Hivi ni kweli tunategemea mzungu kulipa mshahara?

Hivi ni kweli tunategemea mzungu kulipa mshahara?

SAIZI YANGU

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2013
Posts
381
Reaction score
83
Katika Video hii Rais Uhuru anasema Tanzania, Uganda na nchi nyingine katika ukanda huu zinapata zaidi ya 40% ya recurring budget kutoka kwa wazungu. Hivi ni kweli?? Tunategemea mzungu kulipa mshahara? Anajua recurring budget ninini kweli.... Ni nawazo tu
 
Attachments

Ni kweli yupo sahihi
Mi hizo habari nilizisoma kwenye global economic forum
 
Katika Video hii Rais Uhuru anasema Tanzania, Uganda na nchi nyingine katika ukanda huu zinapata zaidi ya 40% ya recurring budget kutoka kwa wazungu. Hivi ni kweli?? Tunategemea mzungu kulipa mshahara? Anajua recurring budget ninini kweli.... Ni nawazo tu
sasa hujamwelewa kitu gani hapo, panya wa ciciyenu wamekula na kuuza rasilimali za nchi hii miaka yote bila hata huruma; na kwa sababu ya mikata hovyo iliyoko kwenye nishat na madini, sahau kabisa nchi hii kujitegemea kibajeti labda ciciyenu ife.
 
Tatizo la bajeti kwa nchi zetu ni dogo mno ukilinganisha na ukabila uliokubuhu kenya.Kenyatta amalize kwanza tatizo la ukabila nchini kwake aachane na sisi.Ya kwetu hayamhusu aache umbeya.
 
Mkuu mantiki ipo,utakula ulichopanda,sio mambo ya mbuzi kula kutegemea urefu wa kamba yake.
Ukubwa wa serikali haulingani au haufanani na mapato ya serikali.Tuna wabunge wengi kupita kiasi,tuna mikoa na wilaya ziliongezwa kisiasa.Vile vile matumizi mabovu ya pesa za umma ndio kisiki cha maendeleo kwa muda mrefu sasa,labda Magufuri ataondoa hilo.
Kama haitoshi vipaumbele vya maendeleo havikupewa msukumo,msukumo upo kwenye chaguzi sababu kuna pesa za wafadhili.
Raisi Kenyatta anatutambia kwa sababu asili mia kubwa ya bajeti ya Kenya kwa muda mrefu haitegemei wafadhili kama Tanzania na Uganda,ni pesa ya ndani yaani kodi
 
Tatizo la bajeti kwa nchi zetu ni dogo mno ukilinganisha na ukabila uliokubuhu kenya.Kenyatta amalize kwanza tatizo la ukabila nchini kwake aachane na sisi.Ya kwetu hayamhusu aache umbeya.

Tehe teheee....Kaukweli bwanaa siku zote kanauma, halafu hakaangalii cha mfia Lumumba wala nini....just truth and only truth...
 
Back
Top Bottom