Hivi ni lini tutapata Rais atakewekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,684
149,889
Hivi sisi tunajua kweli kutumia rasimali zetu kujiletea maendeleo?

Tunajua kweli tunatakiwa tuwe na vipaumbele katika maeneo gani ili tutoke hapa tulipo?

Hivi ni kwanini hatufikirii kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji wakati tuna ardhi kubwa yenye rutuba na vyanzo luki vya maji?

Ni lini tutapata Raisi atakeona fahari kuzindia irrigation system za kisasa katika nchi yetu zilizokuwa funded na serikali?

Ni lini tutapata kiongozi atakeweka kipaumbe katika kutoa ruzuku/mikopo kwa wakulima kuwezesha kilimo cha aina hii?

Hivi sisi tukoje?

Elimu zetu ni za kwenye makaratasi tu?

No wonder chuo kikongwe kama UD chenye wasomi na rasilimali kubwa ya ardhi bado kinaona fahari kujengewa hostel na serikali.
 
Tunamito inatiririsha maji toka nyanda za juu kusini mpaka yanaingia Bahaini tunayaangalia tu.tunasubiri mvua za msimu
 
Mkuu umeleta changamoto kuntu ambayo inatakiwa isemwe na wabunge wa upinzani...na sio blah blah za ujuaji kuhusu TISS
 
Ukweli mchungu ni kwamba tuna maji mengi sana katika nchi yetu lakini kwa utawala huu tusitarajie uwekezaji kwenye irrigation schemes ambazo zingeongeza uzalishaji kwa ajili ya chakula na biashara; tena hata hizo dream liners tungezinunua bila hata kuongeza deni la taifa.

Anywa, by the time tunamaliza kulipia dream liners (ambazo kimsingi si hitaji la jamii) na kujenga flyovers, miaka itakuwa imekwenda sana na izo ndo priorities kwa sasa. Inasikitisha lakini huo ndiyo ukweli na sisi wenyewe ndo wa kulaumiwa!
 
CCM na CDM mmefanya dhambi kubwa katika uchaguzi uliopita matokeo yake tunapata viongozi wa kubahatisha wanaojua kuendesha malori badala ya basi au meli au treni kwa ajili ya abiria. Ni kosa linalotaka kukaribiana na la 2005. Katika uchaguzi uliopita Bernard Membe alijiandaa vizuri sana kuwa Rais wa nchi yenu tena aliyejua matatizo ya nchi kwa uhalisia. Pamoja na kutokulia mjini, lakini amepata elimu yake katika chuo bora kabisa duniani. He is really good and bright. Network ya Alumni ya chuo chake (like Business tycoon Michael Bloomberg) pekee ni fursa tosha ya ku-access fursa za kiufundi na reforms zinazohitajika katika dunia ya leo.

Alikuwa anajua nini kimepungua katika uwamu ya 4, alijiandaa kuja na sera ya umeme kila kaya, Irrigation Scheme kila kijiji, Chuo cha Teknolojia na Ubunifu kila Wilaya. Alikuwa na plan kubwa ya kuleta wawekezaji wakubwa kwenye kilimo na Viwanda. Tayari alishakuwa na orodha ya nchi ambazo zilikwishakubali kumpa teknolojia ya viwanda, uzalishaji na ubunifu. Aliamini kwenye ushirikiano na mataifa yaliyoendelea katika kuharakisha maendeleo kama nchi zote za Asia zilivyofanya. Ukifuatilia media utadhani China na US ni maadui lakini biashara na ushirikiano wa teknolojia, elimu na ubunifu katika ya China na Marekani namna ulivyo mkubwa, utashangaa. Cha ajabu dereva wenu wa Lori ameaminishwa kila tajiri ni mwizi, mpiga dili, hivyo anapaswa kuchukiwa. Mtu anayeamini kwenye userikali pekee huku akijinasibu kuongeza ajira, sijui ajira za u DC.

Mkaaminishwa na wajinga wachache kuwa Membe ni zao la Kikwete, mkampiga fitna matokeo yake mmepata dereva wa Lori mnalalamika kutwa kucha. Subirini lori likikaribia kitonga ndio mtamjua vizuri dereva. CCM na Chadema dhambi hii itawaandama na itawaadhirisha mpaka mwisho wa uhai wenu. Staki siasa.
 
Tukimalzak Akimalza teua tengua , kutumbua vijipu&kuyaacha majipu(BASHITE)ununuz wa bombardier, kuwafanya muishi kama mashetani na kuweteka atarudi kwenye kilimo cha umwagiliaji
 
"Ngoja nchi inyooke kwanza mana ilipinda sana toka marais wote wanne waliopita"i thnk in magufuli voice
 
CCM na CDM mmefanya dhambi kubwa katika uchaguzi uliopita matokeo yake tunapata viongozi wa kubahatisha wanaojua kuendesha malori badala ya basi au meli au treni kwa ajili ya abiria. Ni kosa linalotaka kukaribiana na la 2005. Katika uchaguzi uliopita Bernard Membe alijiandaa vizuri sana kuwa Rais wa nchi yenu tena aliyejua matatizo ya nchi kwa uhalisia. Pamoja na kutokulia mjini, lakini amepata elimu yake katika chuo bora kabisa duniani. He is really good and bright. Network ya Alumni ya chuo chake (like Business tycoon Michael Bloomberg) pekee ni fursa tosha ya ku-access misaada ya kiufundi na reforms zinazohitajika katika dunia ya leo.

Alikuwa anajua nini kimepungua katika uwamu ya 4, alijiandaa kuja na sera ya umeme kila kaya, Irrigation Scheme kila kijiji, Chuo cha Teknolojia na Ubunifu kila Wilaya. Alikuwa na plan kubwa ya kuleta wawekezaji wakubwa kwenye kilimo na Viwanda. Tayari alishakuwa na orodha ya nchi ambazo zilikwishakubali kumpa teknolojia ya viwanda, uzalishaji na ubunifu. Aliamini kwenye ushirikiano na mataifa yaliyoendelea katika kuharakisha maendeleo kama nchi zote za Asia zilivyofanya. Ukifuatilia media utadhani China na US ni maadui lakini biashara na ushirikiano wa teknolojia, elimu na ubunifu katika ya China na Marekani namna ulivyo mkubwa, utashangaa. Cha ajabu dereva wenu wa Lori ameaminishwa kila tajiri ni mwizi, mpiga dili, hivyo anapaswa kuchukiwa. Mtu anayeamini kwenye userikali pekee huku akijinasibu kuongeza ajira, sijui ajira za u DC.

Mkaaminishwa na wajinga wachache kuwa Membe ni zao la Kikwete, mkampiga fitna matokeo yake mmepata dereva wa Lori mnalalamika kutwa kucha. Subirini lori likikaribia kitonga ndio mtamjua vizuri dereva. CCM na Chadema dhambi hii itawaandama na itawaadhirisha mpaka mwisho wa uhai wenu. Staki siasa.
Kinachokera na kuudhi ni kuona baadhi ya watanzania wenzetu hawafuatilii wala hawajali ni nini kinaendelea ila wakati wa uchaguzi ndio wako mstari wa mbele kupiga kura.

Siuji kwanini nilizaliwa katika hii nchi!!
 
Kwa hakika hili ni kosa kubwa. Kwao uchaguzi ni kama tukio la kiutamaduni tu, hawajui thamani halisi ya uchaguzi ni nini. Yaani wanaamini uchaguzi ni formalities tu na haina athari katika maisha yao. Ila kuanzia 2020, watu watajua kwamba kumbe uchaguzi una athari katika maisha yao. Wacha waisome namba ili wapate adabu.
 
"Ngoja nchi inyooke kwanza mana ilipinda sana toka marais wote wanne waliopita"i thnk in magufuli voice
Nchi haikupinda hata kidogo, kulikuwa na changamoto za kisera tu na kitaasisi ambapo JK aliziweka vizuri. Kilichotakiwa na kiongozi badala ya JK ni uwezo mzuri wa kusimamia taasisi, nidhamu na priority-based plans. Bahati mbaya tumempata mtu ambaye haamini katika taasisi. Very sad.
 
Back
Top Bottom