitokea jambo kubwa wewe kama kiongozi unabeba dhamana ya madudu ya eneo lako na kwa kufanya hivyo unajijiengea heshima.
 
Back
Top Bottom